Nov 1, 2011

Papic asajili silaha tatu mpya yanga

MWANDISHI WETU
YANGA itaongeza wachezaji watatu katika dirisha dogo la usajili ambalo linaanza leo Jumanne ili kuongeza nguvu katika kikosi chake.

Akizungumza na Mwanaspoti jana Jumatatu, Kocha wa Yanga, Kosta Papic alisema wachezaji wote wa kigeni waliopo katika timu hiyo wapo salama, lakini atapunguza wachezaji watatu wa Tanzania na kuleta wengine watatu kutoka nchini.

"Hakuna ubishi tutasajili wachezaji watatu, na kuwaondoa watatu. Wachezaji wote wa kigeni tutaendelea kuwa nao kwa sababu wana umuhimu mkubwa katika kikosi chetu," alisema Papic ambaye timu yake itacheza na Polisi mjini Dodoma kesho Jumatano.

Kocha huyo wa Serbia alifafanua kuwa baada ya mchezo wao na Polisi, watakuwa katika mazingira mazuri ya kujua wachezaji wanaowaacha na wanaowasajili.
"Kuna nafasi zina upungufu, hatuna budi kuongeza nguvu, tutahakikisha tunazitumia siku 30 hizi za usajili kuimarisha kikosi chetu," alisema.

Mwanaspoti linajua kuwa Godfrey Bonny, Fred Mbuna, Zubery Ubwa na Abuu Ubwa wapo katika hatari kubwa ya kupigwa mstari mwekundu.

Wachezaji wa kigeni ambao Papic amewahakikisha usalama ni Yaw Berko (Ghana), Davies Mwape (Zambia), Kenneth Asamoah (Ghana), Haruna Niyonzima (Rwanda) na Hamisi Kiiza (Uganda).

Akiizungumzia mechi dhidi ya watani wao Simba waliyoshinda bao 1-0 mwishoni mwa wiki, Papic alisema ilikuwa mechi nzuri kwa pande zote mbili.

"Katika Afrika ile inaweza kuwa miongoni mwa mechi nzuri kabisa za watani, mara nyingi mechi za watani huwa zinakuwa na presha kubwa, lakini ile ilikuwa mechi nzuri kwa pande zote," alisema Papic, mwenye uzoefu wa bara la Afrika kwa miaka 15.

Alisema alimpanga Mwape ambaye kwa muda mrefu alikuwa majeruhi baada ya kuzungumza naye na kukubali kucheza.

"Sikumlazimisha kucheza, nilimuuliza kama yupo tayari, akanihakikisha kuwa yupo tayari kwa mchezo, nikampanga na akaleta ushindi," alisema Papic.

Papic ni mzoefu wa mechi za watani kwani amefundisha soka katika nchi mbalimbali Afrika ambako kuna mechi ngumu za watani.

Alifundisha Lobi Stars, Enugu Rangers na Enyimba za Nigeria, Kaizer Chiefs, Orlando Pirates na Martizburg za Afrika Kusini, Hearts CHANZO NA http://www.mwanaspoti.co.tz
  

No comments: