Oct 5, 2011

Timu ya Bonde fc inaendelea na mazoezi kwa ajiri ya mechi zake

 
Timu ya bonde fc ya mwananyamala inaendelea na mazoezi magumu ili kujiwinda na mechi zinazowakabiri akiongea na mwandishi wa habari hii kiungo mkabaji wa timu hiyo ya under 14 Hassani Rashid Banda alisema kuwa mazoezi wanayopewa na makocha wao ni magumu na ya kufa mtu . Ila amewatoa wasi wasi mashabiki wao kuwa yeye na wenzeke watandeleza mapambano mazito katika mechi ijayo ya jumamosi dhidi ya mikocheni kids itakayochezwa katika uwanja wa mikocheni shule ya msingi na pia aliwasihii mashabiki wa soka kokote pale jijini kujitokeza kwa wingi kuja kujionea vipaji vya kweli na pasi za kweli  na si butua butua kama baadhi ya timu za ligi kuu

No comments: