Dec 30, 2011

BONDE FC KUANZA MAZOEZI SIKU YA JUMATATU

  na shabani kpl

Juu na chini ni vijana wa bonde fc wakijifua kabla ya mechi















Timu ya Bonde fc inawatangazia mashabiki na wanachama wake kuwa itaanza  mazoezi rasmi siku ya jumatatu. Akiongea na chumba cha habari kocha mkuu wa Bonde fc ndugu Issa Joseph  amesema kuwa wataanza mazoezi rasmi siku hiyo ikiwa ni baada ya mapumziko ya sikukuu xmss na mwaka mpya hata hivyo kocha huyo alizidi kukipasha chumba cha habari kuwa mazoezi hayo watakuwa wakifanyia katika uwanja Magomeni Tuliani kufuatia uwanja wao wa nyumani kukumbwa na mafuriko hivyo amewahasa wachezaji kufika mazoezini siku hiyo pia wanawakaribisha mashabiki wa soka kuja kushuhudia 
 

Dec 14, 2011

Kampuni ya 2F CO.LTD YAJITOSA KUIDHAMINI BONDE KIDS

 Picha juu na china mmoja wa wakurugenzi wa 2F CO.LTD mwenye kanzu akiwa  na viongozi pamoja na wachezaji wa Bonde Fc siku ambapo Bonde fc ilishinda mechi yake ya nusu fainali .
2F CO.LTD imejitolea kuisaidia timu ya Bonde Kids.  Itakuwa ikiisaidia Bonde Kids katika vifaa vya michezo zikiwemo jezi na masuala mbalimbali yanayohusu kuindeleza timu 
Pia kampuni ya 2F CO.LTD kupitia kwa mmoja wa wakurugenzi wake Bwana SALM NGINGO pia imewataka watu wengine wenye uwezo kujitokeza katika kuisaidia timu kwani kusaidia timu kama hizi ndio kusaidia kukuza soka la nchi yetu. Nao uongozi mzima wa Bonde Kids unatoa shukrani kwa kampuni ya 2F CO.LTD kwa uamuzi wao wa kuamua kidhamini timu yao pia wanawaomba watu wenye nia nzuri na soka la vijana kujitokeza kuzisaidia timu kama hizi zenye malengo ya kuinua soka la vijana.

SIKU BONDE FC ILIPOINGIA NUSU FAINALI TA TEWA CUP

 Kikosi cha Bonde Fc kikiwa katika ukaguzi kabla ya mechi ya nusu fainali  dhidi ya Makumbusho Talent Bonde fc iliibuka na ushindi wa 6-5 magoli yaliyopatikana kwa njia ya kupigiana mikwaju ya penati baada ya kutoka nguvu sawa katika muda wa kwaida chini ni kikosi kamili cha Bonde Fc na makocha wao .kulia ni kocha mkuu Issa Joseph na kushoto ni Rashid Banda kocha msaidizi.  

Hiki ni kikosi cha Makumbusho Tarent ambacho kilifungwa na Bonde fc katika mechi ya nusu fainali

Dec 13, 2011

BONDE FC YAJITOA MASHINDANO YA DAYOSA

 
 Siku Mwinyimaji Tambaza alipoitembelea Bonde fc mazoezini hakuna alietegemea kama iko siku atatugeuka
 
 
 
 
Timu ya Bonde Fc inawatangazia mashabiki wake kuwa imeamua kujitoa katika michuano ya DAYOSA kutokana na ukiritimba na ufisadi unaofanywa na katibu wa chama hicho ndugu Mwinyimaji Tambaza kwa kitendo chake cha kuzifungia timu za Shein Rangers na Bonde fc zisishiriki michuano ya aina yoyote inayoandaliwa na chama hicho na hata kutotakiwa kucheza mechi za kirafiki na timu yeyote unayoshiriki michuano inayoandaliwa na chama hicho sasa tunajiuliza hivi huyu jamaa kazi yake kuendeleza soka au kuua vipaji vya vijana.kwani alikwisha wahi kumshawishi ndugu Ibrahimu Tewa kuifuta Shein katika michuano ya TEWA CUP baada ya shein kugoma kushiriki michuano ya DAYOSA inayoendelea kutokana na ukilitimba wa kiongozi huyu

Nov 22, 2011

Muundo wa kampuni ya ligi Kuu

          Muundo wa kampuni ya ligi Kuu
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Ligi kuu TPL atakuwa kiongozi wa Juu wa Klabu iliyoshinda ubingwa Ligi Kuu msimu uliotangulia
Makamu wenyeviti watatu wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya ligi kuu TPL ni (viongozi wa juu wa timu mbili zilizoshika nafasi ya pili na tatu na Makamu wa pili wa Rais TFF anayewakilisha vilabu
Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Ligi kuu inahusisha wenyeviti au wakurugenzi au kiongozi wa juu wa vilabu vyote 14 (16) vinavyocheza ligi kuu, (kila klabu itatoa mjumbe mmoja) TFF pia itakuwa na hisa kwenye kampuni ya ligi kama klabu na itakuwa na mjumbe mmoja kwenye bodi ya wakurugenzi wa kampuni. Wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya ligi ambao hawatapiga kura ni pamoja na Mjumbe mmoja toka chama cha wanasoka wa kulipwa, chama cha waamuzi FRAT, chama cha makocha TAFCA na Wadhamini wa ligi kuu
Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya ligi inapaswa kukutana wiki ya mwisho ya mwezi July (kabla ligi haijaanza) na wiki ya mwisho ya mwezi Januari (kabla raundi ya pili haijaanza )kila mwaka
Wajumbe wa kamati tendaji wa kampuni ya ligi inahusisha angalau kiongozi mmoja wa kila timu inayoshiriki ligi kuu, mwakilishi kutoka shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF, chama cha makocha, chama cha waamuzi, na wawakilishi toka kwa wadhamini ambao hawatakuwa na nguvu ya kupiga kura. Wajumbe wa kamati hizi wanapaswa kukutana angalau kila baada ya miezi miwili.
Kamati kuu ya TPL inahusisha Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa TPL, Makamu wenyeviti wa bodi ya wakurugenzi wa TPL, na wajumbe watatu watakaochaguliwa na bodi ya wakurugenzi. Kazi kuu ya kamati kuu ya TPL ni kuhakikisha sera zilizopitishwa na TPL zinatekelezwa na secretariet ya TPL.
Kamati ya Ufundi na Maendeleo ya TPL itahusisha mameneja na makocha wakuu wa vilabu vyote vinavyocheza ligi kuu na Mkurugenzi wa ufundi TFF kama wapiga kura sambamba na Mwakilishi wa chama cha makocha, na chama cha wachezaji wa kulipwa ambao hawatapiga kura.
Kutakuwa na kamati huru ya nidhamu na rufaa ambayo itateuliwa na Bodi ya wakurugenzi ya TPL kila mwaka. Maamuzi ya kamati hii yatapaswa kutekelezwa na klabu zote zinazoshiriki ligi kuu lakini yanaweza kupigwa kwenye kamati ya nidhamu na Rufaa ya TFF.
Wajumbe wa kamati nyingine za TPL watateuliwa na bodi ya wakurugenzi wa TPL

Uhusiano kati ya TPL na TFF



Makamu wa pili wa Rais TFF atapaswa kuwa mmoja wa makamu wenyeviti wa bodi ya wakurugenzi wa TPL lakini pia uchaguzi wa makamu wa rais wa TFF utafanywa na Bodi ya Wakurugenzi wa TPL au UTAFOC na kiongozi huyu atapaswa kuwa ama kiongozi wa juu wa klabu ya ligi kuu au ligi daraja la kwanza au Mmoja wa wanahisa wa Klabu inayoshiriki ligi kuu au ligi daraja la Kwanza.
TFF itakuwa na hisa kwenye kampuni ya TPL na itakuwa na mwakilishi atakayepiga kuea lakini hataruhusiwa kugombea nafasi yoyote ya uongozi na wala hatakuwemo kwenye kamati tendaji za TPL
TPL itapaswa kuwa mwanachama wa TFF kama ilivyo kwa TAFCA, FRAT nk
Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF ni mjumbe wa kamati ya ufundi na maendeleo ya TPL
Kamati ya watu watatu ya waamuzi itakuwa na mjumbe mmoja atakayeteuliwa na TFF
TPL itatambua na kuheshimu maamuzi ya kamati ya nidhamu na rufaa ya TFF endapo suala lililoshindwa kupatiwa ufumbuzi na kamati ya rufaa na nidhamu ya TPL litapelekwa huko.
TPL itapaswa kutoa asilimia ya hisa za TFF toka kwenye pato lake kwa TFF na vilabu vitapaswa kutoa asilimia tano (5%) pato la milangoni viwanjani.
Kamati ya ushirikiano kati ya TFF na TPL itaundwa wajumbe kumi (10) watano watakaoteuliwa na TFF na watano watakaoteuliwa na Bodi ya wakurugenzi ya TPL.

Kamati za TPL



Mkutano mkuu wa TPL unahusisha wenyeviti na makatibu wakuu wa vilabu vyote vya ligi kuu, Makamu wa Rais TFF anayewakilisha vilabu, Mjumbe moja toka Chama cha Wachezaji wa kulipwa, TAFCA na FRAT
Kamati tendaji ya TPL itaundwa na makatibu wakuu/ECO wa vilabu vyote vinavyoshiliki ligi kuu na TAFCA, FRAT na Chama cha wachezaji wa kulipwa
Kamati ya Fedha na Miradi itaundwa na wajumbe watatu toka vilabu vya TPL
Kamati ya Ufundi na maendeleo itaundwa na wajumbe watatu, mmoja toka TAFCA, Mkurugenzi wa ufundi TFF makocha au mameneja watatu watakaoteuliwa na TPL
Kamati ya Nidhamu na haki za wachezaji itaundwa na wajumbe watano ambao watateuliwa na Bodi ya wakurugenzi wa TPL

Secretariet



CEO – Aajiliwe toka nje ya Nchi, atakuwa mtendaji mkuu wa TPL
Bwana Fedha – awe qualified accountant
Meneja masoko – Aajiliwe toka nje ya nchi, afanye kazi kwa kushirikiana na makampuni ya masoko ambayo yatalipwa kamisheni ya biashara watakayoingiza
Mhariri mkuu na meneja mawasiliano TPL - atafanya kazi kama afisa habari na meneja mawasiliano wa TPL, pia atatunza rekodi na taarifa zote zitakazohitajika kwa wana habari. Ataendesha tovuti ya TPL kwa kushirikiana na kampuni itakayoteuliwa kuendesha tovuti ya TPL. Atasimamia uandaaji wa vipindi vya TV vya TPL kwa kushirikiana na kituo cha televisheni kitakachokuwa na haki za matangazo ya TV



Chief Operations, Logistics & League liaison Officer, - 
   
atafanya kazi chini ya mratibu wa mashindano. Atashughulika na vilabu kuhakikisha viwanja vina viwango, mechi zinaanza kwa wakati, taratibu zote kabla ya kuanza kwa mechi zinafuatwa na haki za wadhamini wa ligi kuu zinalindwa.
Mkuu wa kitengo cha ufundi, ulinzi na usalama. Atafanya kazi chini ya Mratibu wa mashindano. Atahakikisha mambo yote ya kiufundi yanazingatiwa na wachezaji, makocha na waandishi wa habari wanapata ulinzi wa kutosha wakati wa mchezo wa ligi



Mratibu wa mashindano –
 
Atoke nje ya nchi. Atashughulika na mambo yote ya kiufundi kuanzia Usajili, Upangaji wa ratiba, utengenezaji wa kanuni za ligi, mafunzo kwa makocha, waamuzi, mameneja nk, na atawasimamia wahusika wa kipengele cha 5 na 6.

Udhamini



Ligi kuu itakuwa ni Brand name ya ligi itakayoendeshwa na TPL na kampuni ya TPL ingependa ligi hiyo iitwe Ligi Kuu isipokuwa tuu endapo atajitokeza mdhamini atakayenunua jina hilo kwa kipindi flani. Mdhamini atakayenunua jina la Ligi Kuu na kuweka la kwake ikiwemo kubadili logo ya ligi atalazimika kutumia logo ya Ligi Kuu kama frame ya logo yake mpya na atalazimika kuruhusu angalau kwa asilimia chache jina la ligi kuu kuendelea kutumika kwenye ligi.
Kampuni ya TPL itaruhusu ligi kudhaminiwa na wadhamini zaidi ya mmoja ambao wanafanya biashara zisizoshindana sokoni
Mdhamini yoyote wa ligi kuu atazuiwa kuweka logo ya kampuni yake kifuani lakini endapo mdhamini wa ligi kuu atatoa pesa kubwa ambayo bodi ya wakurugenzi wa TPL wataridhika kuvaa nembo yake, basi nembo hiyo itawekwa begani na siyo kifuani
Kutakuwa na wadhamini wadogo wadogo ambao watauziwa haki ya kutumia logo ya Ligi Kuu kwenye promosheni zao.
Kampuni ya TPL itawajibika kusaka mdau wa matangazo ya televisheni ili kuweza kupata pesa ya udhamini lakini nia kuboresha mazingira ya udhamini wa ligi kuu na udhamini wa vilabu.
Kwa kushilikiana na viongozi wa vilabu, meneja masoko wa TPL atakuwa na wajibu wa kuvsaidia vilabu kupata udhamini.
Kampuni ya ligi kuu TPL itashirikiana na makampuni ya masoko kusaka wadhamini

Mtaji wa kuanzisha Kampuni

Vilabu vitajitolea kucheza mechi za kuchangisha pesa kwa ajili ya kuanzisha kampuni. Muda muafaka kwa ajili ya Mashindano haya maalum yatakayoendeshwa na TPL uwe disemba 15 hadi 30 2011.

Mashindano haya yatatumika kama changamoto kwa kampuni kujifunza na kujiandaa kuendesha ligi kuu. Baada ya mashindano haya kampuni ya ligi kuu inaweza kuandaa mashindano mengine yatakayoenda sambamba na ligi kuu raundi ya pili ambayo yataitwa TPL Top 8 Knockout Tournament ambayo yatakuwa ni ya mtoano. Mashindano haya pia yatatoa changamoto kwa TPL kujifunza namna ya kuendesha ligi. Baada ya mashindano haya mawili ni imani yetu kuwa TPL itakuwa imeiva na tayari kuendesha Ligi Kuu

Katika mazingira kama haya ni lazima kampuni iwe imeshasajiliwa hadi kufikia muda huo na angalau CEO wa muda, bwana fedha na Mratibu wa mashindano wawe wameshaajiliwa (ajira ya uangalizi ya miezi mitatu)

Mashindano haya yatafanyika Dar es salaam, vilavu toka mikoani ambavyo havitakuwa na uwezo wa kushiriki mashindano haya kutokana na gharama havitadaiwa mtaji wa uanzishwaji wa kampuni.

Vilabu vyote vinavyocheza ligi kuu vitakuwa na hisa sawa kwenye kampuni. Hisa hizi hazitapatikana kutokana na klabu kununua hisa kwa pesa taslimu bali kutokana na kuwa mwanachama wa ligi kuu na pindi klabu inaposhuka daraja, hisa zake zitahamia kwa klabu iliyopanda daraja.

chanzo na Ligi Kuu Tanzania na  patrick Kahemele (PK)

Ndolanga afunguka soka ya vijana

 



Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Simba, Miraji Athumani (kushoto),akiwania mpira na beki wa JKT Oljoro kwenye mechi ya robo fainali ya Michuano ya Vijana ya U-20 inayoendelea kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Simba ilishinda mabao 6-2. Picha na Michael Matemanga.
Mwandishi Wetu


MWENYEKITI wa zamani wa Chama cha Soka Tanzania, FAT, (sasa Shirikisho la Soka Tanzania-TFF), Muhidin Hamad Ndolanga amesema hajaona uwapo wa nia ya dhati ya shirikisho hilo kuwekeza na kuendeleza soka ya vijana ikilinganisha kipindi chake.

Akizungumza katika mahojiano maalum jana Makao Makuu ya TFF, Ndolanga alisema: "Nilipokuwa naondoka FAT, niliacha misingi ya soka ya vijana, lakini kwa sasa sioni kama kuna seriousness (umakini zaidi) katika kuendeleza soka ya vijana.

Ndolanga, alisema kwa sasa kuna mashindano mbalimbali ya vijana yanaendeshwa lakini baada ya hapo yanaishia njia na hivyo kutokuwa na faida kwa vijana."Nadhani cha kufanya hapa, inatakiwa kuanza kutengeneza watoto tangu wakiwa darasa la nne na hadi kumaliza kidato cha sita, watapatikana timu za miaka mbalimbali.

"Wakiwa kidato cha nne, watakuwa wana sifa za kucheza U-17 kwa kuwa watakuwa na miaka 17 na akiwa kidato cha sita watakuwa na miaka 19 hivyo wanaweza kucheza U-20, utaratibu huu unawezekana.

"Hivi sasa kuna wadhamini wengi, wanaweza kuwaanzishia mashindano kila umri, angalia hapa, kuna mashindano ya vijana ya U-20 yanayodhaminiwa na Uhai, sasa kuna watu wana hela zao, ni mipango tu na taratibu zikiwekwa.
Ndolanga aliyeshindwa na Tenga kwenye uchaguzi wa kwanza wa TFF, 2004 alisema kuwa TFF ikiwekeza katika madarasa hayo, kwanza itakuwa na timu nyingi kwa umri mbalimbali na pia vijana ni rahisi kuwajenga kitabia kuliko waliokomaa.

Ndolanga ambaye wakati wa uongozi wake FAT, wadau walishuhudia mizozo ya uongozi ya mara kwa mara na aliyekuwa katibu mkuu wake, Michael Wambura alisema ili nchi ifikie mafanikio katika soka, uwekezaji katika eneo hilo ni jambo lisilokwepeka.

"Mtoto anajengeka kitabia, unamfundisha anaelewa nini maana ya soka na nini haramu ya soka, lakini si wazee (wachezaji wakongwe)," alisema Ndolanga.

Alisema kuwa TFF isiogope gharama kutengeneza wachezaji kwani kama itawekeza na wakapatikana wachezaji wazuri, inaweza kufanya utaratibu wakauzwa nje na yenyewe kupata fedha."Wenzetu wanafanya hivyo, wanatumia pesa nyingi kuwekeza kwenye soka la vijana na baadaye wanavuna faida kubwa."

"Watafutwe wadhamini kwa ajili ya kuendeleza vijana, na waendelezwe pindi wanapopatikana na si kuwaacha wanapotea hewani," alisema Ndolanga aliyesisitiza kuwa kuna wadhamini wengi wanaopenda kudhamini soka mradi kuwepo na utaratibu kwa udhamini.
 chanzo na mwanannchi

MAN U NA MADRID VITANI LEO KESHO NI VITA KATI YA FC BACERONA NA MILAN

 MECHI ZA CLUB BINGWA ULAYA LEO NA KESHO NI KAMA IFUATAVYO
                   
                 
                       









    leo              Oţelul Galaţi     11 : 45      Basel
         
            Manchester United     11 : 45      Benfica


                       Real Madrid     11 : 45      Dinamo Zagreb  
     
   
 
kesho  .   .   .         Zenit        09 : 00             APOEL  
                             
                                BATE     10 : 00           Viktoria Plzeň  
           
        Olympique Marseille   11 : 45          Olympiakos Piraeus 
                           
                            Arsenal       11 : 45           Borussia Dortmund
                           
                           Valencia       11 : 45            Genk
                                
                                Milan      11 : 45            Barcelona    
               
           Bayer Leverkusen       11 : 45          Chelsea

Nov 21, 2011

Yanga inatia raha


                                           kikosi cha yanga                                                                                                      
                                                                                                              
                                                                                                  MICHAEL MOMBUR


KAMA wewe ni shabiki wa Yanga, shusha pumzi kwanza. Ukisikia maneno wanayozungumza matajiri wanaofanya usajili unaweza kuchanganyikiwa kwa furaha. 

Viongozi hao wamepania kufanya usajili wa bandika bandua na tayari wameanza kumnyemelea beki matata wa kati kutoka Zanzibar ambaye akitua tu Jangwani, shughuli imekwisha.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Seif Ahmed Seif Magari, aliiambia Mwanaspoti jana Ijumaa kwamba mambo yanakwenda kisayansi na timu itakuwa imara mno katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kiongozi huyo alisema kwamba: Kuna beki wa kati mahiri sana kutoka Zanzibar, tunaendelea kumfuatilia na nadhani ndani ya wiki moja tutakuwa tumejua kama tutamsainisha au la, lakini rekodi zake zinaonyesha ni beki kiboko.

Kocha anaendelea kumfuatilia kwa karibu sana na hakuna chochote kilichofanyika rasmi mpaka sasa, ndiyo maana siwezi kutaja jina lake wala klabu anayotoka.

Aliongeza: Athuman Idd tumemrudisha na kocha amekubaliana naye na kwamba ataendelea kumwangalia kwa muda fulani, Salum Telela na Omega Seme waliokuwa Moro United kwa mkopo pia wamerudi kikosini.

Unaweza kuona kwamba Yanga katikati kuna mashine kali Haruna Niyonzima, Nurdin Bakari, Godfrey Bonny, Rashid Gumbo, Seif Juma �Kijiko, Omega na Chuji mwenyewe.

Ni wachezaji ambao wanaweza kufanya chochote muda wowote.
Bonny alikuwa hatumiki sana, lakini ni mzoefu, Gumbo ni kiungo, lakini anahamishiwa mara nyingi kwenye winga, angalia Nurdin anacheza popote beki, kiungo, mshambuliaji yaani anapachikwa tu kuendana na matakwa na malengo ya kocha.

Mwone Haruna, anaweza kucheza namba 10 pia, yaani Yanga hii tuliyosajili itakuwa inatumia viungo wengi sana kwa wakati mmoja kwa mujibu wa kocha, na siyo ajabu siku moja ukaona wakicheza hata watano kwa mpigo, tumejiwekea malengo ya mbali sana na tunataka kubadili kabisa staili ya mchezo.

Tunalenga mzunguko wa pili na mashindano ya kimataifa. Ubingwa tunautaka lakini akili nyingi tumeziweka kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani, tunataka kufanya kitu cha tofauti kabisa.
MWISHO. chanzo na mwanaspoti

Juma Kaseja ampoteza Fabregas


                                                                 




DORIS MALIYAGA 



KIPA namba moja wa Simba na Taifa Stars, Juma Kaseja, ndiye mkali wa mastaa wa Simba na Yanga, akimpiga bao hata kiungo hatari, Haruna Niyonzima �Fabregas� kwa kucheza mechi nyingi katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara 

Katika mzunguko huo, Kaseja, alicheza mechi zote 13 kwa dakika 90 ikimaanisha alikaa langoni kwa dakika 1170, hakuna mchezaji mwingine wa Simba na Yanga aliyefikia rekodi hiyo msimu huu hadi sasa.

Fabregas alicheza mechi 11. Mbili alizokosa, moja alikuwa akitumikia adhabu na nyingine alichelewa kurudi kutoka kwao Rwanda, alikokuwa na majukumu ya timu yake ya taifa.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kaseja ambaye ni nahodha wa Simba alisema: Siri ya mafanikio ya kucheza mechi zote ni kutokana na mazoezi na kufuata maelekezo ya kocha, lakini pia najitunza.

Siyo kwamba najua sana, ingawa nafahamu watu wataongea sana, lakini haya yote yanatokana na imani ya kocha kwangu.
Katika mechi hizo 13, Kaseja amefungwa mabao manane tu.
Beki wake wa kati, Juma Nyosso na kiungo Jerry Santo, wao walikosa mchezo mmoja. Nyosso alikosa mechi kutokana na kuonyeshwa kadi mbili za njano wakati Santo alishindwa kucheza kutokana na kuumia.

Kwa upande wa Azam FC ni Aggrey Morris na Ramadhani Chombo �Redondo� tu ndiyo waliocheza mechi zote, sawa na Ibrahim Mwaipopo na John Boko Adebayor, lakini wao hawakumaliza dakika 90 katika michezo miwili.

Kwa upande wa Mtibwa Sugar, beki wa kati Salvatory Ntebe na Juma Abdul ndiyo wamecheza mechi nyingi, walicheza mara 12.
MWISHO.  chanzo na http://www.mwanaspoti.co.tz

BONDE FC YA YATINGA NUSU FAINALI YA TEWA CUP

  picha juu ni Mamani (fundi) kiungo mchezeshaji na chini ni John Omary beki wa kutegemewa  ambae jana     alikuwa mwiba kwa Kimara fc
Hatimae timu ya bonde fc jana iliibuka na ushindi mnono wa goli  2-1 dhidi ya watoto wenzao wa Kimara fc katika mchezo huo uliokuwa wa kuvutia na wenye kila aina ya burudani na ulioshuhudiwa na mashabiki wengi sana ambao hawajawahi kutokea katika michuano hiyo ya TEWA CUP. 
 ilikuwa ni Kimara iliyokuwa ya kwanza kupata goli kupitia kwa mshambuliaji wao Omary Juma aliepiga shuti la mbali nje ya kumi na nane na kumshinda mlinda mlango wa Bonde fc Afidhi Juma na kuingia moja kwa moja  nao Bonde fc ilipata goli la kusawazisha kupitia kwa Hassani Rashid Banda alieingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Afidhi Salum baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Mamani (Fundi) ambae kwa mechi ya jana ndio aliibuka kuwa mchezaji bora alikuwa Hassani tena alieinua mashabi wa soka baada ya kupiga goli la ushindi dakika ya 90 na kuifanya timu ya Bonde fc kuibuka na ushindi wa goli 2-1 na kwa matokeo hayo timu ya Bonde fc inakuwa imejiakikishia kutinga moja kwa moja hatua ya nusu fainali katika michuano hiyo inayoshilikisha timu za vijana chini ya miaka 14 (under 14) kikubwa  kilichotokea jana ni jinsi vijana wa Bonde fc walivyokuwa wanasakata kabumbu safi hali iliyofanya mashabiki wote uwanjani kuweka ushabiki pembeni na kuanza kuwashabikia 

Nov 5, 2011

Asamoah kufanya kufuru

Kenneth Asamoah
DORIS MALIYAGA, aliyekuwa Dodoma
MSHAMBULIAJI hatari wa Yanga, Kenneth Asamoah, ameapa kutumia mapumziko ya Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa kwao huku akifanya mambo ambayo anasema akirejea, hakutakuwa na wa kumsogelea katika ufungaji, akiwamo mkali wa Simba, Felix Sunzu.

Mghana huyo mwenye mabao manane kwenye msimamo wa wafungaji akifungana na John Boko �Adebayor� wa Azam FC, alisema haoni wa kumtisha kwa vile anajua atakachokifanya kukoleza makali yake. Sunzu ana mabao matano.

�Najiamini naweza kuwa Mfungaji Bora, lakini kubwa Mungu anilinde na mambo mengine maana unaweza kupanga hili na yeye anapanga jingine,� Asamoah alisema.
�Ninaenda nyumbani kujifua zaidi ili nikija niwe na kasi mpya ni mabao kwenda mbele.�

Asamoah ametua Yanga msimu huu baada ya usajili wake kukwama msimu uliopita, alipokosa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC).

Akimzungumzia Boko alisema: �Hilo haliniumizi kichwa hata kidogo kwa sababu naamini ninachokifanya.

�Atakayenifananisha mimi na yeye anakosea, angalia mwenzangu amecheza mechi ngapi na kwa dakika ngapi, angalia na mimi muda niliocheza.

�Hatuko sawa na ndiyo maana nasema mzunguko wa pili nitamaliza kila kitu.�

Asamoah, ambaye ni kipenzi cha kocha wa sasa wa Yanga, Kostadin Papic, awali alikuwa akisumbuliwa na majeruhi akashindwa kuitumikia vizuri klabu hiyo.

Baada ya Boko na Asamoah wanaowafuata kwa ufungaji ni Gaudence Mwaikimba wa Moro United mwenye mabao saba.
Waliofunga mabao matano ni Emmanuel Okwi (Simba), Said Rashid (Mtibwa), Rajabu Chau (JKT Ruvu),
Mohamed Kijuso (Villa Squad), Said Dilunga (Kagera Sugar), Enyinna Darlington, Felix Sunzu na Patrick Mafisango (wote Simba).

Pia kuna Davies Mwape (Yanga), Juma Semsue (Polisi Tanzania) na Soud Mohamed (Toto African) ambao wamefunga mabao manne kila mmoja.

Naye Msaidizi wa Yanga, Fred Felix Minziro, amemsifu Asamoah na kusema maendeleo yake ni mazuri na kiwango chake kimekuwa kikibadilika siku hadi siku.chanzo na http://www.mwanaspoti.co.tz

Yanga yavunja rekodi

MASOUD MASASI, Dodoma
YANGA imeweka rekodi mpya ya mapato katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, baada ya kuingiza mapato ya Sh. 28.52 milioni kwenye mechi yake na Polisi Tanzania.
Katika mchezo huo uliofanyika Jumatano iliyopita, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Mapato hayo ni rekodi kwani tangu kujengwa uwanja huo mwaka 1977, haujawahi kuingiza fedha nyingi kiasi hicho.
Yanga pia imevunja yake rekodi yake yenyewe kwenye uwanja huo, kwani msimu uliopita ilipocheza na timu hiyo, mapato yalikuwa kiasi cha Sh. 20 milioni.

Watani wao wa jadi, Simba, msimu uliopita iliingiza Sh.19.3 milioni katika pambano lililochezwa katika uwanja huo. Simba ilishinda mabao 2-0.

Akizungumza na Mwanaspoti, Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dodoma (DOREFA), Abubakar Ibrahim, alisema katika mchezo huo kiingilio kilikuwa Sh. 5,000 kwa Jukwaa Kuu na mzunguko ilikuwa Sh. 3,000. Watazamaji 7,525 waliingia uwanjani.

Bao la Yanga katika mchezo huo lilipatikana dakika ya 44 kupitia kwa mshambuliaji wake Keneth Asamoah aliyemalizia pasi ya Hamisi Kiiza.chanzo na http://www.mwanaspoti.co.tz

Afrika Mashariki waipinga TFF


MICHAEL MOMBURI
WAANDISHI wa Habari mbalimbali wa Afrika Mashariki, wamesisitiza kwamba Ligi Kuu Tanzania Bara itapiga hatua kama itaendeshwa na kampuni kuliko kamati au Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Wakizungumza na Mwanaspoti kwa nyakati tofauti, waandishi hao mahiri kutoka Uganda, Kenya na Rwanda, wametoa maoni tofauti hasa wakitolea mfano ligi zinavyoendeshwa katika nchi zao na nyingine zenye mfumo huo wa kisasa.

James Waindi wa Standard la Kenya alisema: �Kampuni itakuwa makini zaidi na itaendesha mambo kitaaluma na kibiashara kuliko ilivyo sasa.

�Hata wadhamini wengi watajitokeza kwa vile siasa zitapungua na klabu zitapata nafasi ya kufanya mambo kwa uwazi zaidi.

�Shirikisho lilipokuwa linaendesha ligi hapa Kenya, ilikuwa ni matatizo. Timu zilikuwa haziwezi hata kulipa mishahara, lakini baada ya kuingia Kampuni (KPL), Supersport imeingia na kutoa fedha kwa klabu zote.

�Klabu sasa zinapata kama Sh 55 milioni za Kenya (Sh 982 milioni) kwa msimu, ambayo haikuwapo awali.
�Matangazo ya Supersport pamoja na promosheni inayofanywa na KPL imeongeza msisimko na kufanya mashabiki matajiri na makampuni kuingiza fedha kwenye timu.

�Hali hii haikuwapo kipindi cha KFF. Hivi sasa Gor Mahia, AFC Leopard zinaleta watu wengi sana uwanjani, hicho kitu kilishafutika enzi za KFF.

�Kampuni ikiingia Tanzania itafuta ukiritimba wa Simba na Yanga, hata Coastal Union au Villa Squad zitakuwa na fedha na nguvu ya kuzifunga Simba na Yanga na wachezaji watalipwa vizuri. TFF ina matakwa binafsi mara nyingine.�

Isaack Mukasa wa redio VOA FM ya Kampala, Uganda alisema: �Uganda Super League Ltd ndiyo inayoendesha Ligi Kuu hapa, kila klabu inapata Sh 78 milioni za Uganda (Sh 51.8 milioni) kutoka Kampuni ya Bia ya Uganda na Supersport.

�Fedha hizo hazikuwepo wakati Fufa inaongoza ligi. Angalia ligi zote za Afrika zilizoendelea na hata Ulaya, kuna kampuni inaongoza.

�TFF iziache klabu ziunde kampuni yao ya kuongoza ligi, hapa Uganda siku hizi hakuna cha Villa wala URA zote zinapigwa na klabu ndogo kwa sababu ya fedha za udhamini ambazo zimeongeza morali kwa wachezaji.

�Kampuni nyingi zinapenda kufanya kazi na taasisi za biashara na si watu wa kuchaguliwa au vikundi vya watu fulani.

�Ikiingia kampuni kwa sehemu kama Tanzania ambako watu wanapenda soka, klabu zitanufaika sana na hata zawadi za ligi zitaongezwa.�

Bonnie Mugabe wa Newtimes la Kigali, Rwanda naye alisema: �Kampuni kuendesha ligi ni sahihi kabisa kwani shirikisho lina mambo mengi.

�Kampuni ikiruhusiwa, ligi itakuwa ya kulipwa na yenye maslahi zaidi kwa klabu zenyewe na wachezaji, ili mradi kampuni iwe na sera, malengo na misingi imara.

�Kampuni itaendesha ligi kisasa na kupata wadhamini wengi wakubwa, lakini hiyo kampuni lazima iwe sehemu ya shirikisho, isimiliki ligi kwa asilimia 100. Shirikisho libaki na sehemu yake.�

Bonnie ni Mhariri wa gazeti la hilo la michezo la kila siku.
Lakini mtangazaji wa Contact FM ya Kigali, Rwanda, Kazungu Clev, alitofautiana na wenzake akisema: �Ligi ya Tanzania bado iko juu kwenye ukanda huu na sidhani kama kampuni inaweza kuongeza chochote hapo.

�TFF iendelee kuongoza ligi, lakini Kamati ya Masoko ifanye kazi yake kuongeza wadhamini. Mkiruhusu kampuni, Simba na Yanga zitazidi kutawala zitaminya klabu ndogo na mianya ya rushwa itaongezeka.

�Bora sasa kwani klabu zinadhibitiwa kirahisi na TFF. Kinachotakiwa ni mpira uwepo na fedha ziwepo.�chanzo  na http://www.mwanaspoti.co.tz

Waghana wafunga virago Azam

DORIS MALIAYAGA
WAGHANA wanaochezea Azam FC, Nafiu Awudu na Wahab Yahaya, wamenyoosha mikono na kufungasha virago na kurejea kwao.

Nafiu anayecheza nafasi ya beki na Wahab, ambaye ni mshambuliaji, waliondoka Jumatano iliyopita.

Akizungumza na Mwanaspoti, Nafiu alisema ameamua kuondoka kwani soka la Tanzania limenishinda.

�Mambo ni mengi, unacheza bila kujielewa, kuna mambo mengi yametokea, ambayo siwezi kueleza,� alisema Nafiu, ambaye anaelezewa kuwa mcha Mungu.

Alisema uwanjani ligi ya Tanzania si ngumu, ila amechoshwa na mambo yanayoendelea katika timu.

Aliongeza: �Nimeshamalizana na Azam na sina ninachodai, narudi nyumbani kufanya mipango mingine.

�Nategemea kwenda Afrika Kusini au Croatia kwani kabla ya kuja Azam kuna timu zilikuwa zikinitaka. Sasa nakwenda kufanya mipango mengine.�

Wahab naye kwa upande wake, alisema anayo mipango mingine. �Mambo ndiyo kama hivyo, mtanisikia kwenye vyombo vya habari nikiweka mambo yangu sawa.�

Kuondoka kwa Waghana hao, kunaifanya Azam kubakiwa na wachezaji watatu wa kigeni. Hao ni Obren Cirkovic wa Serbia, Kipre Tchetche wa Ivory Coast na Ibrahim Shikanda wa Kenya.

Pia kuondoka kwa Waghana hao, kunafungua njia ya beki wa zamani wa Simba, Joseph Owino kutua katika timu hiyo.

Owino aliachwa na Simba kutokana na kukabiliwa na maumivu ya goti yaliyomweka nje msimu mzima.
Lakini kuna habari Azam inajipanga kumsajili katika kipindi hiki cha dirisha dogo.chanzo na http://www.mwanaspoti.co.tz 

TFF, Mrwanda wachenjiana

MWANDISHI WETU
MSHAMBULIAJI, Danny Mrwanda, amesema amejitoa katika kikosi cha Taifa Stars kitakachochuana na Chad, lakini Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limedai mchezaji huyo hajatoa, ila ameondolewa.

Stars inawania kutinga hatua ya makundi ya kugombea tiketi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2014 .

Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, aliiambia Mwanaspoti jana Ijumaa kwamba Mrwanda hajaomba kujitoa, bali alikuwa hapatikani kwa mawasiliano yoyote yale, hivy kocha akaamuru aondolewe kwenye timu.

�Kocha alituambia tumwondoe na tumuite Boko kwa kuwa Mrwanda alikuwa hapatikani, kocha alituagiza hivyo na kama angekuwa amezungumza naye angetuarifu,� Osiah alisema.
�Kocha anasisitiza kwamba mchezaji yeyote ni lazima awe na mwamko na timu yake ya Taifa.

�Kila mara anatakiwa kufuatilia mambo yanavyoendelea. Sasa kwa Mrwanda haiko hivyo, hata kwenye simu hatumpati.�

Mrwanda aliiambia Mwanaspoti jana Ijumaa kupitia barua pepe kuwa amemwambia Poulsen kwamba hawezi kujiunga na Stars.

�Kwa sasa nasaka timu mpya kabla ya dirisha la usajili halifungwa, ndiyo sababu kubwa ya mimi kushindwa kutokea huko,� alisisitiza Mrwanda katika barua pepe hiyo.

Kuhusu kauli ya TFF kuwa hapatikani kwa mawasiliano yoyote, Mrwanda alisema: �Mbona wanawasiliana na Babi kupitia barua pepe yangu na kumtumia tiketi, inakuwaje hawanipati mimi?�

Mchezaji huyo aliyemaliza mkataba na DT Long ya Vietnam, aliwahi kuandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa mawasiliano wa Facebook kwamba anafikiria kujiondoa katika kikosi cha Taifa Stars ingawa hakuwahi kutekeleza azma yake.

Stars itakuwa ugenini dhidi ya Chad Novemba 11, kabla ya kurudiana siku tano baadaye jijini Dar es Salaam.
Endapo itaitoa Chad, itaingia Kundi C lenye timu za Gambia, Morocco na Ivory Coast ili kuwania kufuzu fainali hizo zitakazofanyika Brazil  chanzo na http://www.mwanaspoti.co.tz

Yondani ruksa Jangwani,Simba yanasa bonge la beki



MICHAEL MOMBURI
SIMBA iko tayari kufanya mazungumzo na Yanga ili iwauzie, Kelvin Yondani, muda wowote huku beki wa shughuli, Derrick Walulya, wa Uganda akiwa na nafasi kubwa ya kurejea Msimbazi, uongozi umethibitisha.

Wekundu wa Msimbazi hao pia wamemwachia kwa shingo upande kiungo Mkenya, Jerry Santo, anayekwenda Vietnam. Santo amekataa ofa ya kubaki Simba kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Santo aliyekuwa akivaa jezi namba 13 amekuwa tegemeo kwenye kikosi cha kwanza cha Simba kwa misimu miwili mfululizo.

Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange �Kaburu� aliiambia Mwanaspoti jana Ijumaa kuwa Santo hataichezea Simba mzunguko wa pili lakini Walulya, ambaye aliicheza timu hiyo kwenye Kombe la Kagame ana nafasi kubwa ya kurejea Msimbazi.

�Santo amemaliza mkataba na Simba na ametuaga kwamba anaondoka hawezi kurudi, tumembembeleza lakini amekataa ofa yetu mpya,� Kaburu alisema.

�Alisema anakwenda Vietnam tumemtakia kila la kheri, lakini tumemwambia kwamba mambo yakibadilika arudi muda wowote tutampokea.

�Ni mchezaji mahiri, tulipenda kuendelea naye lakini inaonekana akili yake ameigeuzia kwenye soka la nje zaidi.�
Kuhusu Yondani, ambaye amekuwa akihusishwa na Yanga, Kaburu alisema: �Yondani bado ni mchezaji wa Simba na tuna mkataba naye kisheria mpaka mwakani.

�Hatujapata ofa yoyote kwa klabu inayomhitaji, lakini timu yoyote hata kama ni Yanga ikija kwetu wakitupa ofa nzuri tutamwachia kama mchezaji mwingine yoyote yule, ili mradi tuelewane na dau lifikiwe.�

Lakini viongozi wazito kwenye Kamati ya Usajili ya Yanga, jana Ijumaa walisema kuwa hawako tayari kumnunua Yondani kwa dau kubwa labda kama atakubaliana na Simba wavunje mkataba kwa masharti mepesi.

Yondani amegoma kuchezea Simba katika siku za karibuni ikidaiwa kuchukizwa na kutopangwa katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.chanzo na http://www.mwanaspoti.co.tz

Michezo na Burudani

Michezo na Burudani

Nov 1, 2011

Tanzania na matatizo katika soka

Kila ukifungu kurasa za wahariri wa habari za michezo utakutana na kichwa cha habari kinachosema tuwekeze katika soka la vijana ili kujikomboa katika soka.

Mara nyingi kauri kama hizi huja pale timu zetu zinapofanya vibaya ila zinapobahatisha kushinda timu hizo hizo husifiwa na suala la kuanzisha timu za vijana wadogo hufa vichwani mwa wahariri na wanaharakati wa soka.

Hata ukitembelea vyama vya soka vya wilaya na mikoa ukiwauliza viongozi wake wanafanya nini ili kuinua viwango vya soka katika eneo lao wao hapo akuna jibu la moja kwa moja utakalopata dhidi ya kujigonga gonga tu .

Mfano leo hii kamuulize katibu wa chama cha soka wilaya yeyote ile nchini je katika wilaya yako kuna timu ngapi zilizosajiliwa na ziko hai hawajui ila mara nyingi huwa wanazilipia timu hada kipindi cha kampeni ili zipate nafasi ya kushiriki katika uchaguzi na kuwachagua wao .

Hebu jiulize kama vyama vyote vya soka kuanzia wilaya na mikoa vingekua makini unadhani tungekupo hapa tulipo sasa katika maendeleo ya soka .

Leo hii hakuna hata chama kimoja cha soka ambacho kimeanzisha japo michuano kwa ajiri ya watoto wadogo under 14  au under 17 lakini cha kushangaza tuna timu ya taifa ya under 17 tff wao wanaitoa wapi hiyo timu kama hiyo timu sio azam fc wanaibadilisha jina tu na hii ndio maana timu zetu za taifa zinakosa uzalendo kutokana na timu moja kujaza wachezaji kisha unaiita taifa staz

 Leo kuna chama kinajiita chama cha kuendeleza soka la vijana kinondoni (KIDIYOSA) lakini nacho hiki kinamapungufu makubwa kila michuano inayoandaliwa na viongozi wa chama hiki sehemu kubwa ya timu zinazoshiliki zinatoka katika kata ya Makumbusho sasa je makumbusho imekuwa wilaya na michuano yenyewe inakosa hata motisha kwa wachezaji wenyewe vijana wanajituma hadi kufika fainali matokeo yake wanapewa kikombe kitupu tena hakina hadhi ya michuano yenyewe nali timu zimetumia gharama kubwa sana katika kushiliki michuano hiyo pia timu ndio huamuliwa kuwalipa waamuzi na wafunga nyavu hivi kuna humuhimu wa kuwa na vyama kama hivi hapa nchini .

Sisi Bonde fc tunapenda kushauli kwa viongozi wa soka na waandishi wa habari wapende kushirikiana na sisi tunaomiliki timu za watoto wadogo kuanzia miaka 7 hadi 21 kwani kuna hadi timu zinashiliki ligi kuu hazina timu za vijana wadogo.

Ukitazama kwa haraka katika wilaya ya kinondoni timu zenye watoto wa kuanzia miaka 8 hadi 21 ni chache sana na zina hali ngumu zimekuwa zikitegemea kuombaomba tu ilizishiliki katika michuano mbalimbali inayozikabili timu hizo ni Bonde Fc, Makumbusho Talent, Shein Rangers, Lion Magomeni, Kimara hizi ndio timu zenye mipango ya muda mrefu basi tunawaomba wadau wa soka kujitokeza kwa kuzisaidia timu hizi na kuacha tabia ya kusubili mchezaji hujui katokea wapi wewe unamsajili matokeo yake timu zinakosa wachezaji wenye nidhamu na wengine kujiona wao ni bora zaidi na hii inatokana na kukosa misingi imara  

Katika kudhibitisha hili tunawakalibisha wadau wotewa soka kuwa wawe wanafika siku za jumapili maeneo ya magomeni barafu kuja kuona timu za under 14 zinavyo oneshana kabumbumbu safi

BONDE FOOTBALL CLUB: Simba wasaka faraja, Yanga vitani

BONDE FOOTBALL CLUB: Simba wasaka faraja, Yanga vitani

Simba wasaka faraja, Yanga vitani

OLIVER ALBERT
BAADA kulizwa na watani wao, Simba watasaka faraja kutoka kwa Moro United wakati Yanga itakuwa katika vita dhidi ya Polisi wakati timu hizo zitakapokabiliana kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma wakati wa mechi za kufunga mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara zitakazochezwa kesho Jumatano.

Simba inayoongoza Ligi Kuu ikiwa na pointi 24 baada ya kufungwa na wapinzani wao wa jadi, Yanga 1-0 itapenda kutuliza mzuka wa mashabiki wake kwa kuifunga Moro United kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ili kuhakikisha inabaki kwenye usukani wa Ligi Kuu.

Yanga kwa upande wake, itakuwa inaiombea mabaya Simba wakati huo ikipigana kuifunga Polisi ili kuwakamata wapinzani wao wa jadi. Yanga ipo pointi tatu nyuma ya Simba.
Sala za Yanga zinaweza kufanikiwa ikiwa Simba wataendeleza harakati za kumsaka mchawi baada ya kufungwa na watani zao. Ni kawaida kwa klabu hizi kubwa mbili kuingia katika migogoro pale zinapofungwa na mtani wake.
Sasa kuna maneno tayari kuwa ajira ya kocha wa Simba, Moses Basena ipo hatarini baada ya kufungwa na Yanga.

Simba wameshasahau kuwa Mganda huyo amesaidia timu hiyo kuongoza ligi na kabla ya kukabiliana na Yanga, ilikuwa haijapoteza mechi.

"Tusahau kipigo cha Yanga tuangalie mechi nyingine. Ule ni mchezo kama michezo mingine yoyote hivyo watu wasitishike kwa kupoteza, tunahitaji kushinda mchezo ujao dhidi ya Moro United ili tuweze kumaliza mzunguko wa kwanza tukiwa tunaongoza ligi.

"Ninachowaomba wachezaji wangu hasa washambuliaji kuwa makini, kwani tunaongoza kwa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga kwenye ligi lakini hatuzitumii kutokana na papara ya washambuliaji wangu. Wanatakiwa kutulia ili timu iweze kupta mabao," alisema Basena, raia wa Uganda wakati alipozungumza na Mwanaspoti.

Naye kocha wa Moro United, Hassan Banyai alisema watahakikisha wanashinda mchezo huo na kuisimamisha Simba.

Kwa upande wao, Yanga wana nafasi kubwa ya kuvuna pointi tatu dhidi ya Polisi, ambayo inasuasua kwenye ligi hiyo. Polisi inashika nafasi ya pili kutoka mkiani ikiwa na pointi tisa.

Hata hivyo, wanapaswa kuchukua tahadhari ya uwanja wa Jamhuri, ambao unashutumiwa kuwa kati ya viwanja vibovu vya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kocha wa Yanga, Kostadian Papic, hata hivyo, amepania kuendeleza ubabe kwa kutamba kumnyoa kila ajaye mbele yake hadi wahakikishe wanaikamata Simba na kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara.

Mechi nyingine zitakaochezwa kesho Jumatano zitakuwa kati ya JKT Oljoro itakaowakaribisha Villa Squad kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Toto African watakuwa wenyeji wa Azam kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, JKT Ruvu watakuwa wageni wa ndugu zao Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mlandizi mkoani Pwani na Mtibwa itaikaribisha African Lyon kwenye Uwanja wa Manungu. Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Coastal Union keshokutwa Alhamisi kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. CHANZO NA http://www.mwanaspoti.co.tz

Papic asajili silaha tatu mpya yanga

MWANDISHI WETU
YANGA itaongeza wachezaji watatu katika dirisha dogo la usajili ambalo linaanza leo Jumanne ili kuongeza nguvu katika kikosi chake.

Akizungumza na Mwanaspoti jana Jumatatu, Kocha wa Yanga, Kosta Papic alisema wachezaji wote wa kigeni waliopo katika timu hiyo wapo salama, lakini atapunguza wachezaji watatu wa Tanzania na kuleta wengine watatu kutoka nchini.

"Hakuna ubishi tutasajili wachezaji watatu, na kuwaondoa watatu. Wachezaji wote wa kigeni tutaendelea kuwa nao kwa sababu wana umuhimu mkubwa katika kikosi chetu," alisema Papic ambaye timu yake itacheza na Polisi mjini Dodoma kesho Jumatano.

Kocha huyo wa Serbia alifafanua kuwa baada ya mchezo wao na Polisi, watakuwa katika mazingira mazuri ya kujua wachezaji wanaowaacha na wanaowasajili.
"Kuna nafasi zina upungufu, hatuna budi kuongeza nguvu, tutahakikisha tunazitumia siku 30 hizi za usajili kuimarisha kikosi chetu," alisema.

Mwanaspoti linajua kuwa Godfrey Bonny, Fred Mbuna, Zubery Ubwa na Abuu Ubwa wapo katika hatari kubwa ya kupigwa mstari mwekundu.

Wachezaji wa kigeni ambao Papic amewahakikisha usalama ni Yaw Berko (Ghana), Davies Mwape (Zambia), Kenneth Asamoah (Ghana), Haruna Niyonzima (Rwanda) na Hamisi Kiiza (Uganda).

Akiizungumzia mechi dhidi ya watani wao Simba waliyoshinda bao 1-0 mwishoni mwa wiki, Papic alisema ilikuwa mechi nzuri kwa pande zote mbili.

"Katika Afrika ile inaweza kuwa miongoni mwa mechi nzuri kabisa za watani, mara nyingi mechi za watani huwa zinakuwa na presha kubwa, lakini ile ilikuwa mechi nzuri kwa pande zote," alisema Papic, mwenye uzoefu wa bara la Afrika kwa miaka 15.

Alisema alimpanga Mwape ambaye kwa muda mrefu alikuwa majeruhi baada ya kuzungumza naye na kukubali kucheza.

"Sikumlazimisha kucheza, nilimuuliza kama yupo tayari, akanihakikisha kuwa yupo tayari kwa mchezo, nikampanga na akaleta ushindi," alisema Papic.

Papic ni mzoefu wa mechi za watani kwani amefundisha soka katika nchi mbalimbali Afrika ambako kuna mechi ngumu za watani.

Alifundisha Lobi Stars, Enugu Rangers na Enyimba za Nigeria, Kaizer Chiefs, Orlando Pirates na Martizburg za Afrika Kusini, Hearts CHANZO NA http://www.mwanaspoti.co.tz
  

BONDE FOOTBALL CLUB: Boban azua patashika jingine

BONDE FOOTBALL CLUB: Boban azua patashika jingine