Timu ya Bonde fc hapo kesho inatarajia kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya wapinzani wao wa jadi timu ya Sheani Rangers ya Sinza mechi itachezwa katika uwanja wa TP Sinza hivyo watu wote mnakaribishwa kuja kushuhudia vijana wakionyeshana ufundi.
Akiongea na chumba cha habari cha timu hii kocha mkuu wa timu bwana Issa Joseph alisema timu yake iko katika hali nzuri hakuna majeruhi mpaka sasa na kwamba mechi ya kesho atawapanga pia vijana wapya waliojiunga na timu hiyo hivi punde.
Nae msemaji wa Sheani Rangers anasema timu yake imejiaanda vya kutosha na kwamba wako tayari kuendeleza ubabe wao kwa timu ya Bonde Fc hapo kesho.
Kesho kutakuwa na mechi mbili moja itahusisha vijna umri chini ya miaka
14 na nyingine ni chini ya miaka 17 hivyo watu wote mnakaribishwa kuja kuona
vijana wakioneshana ufundi
Picha kushoto ni vijana wa Bonde fc na Sheani Rangers siku zilipokutana kwenye fainali.hapa wakikaguliwa na mwenyekiti wa chama cha cha kuendeleza soka la vijana mkoa (DAYOSA)
No comments:
Post a Comment