Juu na chini ni vijana wa bonde fc wakijifua kabla ya mechi
Timu ya Bonde fc inawatangazia mashabiki na wanachama wake kuwa itaanza mazoezi rasmi siku ya jumatatu. Akiongea na chumba cha habari kocha mkuu wa Bonde fc ndugu Issa Joseph amesema kuwa wataanza mazoezi rasmi siku hiyo ikiwa ni baada ya mapumziko ya sikukuu xmss na mwaka mpya hata hivyo kocha huyo alizidi kukipasha chumba cha habari kuwa mazoezi hayo watakuwa wakifanyia katika uwanja Magomeni Tuliani kufuatia uwanja wao wa nyumani kukumbwa na mafuriko hivyo amewahasa wachezaji kufika mazoezini siku hiyo pia wanawakaribisha mashabiki wa soka kuja kushuhudia