Timu ya Bonde fc ilionyesha kuwa wao ni moto wa kuotembali baada ya siku ya jumamosi kufanikiwa kuitandika timu ya Tabata kids kwa jumla ya goli 3-2 katika mchezo mzuri na wakuvutia uliochezwa katika uwanja wa kumbukumbu ya rais wa kwanza wa Zanzibar ABED AMAN KARUME (TFF) hiyo ilikuwa kwa under 17.
Nao wadogo zao waliendeleza ubabe wao baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya timu ya Buguruni Kids. Mechi zote hizi ni kwa ajiri ya ujirani mwema ambao Bonde fc imepewa na chama kuendeleza soka wilaya ya Ilala na pia ikiwa ni maandalizi kwa ajiri ya michuano ya vijana inayotarajiwa kuanza wiki ijayo
JUU NI KIKOSI CHA BONDE FC UNDER 17NA CHINI NI KIKOSI CHA UNDER 14 picha na shakeel shabani kpl
No comments:
Post a Comment