Nov 5, 2011

Waghana wafunga virago Azam

DORIS MALIAYAGA
WAGHANA wanaochezea Azam FC, Nafiu Awudu na Wahab Yahaya, wamenyoosha mikono na kufungasha virago na kurejea kwao.

Nafiu anayecheza nafasi ya beki na Wahab, ambaye ni mshambuliaji, waliondoka Jumatano iliyopita.

Akizungumza na Mwanaspoti, Nafiu alisema ameamua kuondoka kwani soka la Tanzania limenishinda.

�Mambo ni mengi, unacheza bila kujielewa, kuna mambo mengi yametokea, ambayo siwezi kueleza,� alisema Nafiu, ambaye anaelezewa kuwa mcha Mungu.

Alisema uwanjani ligi ya Tanzania si ngumu, ila amechoshwa na mambo yanayoendelea katika timu.

Aliongeza: �Nimeshamalizana na Azam na sina ninachodai, narudi nyumbani kufanya mipango mingine.

�Nategemea kwenda Afrika Kusini au Croatia kwani kabla ya kuja Azam kuna timu zilikuwa zikinitaka. Sasa nakwenda kufanya mipango mengine.�

Wahab naye kwa upande wake, alisema anayo mipango mingine. �Mambo ndiyo kama hivyo, mtanisikia kwenye vyombo vya habari nikiweka mambo yangu sawa.�

Kuondoka kwa Waghana hao, kunaifanya Azam kubakiwa na wachezaji watatu wa kigeni. Hao ni Obren Cirkovic wa Serbia, Kipre Tchetche wa Ivory Coast na Ibrahim Shikanda wa Kenya.

Pia kuondoka kwa Waghana hao, kunafungua njia ya beki wa zamani wa Simba, Joseph Owino kutua katika timu hiyo.

Owino aliachwa na Simba kutokana na kukabiliwa na maumivu ya goti yaliyomweka nje msimu mzima.
Lakini kuna habari Azam inajipanga kumsajili katika kipindi hiki cha dirisha dogo.chanzo na http://www.mwanaspoti.co.tz 

No comments: