Raisi huyo wa Shirikisho la Vyama vya
soka barani Ulaya (UEFA), akiongea kwenye mkutano uliofanyika mjini
Zurich jana, alisema kuwa, mpango wa kuvidhibiti vilabu ambavyo vimekuwa
vikifanya matumizi makubwa ambayo ni nje ya uwezo wake wa uzalishaji,
uko palepale na kwamba utaanza kutumika kwenye msimu wa mwaka 2012/13,
kama ambavyo imeshakubaliwa.
Chini ya mpango huo, vilabu
havitaruhusiwa kufanya manunuzi ya wachezaji au kulipa mishahara mikubwa
kwa wachezaji wao zaidi ya kile klabu inachoingiza kama mapato yake
kutokana na mikataba mbalimbali ya kibiashara na vyanzo vyao vya mapato
na kwamba vilabu ambavyo vitashindwa kutimiza sharti hilo, vitafungiwa
kushiriki michuano yoyote ya Ulaya katika ngazi ya vilabu.
Akizungumza katika mkutano huo, Platini,
gwiji wa zamani katika kikosi cha Ufaransa na vilabu mbalimbali
alitolea mfano wa klabu ya soka ya Arsenal, ambayo alisema kuwa miaka
kumi iliyopita, mzunguko wake wa fedha kwa mwaka ulikuwa chini sana
kiasi cha kupitwa na vilabu kama Chelsea, Liverpool na Newcastle, lakini
kutokana na mipango mizuri na matumizi sahihi ya fedha, leo hii klabu
hiyo imekuwa juu ya vilabu hivyo kwa karibu mara mbili kiuchumi.
No comments:
Post a Comment