WAANDISHI wa Habari mbalimbali wa Afrika Mashariki, wamesisitiza kwamba Ligi Kuu Tanzania Bara itapiga hatua kama itaendeshwa na kampuni kuliko kamati au Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Wakizungumza na Mwanaspoti kwa nyakati tofauti, waandishi hao mahiri kutoka Uganda, Kenya na Rwanda, wametoa maoni tofauti hasa wakitolea mfano ligi zinavyoendeshwa katika nchi zao na nyingine zenye mfumo huo wa kisasa. James Waindi wa Standard la Kenya alisema: �Kampuni itakuwa makini zaidi na itaendesha mambo kitaaluma na kibiashara kuliko ilivyo sasa. �Hata wadhamini wengi watajitokeza kwa vile siasa zitapungua na klabu zitapata nafasi ya kufanya mambo kwa uwazi zaidi. �Shirikisho lilipokuwa linaendesha ligi hapa Kenya, ilikuwa ni matatizo. Timu zilikuwa haziwezi hata kulipa mishahara, lakini baada ya kuingia Kampuni (KPL), Supersport imeingia na kutoa fedha kwa klabu zote. �Klabu sasa zinapata kama Sh 55 milioni za Kenya (Sh 982 milioni) kwa msimu, ambayo haikuwapo awali. �Matangazo ya Supersport pamoja na promosheni inayofanywa na KPL imeongeza msisimko na kufanya mashabiki matajiri na makampuni kuingiza fedha kwenye timu. �Hali hii haikuwapo kipindi cha KFF. Hivi sasa Gor Mahia, AFC Leopard zinaleta watu wengi sana uwanjani, hicho kitu kilishafutika enzi za KFF. �Kampuni ikiingia Tanzania itafuta ukiritimba wa Simba na Yanga, hata Coastal Union au Villa Squad zitakuwa na fedha na nguvu ya kuzifunga Simba na Yanga na wachezaji watalipwa vizuri. TFF ina matakwa binafsi mara nyingine.� Isaack Mukasa wa redio VOA FM ya Kampala, Uganda alisema: �Uganda Super League Ltd ndiyo inayoendesha Ligi Kuu hapa, kila klabu inapata Sh 78 milioni za Uganda (Sh 51.8 milioni) kutoka Kampuni ya Bia ya Uganda na Supersport. �Fedha hizo hazikuwepo wakati Fufa inaongoza ligi. Angalia ligi zote za Afrika zilizoendelea na hata Ulaya, kuna kampuni inaongoza. �TFF iziache klabu ziunde kampuni yao ya kuongoza ligi, hapa Uganda siku hizi hakuna cha Villa wala URA zote zinapigwa na klabu ndogo kwa sababu ya fedha za udhamini ambazo zimeongeza morali kwa wachezaji. �Kampuni nyingi zinapenda kufanya kazi na taasisi za biashara na si watu wa kuchaguliwa au vikundi vya watu fulani. �Ikiingia kampuni kwa sehemu kama Tanzania ambako watu wanapenda soka, klabu zitanufaika sana na hata zawadi za ligi zitaongezwa.� Bonnie Mugabe wa Newtimes la Kigali, Rwanda naye alisema: �Kampuni kuendesha ligi ni sahihi kabisa kwani shirikisho lina mambo mengi. �Kampuni ikiruhusiwa, ligi itakuwa ya kulipwa na yenye maslahi zaidi kwa klabu zenyewe na wachezaji, ili mradi kampuni iwe na sera, malengo na misingi imara. �Kampuni itaendesha ligi kisasa na kupata wadhamini wengi wakubwa, lakini hiyo kampuni lazima iwe sehemu ya shirikisho, isimiliki ligi kwa asilimia 100. Shirikisho libaki na sehemu yake.� Bonnie ni Mhariri wa gazeti la hilo la michezo la kila siku. Lakini mtangazaji wa Contact FM ya Kigali, Rwanda, Kazungu Clev, alitofautiana na wenzake akisema: �Ligi ya Tanzania bado iko juu kwenye ukanda huu na sidhani kama kampuni inaweza kuongeza chochote hapo. �TFF iendelee kuongoza ligi, lakini Kamati ya Masoko ifanye kazi yake kuongeza wadhamini. Mkiruhusu kampuni, Simba na Yanga zitazidi kutawala zitaminya klabu ndogo na mianya ya rushwa itaongezeka. �Bora sasa kwani klabu zinadhibitiwa kirahisi na TFF. Kinachotakiwa ni mpira uwepo na fedha ziwepo.�chanzo na http://www.mwanaspoti.co.tz |
||
MICHEZO NI UMOJA NA MSHIKAMANO WEKEZA KATIKA MICHEZO ILI KUOKOA VIPAJI VYA VUJANA VISIISHIE KWENYE KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA UJAMBAZI NA UKABAJI
Nov 5, 2011
Afrika Mashariki waipinga TFF
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment