Oct 10, 2011

MTIBWA WAPIGISHWA KWATA NA JKT RUVU



JKT Ruvu imeichapa Mtibwa Sugar mabao 3-2 katika mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania iliyochezwa kwenye uwanja wa Azam, Chamazi jijini Dar es Salaam.Kwa ushindi huo klabu ya JKT Ruvu imefikisha pointi 15 kama ilizonazo klabu za Mtibwa Sugar na Azam.
Mtibwa ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya tisa lililofungwa na Vicent Barnabas aliyeunganisha krosi ya Issa Rashid.JKT Ruvu walisawazisha bao hilo katika dakika yabaada ya Mtibwa kujifunga wenyewe wakizembea kuondoa mpira wa kona.
JKT Ruvu pia waliongeza bao la pili kupitia kwa Rajab Chau aliyepokea mpira wa faulo ndogo uliopigwa na Emmanuel Linjechele.Timu hizo mpaka zinaenda mapumziko JKT Ruvu ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-1, lakini katika kipindi cha kwanza timu zote zilicheza kwa kushambuliana.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ya wachezaji, lakini mabadilko hayo yalionekana kuwasaidia zaidi JKT Ruvu kwa sababu walipata penati katika dakika ya 85 ambayo ilifungwa na Stanley Nkomola na kuandika bao la tatu.
Penati hiyo ilipatikana baada ya Hussein Bunu kudondoshwa na Salvatory Ntebe katika eneo la hatari na mwamuzi Amon Paul wa Mara aliamuru ipigwe penati.Slavatory Ntebe aliipatia Mtibwa bao la pili katika dakika ya 89 baada ya kupiga shuti kali lililomshinda kipa wa JKT, Hamis Seif.
Ligi Kuu itaendelea tena Oktoba 14 kwa Yanga kucheza na Kagera Sugar, halafu Oktoba 15 JKT Ruvu itacheza na Azam, pia Oktoba 16 Simba itacheza na African Lyon.

chanzo na shaffidauda.blogspot.com

No comments: