Hatimae timu ya bonde fc jana iliibuka na ushindi mnono wa goli 2-1 dhidi ya watoto wenzao wa Kimara fc katika mchezo huo uliokuwa wa kuvutia na wenye kila aina ya burudani na ulioshuhudiwa na mashabiki wengi sana ambao hawajawahi kutokea katika michuano hiyo ya TEWA CUP.
ilikuwa ni Kimara iliyokuwa ya kwanza kupata goli kupitia kwa mshambuliaji wao Omary Juma aliepiga shuti la mbali nje ya kumi na nane na kumshinda mlinda mlango wa Bonde fc Afidhi Juma na kuingia moja kwa moja nao Bonde fc ilipata goli la kusawazisha kupitia kwa Hassani Rashid Banda alieingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Afidhi Salum baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Mamani (Fundi) ambae kwa mechi ya jana ndio aliibuka kuwa mchezaji bora alikuwa Hassani tena alieinua mashabi wa soka baada ya kupiga goli la ushindi dakika ya 90 na kuifanya timu ya Bonde fc kuibuka na ushindi wa goli 2-1 na kwa matokeo hayo timu ya Bonde fc inakuwa imejiakikishia kutinga moja kwa moja hatua ya nusu fainali katika michuano hiyo inayoshilikisha timu za vijana chini ya miaka 14 (under 14) kikubwa kilichotokea jana ni jinsi vijana wa Bonde fc walivyokuwa wanasakata kabumbu safi hali iliyofanya mashabiki wote uwanjani kuweka ushabiki pembeni na kuanza kuwashabikia
No comments:
Post a Comment