Oct 24, 2011

Kiiza aipasha Yanga



Winga wa Yanga, Rashid Gumbo akiruka juu kuwania mpira sambamba na beki wa JKT Oljolo, Rashid Roshwa wakati wa mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Azam Chamazi jijini Dar es Salaam. Yanga ilishinda 1-0. Picha na Jackson Odoyo.
  Sosthenes Nyoni
MSHAMBULIAJI Hamis Kiiza aliyeingia kutokea benchi aliiongoza Yanga kuichapa JKT Oljoro kwa bao 1-0, katika mchezo ulioshudiwa na mashabiki ni wengi kwenye Uwanja wa Azam Chamazi.

Kiiza aliyeingia kuchukua nafasi ya Jerryson Tegete katika dakika 61, alimsha shangwe za mashabiki wengi wa mabingwa hao katika dakika 86 akimalizia kazi nzuri ya Haruna Niyonzima.

Kwa ushindi huo Yanga sasa imefikisha pointi 21 na kushika nafasi ya pili  sawa na Azam yenye pointi 21 lakini wama kutofautia kwa mabao.

Kocha Sam Timbe baada ya kukubwa na madai ya kutimuliwa kutokana na kukoseka kwenye benchi katika mchezo wao dhidi Toto African  jana Mganda alikuwa wepo uwanjani hapo  kuwaongoza mabingwa hao kupata pointi tatu muhimu.

Timbe alisema mchezo ulikuwa mgumu kwao, lakini anashukuru wamefanikiwa kupata pointi tatu muhimu kabla ya mechi yao dhidi ya Simba hapo Jumamosi.

Mshambuliaji Asamoah alikosa bao dakika 19 kwa shuti lake kugonga mwamba na kurudi uwanjani alipounganisha krosi ya Shamte Ally kutoka winga ya kulia.

Kipa wa JKT Oljoro, Said Salehe alifanya kazi nzuri dakika 27, 30, kudaka shuti la umbali wa mita 20 lililopigwa na Oscar Joshua na mpira wa kichwa wa Shamte.

Kiungo Haruna Niyonzima akiwa umbali wa mita 25 alipiga shuti kali lilipanguliwa na kipa Salehe aliyekuwa kikwazo kwa Yanga katika kipindi cha kwanza kilichotawaliwa na mabingwa hao.

Washambuliaji wa Yanga,Jerryson Tegete, Shamte na Asamoah walioneka kukosa mbinu ya kuipenya ngome ya Oljoro iliyoruhusu mabao nne tu tangu kuanza kwa ligi msimu huu.
Kocha wa Oljoro amempumzisha Ally Kani na kumwingiza Frank George ambaye dakika 52 alionyeshwa kadi ya njano na mwamuzi Abdalah Kambuzi kutoka Shinyanga kwa kumchezea vibaya Niyonzima.
Asamoah alipoteza nafasi ya kufunga dakika 55 kwa shuti lake kumgogo kipa Salehe na kutoka na kuwa kona ambayo haikuwa na madhara.
Mchezaji  Sunday Musa wa Oljoro walikosa bao dakika 60, baada ya kuwatoka mabeki wa Yanga, lakini kipa Yaw Berko alikuwa makini kuwahi kucheza mpira huo.

Timbe alimpumzisha Shamte na Tegete na kuwaingiza Hamis Kiiza na Rashidi Gumbo mabadiliko hayo yalikuwa na faida kwa Yanga.

Dakika ya 86 Kiiza alifungia Yanga bao kuongoza kwa shuti kali la pembeni akimalizia pasi ya Niyonzima aliyewazidi ujanja mabeki wa Oljoro.
Akizungumzia mchezo huo kocha wa Oljoro, Ally Mohamed aliyepoteza mechi ya pili tu hadi sasa dhidi ya Simba na Yanga alisema ameridhishwa na kiwango cha wachezaji wake na kufungwa ni sehemu ya mchezo.

Wakati huo huo; Juma Mtanda anaripoti Katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Jamhuri timu ya Polisi Morogoro ilichakaza AFC ya Arusha kwa mabao 2-0.

Polisi walipata bao la kwanza dakika ya tisa kupitia Juma Maboga kwa mpira wa adhabu uliombabatiza beki wa AFC na kuingia goli, dakika 81, Nicolaus Kabipe aliunganisha vizuri krosi ya Hassan Kodou kuandika bao la pili kwa wenyeji.

chanzo na
www.mwananchi.co.tz

No comments: