Baada
ya kikao cha karibia masaa 4 au zaidi viongozi wa vilabu 14
vinavyoshiriki ligi kuu ya Tanzania bara walifikia maamuzi ya kuanzishwa
kwa kampuni itayoendesha ligi kuanzia msimu ujao.
Kikao
hicho kilichofanyika katika hoteli ya JB Del-monte (zamani Paradise) @
Benjamin Mkapa Tower kilihudhuriwa na viongozi 13 kati ya 14 wa vilabu
vya ligi kuu isipokuwa Kagera Sugar waliotoa udhuru lakini wakisema
wataunga mkono maamuzi yatakayotolewa
Katika
kikao hicho maamuzi yaliyotolewa ni kwamba uanzishwe mchakato wa
kuwezesha usajili wa kampuni ambayo itaendesha ligi hiyo, huku Makamu
mwenyekiti wa Simba Godfrey Nyange Kaburu akiteuliwa kuwa mwenyekiti wa
kamati hiyo, Celestine Mwesiga katibu mkuu Yanga-Makamu mwenyekiti, Meja
Ruta wa Ruvu Shooting- akiteuliwa Katibu wa hiyo kamati, na Shani wa
Azam FC na Evadius Mtawala wa Simba wakiwa wajumbe, ambao wote kwa
pamoja watashugulikia mchakato wa kupatikana kwa usajili wa kampuni
hiyo.
“Dauda alialikwa na viongozi wa vilabu kutoa mawazo yangu juu mchakato mzima wa kuundwa kwa kampuni itayoendesha ligi kuu.”
Pia
viongozi hao wa vilabu 13 vya ligi kuu walitoa shukrani sana kwa vyombo
vya habari hususani kwa watangazaji wa vipindi vya Sports extra na
Sports Bar kutoka Clouds media group kwa kuwa watu wa kwanza kuanzisha
na kusimamia mjadala wa kuanzishwa kwa kampuni ya kuendesha ligi kuu
Tanzania bara.
chanzo na shaffih dauda wa
www.shaffihdauda.com
No comments:
Post a Comment