Nov 5, 2011

TFF, Mrwanda wachenjiana

MWANDISHI WETU
MSHAMBULIAJI, Danny Mrwanda, amesema amejitoa katika kikosi cha Taifa Stars kitakachochuana na Chad, lakini Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limedai mchezaji huyo hajatoa, ila ameondolewa.

Stars inawania kutinga hatua ya makundi ya kugombea tiketi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2014 .

Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, aliiambia Mwanaspoti jana Ijumaa kwamba Mrwanda hajaomba kujitoa, bali alikuwa hapatikani kwa mawasiliano yoyote yale, hivy kocha akaamuru aondolewe kwenye timu.

�Kocha alituambia tumwondoe na tumuite Boko kwa kuwa Mrwanda alikuwa hapatikani, kocha alituagiza hivyo na kama angekuwa amezungumza naye angetuarifu,� Osiah alisema.
�Kocha anasisitiza kwamba mchezaji yeyote ni lazima awe na mwamko na timu yake ya Taifa.

�Kila mara anatakiwa kufuatilia mambo yanavyoendelea. Sasa kwa Mrwanda haiko hivyo, hata kwenye simu hatumpati.�

Mrwanda aliiambia Mwanaspoti jana Ijumaa kupitia barua pepe kuwa amemwambia Poulsen kwamba hawezi kujiunga na Stars.

�Kwa sasa nasaka timu mpya kabla ya dirisha la usajili halifungwa, ndiyo sababu kubwa ya mimi kushindwa kutokea huko,� alisisitiza Mrwanda katika barua pepe hiyo.

Kuhusu kauli ya TFF kuwa hapatikani kwa mawasiliano yoyote, Mrwanda alisema: �Mbona wanawasiliana na Babi kupitia barua pepe yangu na kumtumia tiketi, inakuwaje hawanipati mimi?�

Mchezaji huyo aliyemaliza mkataba na DT Long ya Vietnam, aliwahi kuandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa mawasiliano wa Facebook kwamba anafikiria kujiondoa katika kikosi cha Taifa Stars ingawa hakuwahi kutekeleza azma yake.

Stars itakuwa ugenini dhidi ya Chad Novemba 11, kabla ya kurudiana siku tano baadaye jijini Dar es Salaam.
Endapo itaitoa Chad, itaingia Kundi C lenye timu za Gambia, Morocco na Ivory Coast ili kuwania kufuzu fainali hizo zitakazofanyika Brazil  chanzo na http://www.mwanaspoti.co.tz

No comments: