Hatimae diwani wa Makumbusho mh Ally Haroub amejitosa katika kusaidia ukarabati wa uwanja wa Bonde Fc.diwani alifikia hatua hiyo baada ya kutembelea uwanja na kuona jinsi ulivyoharibika.
Alipoalikwa katika kikao cha wanakamati ya kukarabati uwanja alifika na ndipo alipowahaidi kuwa atashuhurukia uwanja kwani suala hilo lipo ndani ya uwezo wake na kwa kushirikiana na kamati ya uwanja anahuhakika wa kuifanya kazi hiyo bila tatizo.
Pia katika kikao hicho kamati ndogo ya kusimamia ukarabati iliundwa na diwani akiwa mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo akiwataja wajumbe wa katimati hiyo mratibu wa uwanja wa Bonde Fc ndugu Rashid Maulid Banda alisema kamati inaundwa na watu watano
Nae mwenyekiti wa kamati ya muda iliyoundwa ndugu Omary Maloki amehaidi atahakikisha kamati yake inafanya kila linalowezekana ili kufanikisha matengenezo ya uwanja kwa kuwatafuta wafadhili mbali mbali ili kufikia malego.
- MWENYEKITI OMARY MALOKI
- KATIBU RAMADHANI FARAHANI
- MJUMBE EMANUEL I ISHENGOMA
- NJUMBE MASOUD HEMED
- MJUMBE MH: ALLY HAROUB
- MJUMBE RASHIDI BANDA
Kutokana na hualibifu huo umesababisha timu kuwa na wakati mgumu kutokana wa kukosa uwanja wa kufanyia mazoezi hali iliyopelekea timu kuomba uwanja katika shule ya msingi Tuliani Magomeni jambo ambalo ni hatari kwa wachezaji wa under 14 kwani inawaladhimu kuvuka barabara.
Na hata eneo lenyewe linalotumika kwa mazoezi ni dogo hivyo kusababisha timu kukosa muda wa kucheza full game kwani kila siku wanacheza open space hali ambayo imekuwa ikiwafanya vijana kupata sana tabu katika mechi kutokana na kuzoea kucheza katika stahili hii.
Pia hali hii imepelekea wachezaji wengi kukimbia na kwenda kufanya mazoezi katika viwanja vingine na wengine kufanya mazoezi siku mojamoja.