Nov 5, 2011

Asamoah kufanya kufuru

Kenneth Asamoah
DORIS MALIYAGA, aliyekuwa Dodoma
MSHAMBULIAJI hatari wa Yanga, Kenneth Asamoah, ameapa kutumia mapumziko ya Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa kwao huku akifanya mambo ambayo anasema akirejea, hakutakuwa na wa kumsogelea katika ufungaji, akiwamo mkali wa Simba, Felix Sunzu.

Mghana huyo mwenye mabao manane kwenye msimamo wa wafungaji akifungana na John Boko �Adebayor� wa Azam FC, alisema haoni wa kumtisha kwa vile anajua atakachokifanya kukoleza makali yake. Sunzu ana mabao matano.

�Najiamini naweza kuwa Mfungaji Bora, lakini kubwa Mungu anilinde na mambo mengine maana unaweza kupanga hili na yeye anapanga jingine,� Asamoah alisema.
�Ninaenda nyumbani kujifua zaidi ili nikija niwe na kasi mpya ni mabao kwenda mbele.�

Asamoah ametua Yanga msimu huu baada ya usajili wake kukwama msimu uliopita, alipokosa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC).

Akimzungumzia Boko alisema: �Hilo haliniumizi kichwa hata kidogo kwa sababu naamini ninachokifanya.

�Atakayenifananisha mimi na yeye anakosea, angalia mwenzangu amecheza mechi ngapi na kwa dakika ngapi, angalia na mimi muda niliocheza.

�Hatuko sawa na ndiyo maana nasema mzunguko wa pili nitamaliza kila kitu.�

Asamoah, ambaye ni kipenzi cha kocha wa sasa wa Yanga, Kostadin Papic, awali alikuwa akisumbuliwa na majeruhi akashindwa kuitumikia vizuri klabu hiyo.

Baada ya Boko na Asamoah wanaowafuata kwa ufungaji ni Gaudence Mwaikimba wa Moro United mwenye mabao saba.
Waliofunga mabao matano ni Emmanuel Okwi (Simba), Said Rashid (Mtibwa), Rajabu Chau (JKT Ruvu),
Mohamed Kijuso (Villa Squad), Said Dilunga (Kagera Sugar), Enyinna Darlington, Felix Sunzu na Patrick Mafisango (wote Simba).

Pia kuna Davies Mwape (Yanga), Juma Semsue (Polisi Tanzania) na Soud Mohamed (Toto African) ambao wamefunga mabao manne kila mmoja.

Naye Msaidizi wa Yanga, Fred Felix Minziro, amemsifu Asamoah na kusema maendeleo yake ni mazuri na kiwango chake kimekuwa kikibadilika siku hadi siku.chanzo na http://www.mwanaspoti.co.tz

No comments: