Oct 20, 2011

Timbe amtolea uvivu Kiiza

Jackson Odoyo
KATIKA kuonyesha hataki mzaha, kocha wa Yanga Sam Timbe, jana alijikuta akimfokea vikali winga wake Hamisi Kiiza baada ya kwenda kinyume na maelekezo wakati wa mazoezi ya timu hiyo.Ukali Timbe ulimpelekea kuongea kwa hasira huku akichanganya lugha kwa wakati mmoja, yaani Kiingereza, Kiswahili na Kiganda.
Winga huyo raia wa Uganda wakati wa  mazoezi ya asubuhi Uwanja wa Kaunda alifanya kosa lililompelekea Timbe kupandwa na hasira.
Kosa la Kiiza ilikuwa ni kushindwa kutafuta nafasi ili apokee pasi kutoka kwa Jerry Tegete aliyekuwa na mpira huku akizongwa na mabeki wa timu nyingine.
Kiiza alishindwa kutafuta nafasi ya kupokea pasi badala yake alichukua mpira mguuni mwa Tegete ili asitoe pasi kwa mchezaji mwingine na mwisho akapoteza mpira kirahisi.
Baada ya kosa hilo Timbe alimuuita kwa hasira kwa lugha ya Kiswahili Kiingereza na Kiganda na baada ya mchezaji huyo kufika mbele yake aliendelea kumfokea kwa hasira huku akichanganya lugha hizo tatu.
chanzo na www.mwananchi.com

No comments: