Hatimae uongozi wa timu ya Bonde Fc umekaa kikao na kuamua kuhufanyia marekibisho uwanja wao wa Bonde . Ambao uliaribika vibaya kutokana na mafuriko yaliyotokea mwezi Januari ambayo yaliuwacha uwanja wa Bonde Fc ukiwa umehalibika vibaya. Hali ambayo ilisababisha timu kukosa uwanja wa kufanyia mazoezi na kuamua kuhamia katika uwanja wa shule ya msingi Tuliani iliyoko Magomeni
Hali hii ilikuwa ni pigo kwa timu ya Bonde Fc akiongea na chumba cha habari cha timu hii kocha mkuu wa timu ndugu Issa Joseph anasema hali hii ilikuwa inampa tabu kutokana na sehemu waliyopata kwa ajiri ya kufanyia mazoezi ilikuwa ni ndogo sana hivyo ilikuwa inasebabisha timu kukosa vitu vingi kama umoja,uelewano wa wachezaji wawapo uwanjani kutokana na kuzoea kucheza sana katika uwanja mdogo .
Pia hali hii ilisababisha timu ya under 21 kutokuwepo kabisa kwa muda kutokana na wachezaji wengi kwenda kufanya mazoezi katika viwanja vingine hali hii pia iliweza kusababisha kutoa wakati mgumu kwa kocha kupanga timu katika mechi mbalimbali kutokana na kila mchezaji kuja na aina ya uchezaji wake japo timu iliendelea kujikongoja hivyo hivyo
Pia uongozi wa timu ya Bonde Fc unawaomba watu wote wenye nia ya kusaidia timu ya Bonde fc katika ujenzi wa uwanja kwa wale wenye nia ya kuchangia wanaweza fika moja kwa moja katika club yetu iliyoko Mwananyamala
maelezo zaidi unaweza piga namba zifuatazo
Meneja wa timu ni 0712 877 557
Kocha mkuu ni 0713 658 049
Kocha m/saidizi 0653 728 706
Katibu 0714 333 316
Emil ni bondefc1@hotmail.com
Picha juu ni mahadhi ta vijana wadogo ambao timu ya Bonde Fc inawalea katika mzingira magumu kwa sasa kutokana na uwanja wao kuharibiwa vibaya na mvua hapa ni siku waliocheza katika uwanja wa Karume
Hii ni timu ya under 21 hapa siku walipocheza fainali zidi ya African Peple katika michuano ya KIDIYOSA michuano inayoandaliwa na chama cha kukuza vijana Kinondoni
Meneja wa Bonde Fc ndugu Shakeel Shabani (kpl) akiwa ameshika moja ya makombe ambaya timu ya Bonde Fc imeyachukua hili ni kombe la (KIDIYOSA) under 21 2011/12
Wachezaji na mashabiki wa Bonde Fc wakiwa wanashangilia moja ya makombe ambayo wamechukua katika michuano ya 2011/12
No comments:
Post a Comment