Jan 30, 2012

BONDE FC NDANI YA TFF



Bonde fc yaendeleza ubabe wake kwa timu za Ilala

Timu ya Bonde fc ilionyesha kuwa wao ni moto wa kuotembali baada ya siku ya jumamosi kufanikiwa kuitandika timu ya Tabata kids kwa jumla ya goli 3-2 katika mchezo mzuri na wakuvutia uliochezwa katika uwanja wa kumbukumbu ya rais wa kwanza wa Zanzibar ABED AMAN KARUME (TFF) hiyo ilikuwa kwa under 17.


Nao wadogo zao waliendeleza ubabe wao baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya timu ya Buguruni Kids. Mechi zote hizi ni kwa ajiri ya ujirani mwema ambao Bonde fc imepewa na chama kuendeleza soka wilaya ya Ilala na pia ikiwa ni maandalizi kwa ajiri ya michuano ya vijana inayotarajiwa kuanza wiki ijayo
 JUU NI KIKOSI CHA BONDE FC UNDER 17
NA CHINI NI KIKOSI CHA UNDER 14  picha na shakeel shabani kpl

Jan 14, 2012

Bonde Fc kujipinga nguvu dhidi ya Shean Rangers

Timu ya Bonde fc hapo kesho inatarajia kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya wapinzani wao wa jadi timu ya Sheani Rangers ya Sinza mechi itachezwa katika uwanja wa TP Sinza hivyo watu wote mnakaribishwa kuja kushuhudia vijana wakionyeshana ufundi.
   
Akiongea na chumba cha habari cha timu hii kocha mkuu wa timu bwana Issa Joseph alisema timu yake iko katika hali nzuri hakuna majeruhi mpaka sasa na kwamba mechi ya kesho atawapanga pia vijana wapya waliojiunga na timu hiyo hivi punde.

Nae msemaji wa Sheani Rangers anasema timu yake imejiaanda vya kutosha na kwamba wako tayari kuendeleza ubabe wao kwa timu ya Bonde Fc hapo kesho.

 Kesho kutakuwa na mechi mbili moja itahusisha vijna umri chini ya miaka 14 na nyingine ni chini ya miaka 17 hivyo watu wote mnakaribishwa kuja kuona vijana  wakioneshana ufundi


Picha kushoto ni vijana wa Bonde fc na Sheani Rangers siku zilipokutana kwenye fainali.hapa  wakikaguliwa na mwenyekiti wa chama cha cha kuendeleza soka la vijana mkoa (DAYOSA)