Nov 1, 2011

Boban azua patashika jingine





DORIS MALIYAGA
BAADA ya kuripotiwa kumpiga mchezaji mwenzake, Haruna Moshi `Boban' amehusishwa na tukio jingine la mechi ya Simba na Yanga iliyochezwa Jumamosi iliyopita jijini Dar es Salaam.

Mwanaspoti liliripoti Jumapili iliyopita kuwa Boban alimpiga kichwa mara nne mwenzake Emmanuel Okwi lakini kumbe kiungo huyo mchezeshaji hakuwemo katika kikosi cha timu hiyo kilichotakiwa kucheza siku hiyo, ambayo Simba ilifungwa 1-0.

Orodha ya majina ya wachezaji wa Simba na Yanga ilitolewa saa 9.45 alasiri na Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura kwa waandishi wa habari bila ya jina la Haruna Moshi �Boban�.

Wachezaji 18 wa Simba ndio walikuwa wameorodheshwa ingawa majina 16 yalikuwa yamechapishwa na mawili yaliongezwa kwa kalamu ya wino mweusi. Walioongezwa kwa wino walikuwa Uhuru Selemani na Salum Machaku.

Boban, ambaye alimpiga Okwi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya kukasirishwa na kufungwa na kumtuhumu mwenzake aliuza mechi, inadaiwa aligoma mapema kucheza mchezo huo hadi alipobembelezwa na viongozi.

Boban, ambaye aliingia dakika ya 56, kuchukua nafasi ya Amri Kiemba, inasemekana aliingizwa katika orodha wakati wa mapumziko baada ya mwamuzi kuombwa.  
Wambura alikiri kuwa nyota huyo anayesifika kwa kucheza mpira wa akili, jina lake, halikuwepo katika orodha ya majina ambayo ilitumwa kwa kamishina lakini akadokeza kuwa Simba walimwomba mwamuzi wabadilishe jina la mchezaji huyo.

Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange �Kaburu� alipinga vikali madai hayo na kudai: �Jina la Boban lilikuwepo katika orodha ya majina tuliyopeleka TFF na hatujui kilichotokea, tuligundua jina halipo tukiwa uwanjani, ndiyo likaongezwa.�
Kwa upande wa Yanga, jina la Abou Ubwa lilikuwa limechapishwa na mashine lakini lilikatwa kwa wino na kuwekwa jina la Ibrahim Job.
    chanzo na  http://www.mwanaspoti.co.tz

No comments: