Mar 7, 2012

Yanga yaizidi Simba mapato Taifa


Yanga yaizidi Simba mapato Taifa

Vicky Kimaro
MECHI ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba na Kiyovu ya Rwanda imeingiza kiasi cha Sh 208 milioni, kikiwa ni pungufu ya kiasi kilichopatikana kwenye mechi ya Yanga na Zamalek ya Misri, ambapo zilipatikana Sh 280 milioni.

Katika mchezo huo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 na hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa mabao 3-1, kufuatia sare ya bao 1-1 katika mechi ya kwanza mjini Kigali, Rwanda wiki mbili zilizopita. Kwenye mechi ya Yanga dhidi ya Zamalek, timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1.

Simba itashuka dimbani kati ya Aprili 27, 28 na 29 kwenye Uwanja wa Taifa kucheza na Entente Setif ya Algeria katika raundi ya pili ya michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika CAF.

Katika taarifa iliyotolewa na wasimamizi wa mchezo huo, Prime Time Promosheni, mashabiki 34,506 waliingia uwanjani, wakati kwenye mechi ya Yanga, mashabiki 48,000 ndiyo walioingia.

Katika mchanganuo wa mapato baada ya kukata makato yote Simba imepata zaidi ya shilingi milioni 100.

VIP A zilichapishwa tiketi 740 na ziliuzwa tiketi 287, tiketi za bure 200 na tiketi 253 zilibaki. Kingilio cha Sh 30,000 zilipatikana Sh 8,610,000, wakati VIP B zilichapishwa tiketi 3,760 ziliuzwa 965, tiketi 92 zilikuwa tiketi za bure.

Kwa upande wa VIP C, kingilio kilikuwa sh 15,000 zilichapishwa tiketi 4,077 ziliuzwa 692 (50 tiketi za bure) zilizobaki 3,335 ambapo zilipatika Sh 10,380,000, viti vya Orange zilichapishwa tiketi 10,897 ziliuzwa tiketi 2,581 (26 tiketi za bure), zilibaki tiketi 8,290 kingilio kilikuwa ni Sh8,000 na zilipatikana Sh20,648,000. Viti vya Blue kingilio kilikuwa Sh5,000, zilichapishwa tiketi 36,640 ziliuzwa 29,981 na zilibaki tiketi 6,665, zilipatika Sh 149,905,000.chanzo mwanaspoti

No comments: