Sep 2, 2011

AFRICAN LYON WASHINDWA TAMBA MBELE YA COASTAL UNION

AFRICAN LYON WAPOTEA CHAMANZI

African lyon ya Mbagala wakiwa katika uwanja wa Azam uliopo Chamanzi jana walitoka mikono mitupu baada ya Coastal union kunyakuwa point zote 3 katika muendelezo wa Ligi kuu ya Vodacom.

African lyon wakiwa wenyeji wa Coastal union ya Tanga ja walishindwa kutamba na kuwaruhusu wagosi kuondoka na ushindi wa goli moja bila, goli likifungwa na Salum Azizi Gilla katika dakika ya 20 ya mchezo.

Kutokana na Ushindi huo Coastal union imevikisha point 4 na kupanda mpaka nafasi ya 5.


MSIMAMO WA VPL.
Kwenye Mabano Idadi ya Mechi Zilizochezwa.
1. Toto Africa (4) 7
2. Simba SC (2) 6
3. JKT Ruvu (3) 5
4. Africa lyon (4) 5
5. Coastal Union (3) 4
6. Moro United (3) 4
7. MtibwaSugar (3) 4
8. Villa Squad (3) 4
9. Azam FC (2) 3
10. JKT Oljoro (2) 3
11. KageraSugar (4) 3
12. PolisiDodoma (3) 2
13. RuvuShooting (2) 1
14. Yanga SC (2) 1

No comments: