Jun 25, 2012

BONDE FC NI MABINGWA WAPYA WA BEIRA YOUTH CUP 2012

Timu ya Bonde fc jana iliibuka kuwa mabingwa wapya wa  BEIRA YOUTH CUP 2012 ubingwa huo umepatikana baada ya kuibuka na ushindi wa gili 5-4 dhidi ya New Boys ya Ilala.

Ilibidi mpaka matuta ndio yaamue nani bingwa kwani katika muda wa kawaida timu zote zilitoka sare ya bila kufungana.

Akiongea na chumba cha habari kocha wa timu ya Bonde Fc alisema kuwa Timu yake il;istahili ubingwa huo kutokana na maandalizi waliyofanya kwani michuano hiyo ilikuwa ni migumu sana kutokana na timu zilizoshiriki michuano hiyo.

Pia alitoa pongezi kwa uongozi mzima wa Beira kwa kuweza kuanda michuano kama ile yenye kushirikisha vijana wa umri mdogo kwani ni nadra sana kwa nchi hii watu kuandaa michuano ya umri mdogo hasa u14, u17, u21 kama walivyofanya wao.

Pia aliwataka vijana watu wengine wenye nia na kuendeleza soka la vijana kujitokeza na kuanzisha ligi za vijana ili kuondokana na vijana wengi kuishia kwenye mambo ya kihuni na huku wanavipaji vya kucheza soka.

Nae katibu wa michuano hiyo ndugu Richard alisema baada ya kumalizika kwa michuano hiyo ya vijana chini ya miaka 21 sasa wanajianda kuanzisha ligi ya wachezaji wasiocheza ligi kuu ili nao wapate nafasi ya kucheza.