Apr 23, 2012

DIWANI AJITOSA KUSAIDIA UKARABATI UWANJA WA BONDE FC

Hatimae diwani wa Makumbusho mh Ally Haroub amejitosa katika kusaidia ukarabati wa uwanja wa Bonde Fc.diwani alifikia hatua hiyo baada ya kutembelea uwanja na kuona jinsi ulivyoharibika.

 Alipoalikwa katika kikao cha  wanakamati ya kukarabati uwanja alifika na ndipo alipowahaidi kuwa atashuhurukia uwanja kwani suala hilo lipo ndani ya uwezo wake na kwa kushirikiana na kamati ya uwanja anahuhakika wa kuifanya kazi hiyo bila tatizo.

 Pia katika kikao hicho kamati ndogo ya kusimamia ukarabati iliundwa na diwani akiwa mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo  akiwataja wajumbe wa katimati hiyo mratibu wa uwanja wa Bonde Fc ndugu  Rashid Maulid Banda alisema kamati inaundwa na watu watano  

Nae mwenyekiti wa kamati ya muda iliyoundwa ndugu Omary Maloki amehaidi atahakikisha kamati yake inafanya kila linalowezekana ili kufanikisha matengenezo ya uwanja kwa kuwatafuta wafadhili mbali mbali ili kufikia malego.
  1.    MWENYEKITI               OMARY     MALOKI
  2.    KATIBU                        RAMADHANI  FARAHANI
  3.    MJUMBE                       EMANUEL I ISHENGOMA 
  4.    NJUMBE                       MASOUD      HEMED
  5.    MJUMBE                       MH:  ALLY    HAROUB 
  6.    MJUMBE                       RASHIDI       BANDA   
 
Kutokana na hualibifu huo umesababisha timu kuwa na wakati mgumu kutokana wa kukosa uwanja wa kufanyia mazoezi hali iliyopelekea timu kuomba uwanja katika shule ya msingi Tuliani Magomeni jambo ambalo ni hatari kwa wachezaji wa under 14 kwani inawaladhimu kuvuka barabara.

Na hata eneo lenyewe linalotumika kwa mazoezi ni dogo hivyo kusababisha timu kukosa muda wa kucheza full game  kwani kila siku wanacheza open space hali ambayo imekuwa ikiwafanya vijana kupata sana tabu katika mechi kutokana na kuzoea kucheza katika stahili hii.

Pia hali hii imepelekea wachezaji wengi kukimbia na kwenda kufanya mazoezi katika viwanja vingine na wengine kufanya mazoezi siku mojamoja.




Apr 2, 2012

UONGOZI WA BONDE FC WAKUTANA MWANANYAMALA JANA JUMAPILI 1/04 2012

Hatimae uongozi wa timu ya Bonde Fc umekaa kikao  na kuamua kuhufanyia marekibisho uwanja wao wa Bonde . Ambao uliaribika vibaya kutokana na mafuriko yaliyotokea mwezi Januari ambayo yaliuwacha uwanja wa Bonde Fc ukiwa umehalibika vibaya. Hali ambayo ilisababisha timu kukosa uwanja wa kufanyia mazoezi na kuamua kuhamia katika uwanja wa shule ya msingi Tuliani iliyoko Magomeni 

Hali hii ilikuwa ni pigo kwa timu ya Bonde Fc akiongea na chumba cha habari cha timu hii kocha mkuu wa timu ndugu Issa Joseph  anasema hali hii ilikuwa inampa tabu kutokana na sehemu waliyopata kwa ajiri ya kufanyia mazoezi ilikuwa ni ndogo sana hivyo ilikuwa inasebabisha timu kukosa vitu vingi kama umoja,uelewano wa wachezaji wawapo uwanjani kutokana na kuzoea kucheza sana katika uwanja mdogo .

Pia hali hii ilisababisha timu ya under 21 kutokuwepo kabisa kwa muda kutokana na wachezaji wengi kwenda kufanya mazoezi katika viwanja vingine hali hii pia iliweza kusababisha kutoa wakati mgumu kwa kocha kupanga timu katika mechi mbalimbali kutokana na kila mchezaji kuja na aina ya uchezaji wake japo timu iliendelea kujikongoja hivyo hivyo 

Pia uongozi wa timu ya Bonde Fc unawaomba watu wote wenye nia ya kusaidia timu ya Bonde fc katika ujenzi wa uwanja kwa wale wenye nia ya kuchangia wanaweza fika moja kwa moja katika club yetu iliyoko Mwananyamala
maelezo zaidi unaweza piga namba zifuatazo 

Meneja wa timu ni   0712   877 557   
Kocha mkuu ni         0713   658  049
Kocha m/saidizi        0653   728  706
Katibu                       0714   333  316

Emil ni bondefc1@hotmail.com




Picha juu ni mahadhi ta vijana wadogo ambao timu ya Bonde Fc inawalea katika mzingira magumu kwa sasa kutokana na uwanja wao kuharibiwa vibaya na mvua hapa ni siku waliocheza katika uwanja wa Karume
 Hii ni timu ya under 21 hapa siku walipocheza fainali zidi ya African Peple katika michuano ya KIDIYOSA michuano inayoandaliwa na chama cha kukuza vijana Kinondoni
Meneja wa Bonde Fc ndugu Shakeel Shabani (kpl) akiwa ameshika moja ya makombe ambaya timu ya Bonde Fc imeyachukua hili ni kombe la (KIDIYOSA) under 21  2011/12
Wachezaji na mashabiki wa Bonde Fc wakiwa wanashangilia moja ya makombe ambayo wamechukua katika michuano ya 2011/12