Mar 7, 2012

Samata afunika Mazembe






Mwandishi wetu

KLABU ya TP Mazembe ya DR Congo imetumia mwezi Februari kufanya utafiti kwa wachezaji wake walioitumikia klabu hiyo mwezi huo, huku Mbwana Samatta akiibuka kinara wa kupachika mabao kwa timu hiyo.

Katika utafiti huo uliofanywa na klabu ya TP Mazembe, takwimu zinaonyesha mshambuliaji Mbwana Samatta ameongoza katika kufumania nyavu, ambapo kati ya mabao 15 yaliyofungwa Samata amefunga matano.

Samata amewashinda Luka Lungu aliyefunga manne, Yannick Tusilu amefunga mawili, Treasury Mputu amefunga mawili, Guy Lusadisu amefunga moja na Eric Kanteng amefunga moja pia.

Kwa mujibu wa utafiti huo wa mwezi Februari wa TP Mazembe walitumia wachezaji 31 katika mechi tano, ambapo Samatta, Patrick Ilongo, Joel Kimwaki na Robert Kidiaba waliongoza kwa ubora baada ya kufanya vizuri katika mechi nne kati ya tano walizocheza. Wakati Treasury Mputu akifanya vyema katika mechi 3 kati ya 5, huku Thomas Ulimwengu akitumika kama mchezaji wa akiba.

Katika suala la kutoa pasi za mwisho za ushindi, mchezaji Treasury Mputu aliongoza kwa kutoa pasi sita akifuatiwa na Patrick Ochan pasi mbili, Eric Nkulukuta , Herve Ndonga, Samatta, Serge Lofo, Eric Bokanga, Thomas Ulimwengu na Treasury Salakiaku wote wamepiga pasi moja za mwisho za ushindi.

Kwa jumla, Samatta na Treasury Mputu ndiyo waliofanya vizuri katika takwimu za TP Mazembe, ambapo Samatta aliibuka katika ufungaji na Mputu katika utoaji wa pasi za mwisho za ushindi.             


chanzo na aboodmsuni na soka la bongo

No comments: