Mar 7, 2012

Chuji: Nilifanya makusudi kumchapa kiatu



Beki wa sasa wa Yanga Athuman Idd Chuji akikabiliana na Musa Hassan Mgosi mwaka juzi
MICHAEL MOMBURI, CAIRO
KIUNGO wa Yanga, Athuman Idd 'chuji' amesema hakuwa na jinsi ya kufanya zaidi ya kumchapa kiatu straika wa Zamalek, Razak Omotoyossi na kuonyeshwa kadi nyekundu.

Chuji alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 63 baada ya kumkwatua Omotoyossi, kitendo ambacho Kocha Kosta Papic alikilalamikia baadaye kwa madai kuwa kiliharibu mfumo wake wa uchezaji.

"Hakukuwa na jinsi nyingine zaidi ya kufanya nilivyofanya, bora nilivyofanya kuliko ningeacha tukafungwa goli la pili, yule jamaa alikuwa anakwenda kufunga goli kabisa," alisema Chuji, ambaye alicheza katikati kwenye ulinzi na Nadir Haroub `Cannavaro'.

"Lakini ukiangalia aina ya mchezo, yaani hii mechi ya hapa Misri ilikuwa nyepesi kuliko ile ya Dar es Salaam, haikuwa bahati yetu tu," alisema mchezaji huyo wa zamani wa Polisi Dodoma na Simba.

Yanga ilitolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wikiendi iliyopita kwa jumla ya mabao 2-1 na Zamalek ya Cairo. Katika mchezo wa kwanza ilitoka sare ya bao 1-1 jijini Dar es Salaam kabla ya kufungwa bao 1-0 katika Uwanja wa Jeshi la Misri, Jumamosi iliyopita.

Viongozi wa Yanga wamekuwa wakilalamikia uchezeshaji mbovu, huku baadhi ya wachezaji wakisema mabadiliko ya kumtoa Jerry Tegete na kumuingia Chacha Marwa hayakuwa na manufaa.


No comments: