Nov 22, 2011

Muundo wa kampuni ya ligi Kuu

          Muundo wa kampuni ya ligi Kuu
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Ligi kuu TPL atakuwa kiongozi wa Juu wa Klabu iliyoshinda ubingwa Ligi Kuu msimu uliotangulia
Makamu wenyeviti watatu wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya ligi kuu TPL ni (viongozi wa juu wa timu mbili zilizoshika nafasi ya pili na tatu na Makamu wa pili wa Rais TFF anayewakilisha vilabu
Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Ligi kuu inahusisha wenyeviti au wakurugenzi au kiongozi wa juu wa vilabu vyote 14 (16) vinavyocheza ligi kuu, (kila klabu itatoa mjumbe mmoja) TFF pia itakuwa na hisa kwenye kampuni ya ligi kama klabu na itakuwa na mjumbe mmoja kwenye bodi ya wakurugenzi wa kampuni. Wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya ligi ambao hawatapiga kura ni pamoja na Mjumbe mmoja toka chama cha wanasoka wa kulipwa, chama cha waamuzi FRAT, chama cha makocha TAFCA na Wadhamini wa ligi kuu
Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya ligi inapaswa kukutana wiki ya mwisho ya mwezi July (kabla ligi haijaanza) na wiki ya mwisho ya mwezi Januari (kabla raundi ya pili haijaanza )kila mwaka
Wajumbe wa kamati tendaji wa kampuni ya ligi inahusisha angalau kiongozi mmoja wa kila timu inayoshiriki ligi kuu, mwakilishi kutoka shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF, chama cha makocha, chama cha waamuzi, na wawakilishi toka kwa wadhamini ambao hawatakuwa na nguvu ya kupiga kura. Wajumbe wa kamati hizi wanapaswa kukutana angalau kila baada ya miezi miwili.
Kamati kuu ya TPL inahusisha Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa TPL, Makamu wenyeviti wa bodi ya wakurugenzi wa TPL, na wajumbe watatu watakaochaguliwa na bodi ya wakurugenzi. Kazi kuu ya kamati kuu ya TPL ni kuhakikisha sera zilizopitishwa na TPL zinatekelezwa na secretariet ya TPL.
Kamati ya Ufundi na Maendeleo ya TPL itahusisha mameneja na makocha wakuu wa vilabu vyote vinavyocheza ligi kuu na Mkurugenzi wa ufundi TFF kama wapiga kura sambamba na Mwakilishi wa chama cha makocha, na chama cha wachezaji wa kulipwa ambao hawatapiga kura.
Kutakuwa na kamati huru ya nidhamu na rufaa ambayo itateuliwa na Bodi ya wakurugenzi ya TPL kila mwaka. Maamuzi ya kamati hii yatapaswa kutekelezwa na klabu zote zinazoshiriki ligi kuu lakini yanaweza kupigwa kwenye kamati ya nidhamu na Rufaa ya TFF.
Wajumbe wa kamati nyingine za TPL watateuliwa na bodi ya wakurugenzi wa TPL

Uhusiano kati ya TPL na TFF



Makamu wa pili wa Rais TFF atapaswa kuwa mmoja wa makamu wenyeviti wa bodi ya wakurugenzi wa TPL lakini pia uchaguzi wa makamu wa rais wa TFF utafanywa na Bodi ya Wakurugenzi wa TPL au UTAFOC na kiongozi huyu atapaswa kuwa ama kiongozi wa juu wa klabu ya ligi kuu au ligi daraja la kwanza au Mmoja wa wanahisa wa Klabu inayoshiriki ligi kuu au ligi daraja la Kwanza.
TFF itakuwa na hisa kwenye kampuni ya TPL na itakuwa na mwakilishi atakayepiga kuea lakini hataruhusiwa kugombea nafasi yoyote ya uongozi na wala hatakuwemo kwenye kamati tendaji za TPL
TPL itapaswa kuwa mwanachama wa TFF kama ilivyo kwa TAFCA, FRAT nk
Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF ni mjumbe wa kamati ya ufundi na maendeleo ya TPL
Kamati ya watu watatu ya waamuzi itakuwa na mjumbe mmoja atakayeteuliwa na TFF
TPL itatambua na kuheshimu maamuzi ya kamati ya nidhamu na rufaa ya TFF endapo suala lililoshindwa kupatiwa ufumbuzi na kamati ya rufaa na nidhamu ya TPL litapelekwa huko.
TPL itapaswa kutoa asilimia ya hisa za TFF toka kwenye pato lake kwa TFF na vilabu vitapaswa kutoa asilimia tano (5%) pato la milangoni viwanjani.
Kamati ya ushirikiano kati ya TFF na TPL itaundwa wajumbe kumi (10) watano watakaoteuliwa na TFF na watano watakaoteuliwa na Bodi ya wakurugenzi ya TPL.

Kamati za TPL



Mkutano mkuu wa TPL unahusisha wenyeviti na makatibu wakuu wa vilabu vyote vya ligi kuu, Makamu wa Rais TFF anayewakilisha vilabu, Mjumbe moja toka Chama cha Wachezaji wa kulipwa, TAFCA na FRAT
Kamati tendaji ya TPL itaundwa na makatibu wakuu/ECO wa vilabu vyote vinavyoshiliki ligi kuu na TAFCA, FRAT na Chama cha wachezaji wa kulipwa
Kamati ya Fedha na Miradi itaundwa na wajumbe watatu toka vilabu vya TPL
Kamati ya Ufundi na maendeleo itaundwa na wajumbe watatu, mmoja toka TAFCA, Mkurugenzi wa ufundi TFF makocha au mameneja watatu watakaoteuliwa na TPL
Kamati ya Nidhamu na haki za wachezaji itaundwa na wajumbe watano ambao watateuliwa na Bodi ya wakurugenzi wa TPL

Secretariet



CEO – Aajiliwe toka nje ya Nchi, atakuwa mtendaji mkuu wa TPL
Bwana Fedha – awe qualified accountant
Meneja masoko – Aajiliwe toka nje ya nchi, afanye kazi kwa kushirikiana na makampuni ya masoko ambayo yatalipwa kamisheni ya biashara watakayoingiza
Mhariri mkuu na meneja mawasiliano TPL - atafanya kazi kama afisa habari na meneja mawasiliano wa TPL, pia atatunza rekodi na taarifa zote zitakazohitajika kwa wana habari. Ataendesha tovuti ya TPL kwa kushirikiana na kampuni itakayoteuliwa kuendesha tovuti ya TPL. Atasimamia uandaaji wa vipindi vya TV vya TPL kwa kushirikiana na kituo cha televisheni kitakachokuwa na haki za matangazo ya TV



Chief Operations, Logistics & League liaison Officer, - 
   
atafanya kazi chini ya mratibu wa mashindano. Atashughulika na vilabu kuhakikisha viwanja vina viwango, mechi zinaanza kwa wakati, taratibu zote kabla ya kuanza kwa mechi zinafuatwa na haki za wadhamini wa ligi kuu zinalindwa.
Mkuu wa kitengo cha ufundi, ulinzi na usalama. Atafanya kazi chini ya Mratibu wa mashindano. Atahakikisha mambo yote ya kiufundi yanazingatiwa na wachezaji, makocha na waandishi wa habari wanapata ulinzi wa kutosha wakati wa mchezo wa ligi



Mratibu wa mashindano –
 
Atoke nje ya nchi. Atashughulika na mambo yote ya kiufundi kuanzia Usajili, Upangaji wa ratiba, utengenezaji wa kanuni za ligi, mafunzo kwa makocha, waamuzi, mameneja nk, na atawasimamia wahusika wa kipengele cha 5 na 6.

Udhamini



Ligi kuu itakuwa ni Brand name ya ligi itakayoendeshwa na TPL na kampuni ya TPL ingependa ligi hiyo iitwe Ligi Kuu isipokuwa tuu endapo atajitokeza mdhamini atakayenunua jina hilo kwa kipindi flani. Mdhamini atakayenunua jina la Ligi Kuu na kuweka la kwake ikiwemo kubadili logo ya ligi atalazimika kutumia logo ya Ligi Kuu kama frame ya logo yake mpya na atalazimika kuruhusu angalau kwa asilimia chache jina la ligi kuu kuendelea kutumika kwenye ligi.
Kampuni ya TPL itaruhusu ligi kudhaminiwa na wadhamini zaidi ya mmoja ambao wanafanya biashara zisizoshindana sokoni
Mdhamini yoyote wa ligi kuu atazuiwa kuweka logo ya kampuni yake kifuani lakini endapo mdhamini wa ligi kuu atatoa pesa kubwa ambayo bodi ya wakurugenzi wa TPL wataridhika kuvaa nembo yake, basi nembo hiyo itawekwa begani na siyo kifuani
Kutakuwa na wadhamini wadogo wadogo ambao watauziwa haki ya kutumia logo ya Ligi Kuu kwenye promosheni zao.
Kampuni ya TPL itawajibika kusaka mdau wa matangazo ya televisheni ili kuweza kupata pesa ya udhamini lakini nia kuboresha mazingira ya udhamini wa ligi kuu na udhamini wa vilabu.
Kwa kushilikiana na viongozi wa vilabu, meneja masoko wa TPL atakuwa na wajibu wa kuvsaidia vilabu kupata udhamini.
Kampuni ya ligi kuu TPL itashirikiana na makampuni ya masoko kusaka wadhamini

Mtaji wa kuanzisha Kampuni

Vilabu vitajitolea kucheza mechi za kuchangisha pesa kwa ajili ya kuanzisha kampuni. Muda muafaka kwa ajili ya Mashindano haya maalum yatakayoendeshwa na TPL uwe disemba 15 hadi 30 2011.

Mashindano haya yatatumika kama changamoto kwa kampuni kujifunza na kujiandaa kuendesha ligi kuu. Baada ya mashindano haya kampuni ya ligi kuu inaweza kuandaa mashindano mengine yatakayoenda sambamba na ligi kuu raundi ya pili ambayo yataitwa TPL Top 8 Knockout Tournament ambayo yatakuwa ni ya mtoano. Mashindano haya pia yatatoa changamoto kwa TPL kujifunza namna ya kuendesha ligi. Baada ya mashindano haya mawili ni imani yetu kuwa TPL itakuwa imeiva na tayari kuendesha Ligi Kuu

Katika mazingira kama haya ni lazima kampuni iwe imeshasajiliwa hadi kufikia muda huo na angalau CEO wa muda, bwana fedha na Mratibu wa mashindano wawe wameshaajiliwa (ajira ya uangalizi ya miezi mitatu)

Mashindano haya yatafanyika Dar es salaam, vilavu toka mikoani ambavyo havitakuwa na uwezo wa kushiriki mashindano haya kutokana na gharama havitadaiwa mtaji wa uanzishwaji wa kampuni.

Vilabu vyote vinavyocheza ligi kuu vitakuwa na hisa sawa kwenye kampuni. Hisa hizi hazitapatikana kutokana na klabu kununua hisa kwa pesa taslimu bali kutokana na kuwa mwanachama wa ligi kuu na pindi klabu inaposhuka daraja, hisa zake zitahamia kwa klabu iliyopanda daraja.

chanzo na Ligi Kuu Tanzania na  patrick Kahemele (PK)

No comments: