Nov 21, 2011

Juma Kaseja ampoteza Fabregas


                                                                 




DORIS MALIYAGA 



KIPA namba moja wa Simba na Taifa Stars, Juma Kaseja, ndiye mkali wa mastaa wa Simba na Yanga, akimpiga bao hata kiungo hatari, Haruna Niyonzima �Fabregas� kwa kucheza mechi nyingi katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara 

Katika mzunguko huo, Kaseja, alicheza mechi zote 13 kwa dakika 90 ikimaanisha alikaa langoni kwa dakika 1170, hakuna mchezaji mwingine wa Simba na Yanga aliyefikia rekodi hiyo msimu huu hadi sasa.

Fabregas alicheza mechi 11. Mbili alizokosa, moja alikuwa akitumikia adhabu na nyingine alichelewa kurudi kutoka kwao Rwanda, alikokuwa na majukumu ya timu yake ya taifa.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kaseja ambaye ni nahodha wa Simba alisema: Siri ya mafanikio ya kucheza mechi zote ni kutokana na mazoezi na kufuata maelekezo ya kocha, lakini pia najitunza.

Siyo kwamba najua sana, ingawa nafahamu watu wataongea sana, lakini haya yote yanatokana na imani ya kocha kwangu.
Katika mechi hizo 13, Kaseja amefungwa mabao manane tu.
Beki wake wa kati, Juma Nyosso na kiungo Jerry Santo, wao walikosa mchezo mmoja. Nyosso alikosa mechi kutokana na kuonyeshwa kadi mbili za njano wakati Santo alishindwa kucheza kutokana na kuumia.

Kwa upande wa Azam FC ni Aggrey Morris na Ramadhani Chombo �Redondo� tu ndiyo waliocheza mechi zote, sawa na Ibrahim Mwaipopo na John Boko Adebayor, lakini wao hawakumaliza dakika 90 katika michezo miwili.

Kwa upande wa Mtibwa Sugar, beki wa kati Salvatory Ntebe na Juma Abdul ndiyo wamecheza mechi nyingi, walicheza mara 12.
MWISHO.  chanzo na http://www.mwanaspoti.co.tz

No comments: