Mshambuliaji mpya wa Arsenal Chu-Young
Park, amesherehekea kutimia kwa ndoto yake ya kuwachezea washika bunduki
hao wa London, kwa kuiongoza nchi yake ya Korea Kusini kuibuka na
ushindi wa bao 6-0 dhidi ya Lebanon, katika michuano ya kuwania kufuzu
fainali zijazo za kombe la dunia.
Park, ambaye alitua Arsenal hivi
karibuni akitokea Monaco ya Ufaransa, aliwaonyesha mashabiki wa Arsenal
kuwa huenda akawa tiba ya timu yao kushindwa kupata mabao katika baadhi
ya nyakati, baada ya kutikisa nyavu mara tatu kwenye mechi hiyo
iliyofanyika leo huko nchini kwao.
Pak, alifunga mabao yake kunako dakika
za 8, 45 na 67, huku mabao mengine yakiwekwa nyavuni na Don Won Ji (66
na 85) pamoja na Jung Woo Kim, aliyefunga bao moja kunako dakika ya 82.
No comments:
Post a Comment