Sep 3, 2011

Yossi Benayoun amwaga wino Arsenal

Yossi Benayoun, anaelezwa kuwa mchezaji ambaye ataleta kitu muhimu kwa Arsenal kutokana na aina yake ya uchezaji na aina ya uchezaji wa Arsenal kama timu
Hatimaye Arsene Wenger ameibuka na kicheko dhidi ya mahasimu wake Liverpool na Tottenham Hotspurs, baada ya kufanikiwa kuinasa saini ya kiungo Yossi Benayoun, toka Chelsea.
Dilila kumsaini mchezaji huyo ambalo lilionekana kushika kasi saa chache zilizopita baada ya Arsenal kuelekea kumkosa Mikel Arteta, lilikuwa likiendeshwa kimya kimya sana ukiachilia mbali taarifa zilizokuwa zikitolewa na mchezaji huyo mwenyewe kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Haijawekwa wazi dau lake na lakini inaelezwa kuwa amesaini kwa mkopo wa muda mrefu ambao unaweza kugeuzwa kuwa wa kudumu na bila shaka hizi ni habari njema sana kwa mashabiki wa Arsenal ambao walichokuwa wakiangalia ni kuimarishwa kwa kikosi chao kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Benayoun mwenyewe amezungumzia usajili huo kwa ufupi sana katika ukurasa wake wa Twitter ambako ameandika “I sign with arsenal,very happy and excited about it,but now my head is only in the game against grecce on friday,thanks for the support”.
Je, ni nani atasaini dakika hizi takriban 20 zilizobaki? Ni Arteta, ambaye amelazimisha Everton wamuachie baada ya awali kukataliwa kwa maombi ya Wenger au basi ndio kocha huyo Mfaransa kafunga duka? 

No comments: