Oct 18, 2011

Zitto aingia kwenye utawala wa soka la bongo

Mbunge mwenye makeke bungeni toka Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ameingia kwenye tawala za soka la bongo baada ya kuteuliwa kuwa mmoja wawajube wapya wa Simba sambamba na Mbunge wa Mvomero Amos Makala.

Mwenyekiti wa klabu ya Simba ambaye ni mbunge, Ismail Rage, alizitaja kamati zilizo pitishwa katika kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika Jumamosi ya Oktoba 15 ambapo kumefanyika mabadiliko katika kamati mbalimbali.

Kamati hizo ni:

KAMATI YA FEDHA:
Mwenyekiti: Geofrey Nyange 'Kaburu'
Makamu mwenyekiti: Adam Mgoyi
Wajumbe: Said Pamba, Juma Pinto na Zitto Kabwe.

KAMATI YA MASHINDANO:
Mwenyekiti: Joseph Itang'are
Makamu Mwenyekiti: Azim Dewji
Wajumbe: Jarry Ambe, Swedy Nkwabi, Hassan Hasanoo, Mohamed Nassor, Richard Ndasa na Suleiman Zakazaka.

KAMATI YA UFUNDI:
Mwenyekiti:Ibrahim Masoud,
Makamu Mwenyekiti: Evance Aveva
Wajumbe: Danny Manembe, Khalid Abeid, Musley Luwey, Mulamu Nghambi, Said Tuli, Rodney Chiduo, Patrick Rweyemamu.

KAMATI YA USAJILI:
Mwenyekiti: Zakaria Hans Poppe,
Makamu mwenyekiti: Kassim Dewji
Wajumbe: Francis Waya, Crecensies Magori, Salim Abdallah, Collins Fransch na Gerald Lukomay.

KAMATI YA NIDHAMU:
Peter Swai, Jamal Rwambo, Charles Kenyela, Evody Mmada na Chaurembo.


Rage alisema kamati hizo zimeanza kazi zake mara moja kwa kuwa kila mjumbe tayari ameshakabidhiwa barua yake.


Katika hatua nyingine Rage alisema kuwa kundi la marafiki wa Simba (friends of Simba) ambalo linafanyakazi pega kwa pega na Simba SC wamemaliza tofauti zao.
chanzo na aboodmsuni.blogspot.com

No comments: