|
MICHEZO NI UMOJA NA MSHIKAMANO WEKEZA KATIKA MICHEZO ILI KUOKOA VIPAJI VYA VUJANA VISIISHIE KWENYE KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA UJAMBAZI NA UKABAJI
Mar 22, 2012
QPR YAICHAPA LIVERPOOL NA KUJIKWAMUA KUTOKA KUSHUKA DARAJA
QPR 3 Liverpool 2 YALEEE YALEEEEEEEEEEE TENA
SUPERSUB ... Jamie Mackie celebrates his winner
By PAUL JIGGINS
Last Updated:
22nd
March 2012
The James Bond star watched in disbelief as his beloved Reds threw away a two-goal lead.
Liverpool looked home and dry after goals from Sebastian Coates and Dirk Kuyt
saw them lead 2-0 with just 13 minutes remaining.
But sub Jamie Mackie's injury-time winner completed a remarkable comeback that
epitomised the Kop's Prem season and will give the Hoops hope for the rest
of theirs.
Victory lifted the R's out of the bottom three on a night that will long be
remembered in west London.
While Liverpool were left, once again, to rue a stack of missed chances.
You have to say, it is a good job that Kenny Dalglish is the manager. Were it
any other boss in charge the red half of Merseyside would be calling for his
head this morning.
SUPPORT ... Liverpool players wear t-shirts to send their best wishes to Fabrice Muamba
There was no sign of it with a quarter of an hour to go as Liverpool looked
comfortable at 2-0. But then Shaun Derry pulled one back with a 77th-minute
header and the Reds' wheels started to come off.
SWEET 'N SUAR ... Luis Suarez beats Nedum Onuoha but has his shot saved
It was a sweet moment for Cisse, who claimed this week he still does not know
the reason the club bombed him out in 2006.
STUNNER ... Sebastian Coates hits a screamer for Liverpool
It completely validated his manager Mark Hughes' decision to send him on in
place of ineffective skipper Joey Barton in the 62nd minute.
DOUBLE TROUBLE ... Dirk Kuyt celebrates after scoring Liverpool's second
Liverpool were making their first return to the capital since their Carling
Cup success over Cardiff at Wembley last month.
SHAUN FROM THE DEAD ... Shaun Derry heads in the first goal of a stunning QPR comeback
Luis Suarez looked most likely to break the deadlock but it was another
Uruguayan — Coates — who netted with the kind of spectacular volley QPR boss
Hughes was renowned for in his heyday.
OLD BOY ... Djibril Cisse scores QPR's equaliser against his old side
It seemed nothing could stop the Kop but once again they managed to snatch
defeat from the jaws of victory.
And as for their showbiz fan Craig — there was not even a Quantum of Solace.
MACK ATTACK ... Jamie Mackie stuns Liverpool with a stoppage-time winner
DREAM TEAM
STAR MAN - SHAUN DERRY (QPR)
QPR: Kenny 8, Young 6, Onuoha 6, Ferdinand 6, Traore 6 (Taiwo 7), Barton 5 (Mackie 5), Derry 8, Diakite 6, Taarabt 6, Zamora 6, Cisse 7 (Buzsaky 5). Subs not used: Cerny, Gabbidon, Bothroyd, Wright-Phillips.
Liverpool: Reina 7, Kelly 5 (Coates 7), Carragher 6, Skrtel 6, Enrique 7, Kuyt 7, Spearing 7, Adam 6 (Henderson 6), Downing 5, Gerrard 7, Suarez 8 (Carroll 5). Subs not used: Doni, Aurelio, Shelvey, Flanagan.
TEVEZ AREJEA MAN CITY YAIUA CHELSEA 2-1
Man City 2 Chelsea 1
VERY NAS ... Samir Nasri celebrates his dramatic winner
By SHAUN CUSTIS
Published:
21st
March 2012
AMAZING what can be achieved when you agree to do a bit of warming up and get on with the job you are paid for.
Mancini's men were a goal behind to Gary Cahill's deflected shot when Tevez
was summoned from the bench by the boss with 66 minutes gone — and this time
round the Argy was bang up for it.
After his mate Sergio Aguero equalised from the penalty spot, Tevez played a
sublime one-two with Samir Nasri with five minutes left and the Frenchman
clipped the dramatic winner into the corner.
It marked a record-breaking 20th home Premier League win in a row for City —
and the fans in the Etihad Stadium went mad.
LOOK WHO'S BACK ... Carlos Tevez shares a joke on the Man City bench
They believe once more that they can triumph in this title race as they closed
the gap on rivals Manchester United to a single point.
City deserved victory on the balance of play but, until Tevez came on, there
was concern that their bid to overhaul United was coming to a grinding halt.
Whatever you think of the barrel-chested striker — and there are plenty of
opinions — it is undeniable that he is an extremely gifted footballer.
And when Tevez does actually make it on to the field of play, his work-rate is
rarely questioned.
Nobody expected to see Tevez in a City shirt again but now he is, he could be
the missing piece in the jigsaw.
WELCOME BACK ... Tevez had a mixed reception from fans with some supporting and some booing
Last night, his touch of guile was sorely needed with Aguero getting little change out of Cahill and David Luiz, while Italian hitman Mario Balotelli was so out of sorts he was subbed at half-time.
Mancini had come out defiantly pre-match to claim that his side would win the
title and needed a victory to support his brave boast.
To that end, ever the pragmatist, he welcomed back Tevez.
BREAKTHROUGH ... Gary Cahill's deflected effort gives Chelsea the lead
There was muted applause for the Argentina ace as he practised before kick-off
but none of the fans will be complaining if Tevez helps win them the title.
And with Nasri playing possibly his best game since his £24million summer
arrival from Arsenal, City were unlucky not to take the lead on eight
minutes.
Yaya Toure played a raking 40-yard through ball and Nasri expertly chested
down and chipped over Petr Cech. The crowd were celebrating as it headed
towards goal but there were groans when it struck the bar and bounced away.
Nasri again tried a long-range drive which was just over the bar — and when
the Blues' skipper for the night Frank Lampard gave the ball away, it seemed
Balotelli must go on and score.
But the striker was having one of those nights and, though Cech saved his
shot, it was never going in anyway.
SPECIAL CAHILL ... Chelsea goal-scorer Cahill wheels away in celebration
Mancini made no apology for hauling the sulky frontman off and replacing him with Gareth Barry arguing, quite simply, afterwards that his fellow Italian was not any good.
Chelsea had enjoyed a resurgence under caretaker-boss Roberto Di Matteo,
winning four games in a row since he took over from the axed Andre
Villas-Boas.
It was a big week for the West Londoners, with a home game against Spurs to
follow and the trip to Lisbon next Tuesday for the first leg of the
Champions League quarter-final against Benfica.
But they were digging in to keep the scores level and Nasri again caused
problems when his cross-cum-shot was tipped on to the bar by Cech. From
there, the ball was turned back in and David Silva's effort was deflected
just wide.
From the corner, Aguero's acrobatic volley flew over.
KNEESY DOES IT ... City boss Roberto Mancini on the sidelines
Di Matteo decided he needed more steel in midfield and replaced Raul Meireles with Michael Essien.
Within a minute, Chelsea were ahead against the run of play as Barry lost out
in a tangle with David Luiz and Cahill's shot was deflected past Joe Hart by
the unfortunate Yaya Toure.
That meant it was time for Tevez — and he came on in place of Nigel De Jong to
more cheers than boos.
City fans might not like what he has done but they are a forgiving bunch.
For Chelsea, Didier Drogba replaced Fernando Torres, who had battled hard up
front without reward.
POWER SERGE ... Sergio Aguero fires home from the penalty spot
The former Liverpool man retained his place after his double against Leicester
in the FA Cup broke a goal drought which had lasted longer than 24 hours of
pitch time.
However, you still had to go back to September for his last goal in the
Premier League and he was far from happy at being hooked.
It needed a consoling word from Di Matteo to stop him throwing his toys out of
the pram.
City looked shattered and without the same purpose they had shown in the first
half.
But they got a lifeline when Pablo Zabaleta crashed in a drive which would
have gone high into the stands had Essien not blocked it with a raised arm.
It happened at close range and, though Di Matteo claimed it was harsh,
credit to him for conceding it probably was a penalty.
DRAMA ... Samir Nasri celebrates his late winner
When Nasri collected he knew exactly what to do. The Frenchman played it in to the feet of Tevez, continued his run and took the return pass from which he gleefully converted.
Last term, Tevez lifted City's first silverware in 35 years as his team claimed the FA Cup.
What a twist it would be if he is parading the Premier League trophy at the Etihad on May 13.
DREAM TEAM
STAR MAN - SAMIR NASRI (Man City)
Man City: Hart 6, Zabaleta 6, Richards 7, K Toure 6, Clichy 6, Silva 5
(Dzeko 6), Y Toure 7, De Jong 6 (Tevez 7), Nasri 8, Aguero 6, Balotelli 5
(Barry 6). Subs not used: Pantilimon, Milner, Kolarov, Savic. Booked: Nasri.
Chelsea: Cech 6, Ivanovic 5 (Bosingwa 6), Luiz 7, Cahill 7, Cole 6,
Mikel 6, Meireles 5 (Essien 6), Ramires 6, Lampard 6, Mata 6, Torres 6
(Drogba 6). Subs not used: Turnbull, Malouda, Kalou, Sturridge. Booked:
Mata, Lampard.
Mar 7, 2012
Michael Wambura Afungiwa milele kuongoza soka la Bongo.
ELECTIONS COMMITTEE
TAARIFA KWA VYOMBO YA HABARI
06 MACHI 2012
UFAFANUZI KUHUSU MAJUKUMU, WAJIBU NA MAMLAKA YA KAMATI YA UCHAGUZI NA
MAELEZO YA KINA KUHUSU MAAMUZI YA KAMATI ZA UCHAGUZI ZA TFF KUHUSU MAOMBI
YA NDG. MICHAEL RICHARD WAMBURA KUGOMBEA UONGOZI KWENYE UCHAGUZI WA
TFF 2008, UCHAGUZI WA KLABU YA SIMBA 2010 NA FAM 2011.
1. USIMAMIZI WA CHAGUZI ZA WANACHAMA WA TFF
Muundo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) umeelezwa wazi kwenye Katiba ya TFF Ibara ya 18. Kamati ya Uchaguzi ya TFF ni moja kati ya vyombo sita vilivyoainishwa
katika Muundo wa TFF. Majukumu, wajibu na mamlaka ya vyombo vya TFF
yameainishwa katika Katiba ya TFF na Kanuni zilizotungwa na kuidhinishwa
na Kamati ya Utendaji ya TFF kwa kuzingatia Ibara ya 34 ya Katiba hiyo.
Majukumu,
wajibu na mamlaka ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF yameainishwa kwenye
Katiba ya TFF Ibara ya 49 na kwenye Kanuni za Uchaguzi za TFF na Kanuni
za Uchaguzi za wanachama wa TFF. Mbali na majukumu na wajibu wa
kusimamia uchaguzi wa TFF na chaguzi za wanachama wake na kuishauri
Kamati ya Utendaji ya TFF kuhusu Kanuni za Uchaguzi, Kamati ya Uchaguzi
ya TFF inao wajibu wa kulinda Katiba na Kanuni za uchaguzi za TFF na
Katiba ya FIFA na Katiba za wanachama wa TFF kama ilivyotamkwa kwenye
Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 6 na Kanuni za Uchaguzi za wanachama
wa TFF Ibara ya 26.
Uchaguzi Mkuu wa TFF hufanyika kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa TFF.
Chaguzi za wanachama wa TFF na wanachama wao hufanyika kwa mujibu wa
Kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF na si vinginevyo. Kanuni hizi
zimeainisha taratibu mbalimbali ambazo lazima zizingatiwe kikamilifu,
ikiwa ni pamoja na utaratibu wa ukataji rufaa katika ngazi mbalimbali za
uchaguzi. Vyombo na Kamati zote za TFF,
Wanachama wote wa TFF na wanachama wao, na wadau wote wa soka wanao
wajibu wa kuheshimu Kanuni mbali mbali za TFF ambazo ni pamoja na Kanuni
za Uchaguzi.
2. MAAMUZI KUHUSU MAOMBI YA UONGOZI YA NDG. MICHAEL WAMBURA
Kwa
muda mrefu pamekuwepo na taarifa mbalimbali kupitia vyombo vya habari
zenye lengo la kuwafanya wadau na wapenzi wa soka na umma wa watanzania
kwa ujumla kuaminishwa kuwa Ndg. Michael Wambura huonewa na vyombo vya
TFF vinavyosimamia uchaguzi kila anapoomba nafasi za uongozi katika TFF.
Baadhi ya vyombo vya habari na baadhi ya wapenzi wa soka wamesikika
wakisema kwamba kuenguliwa kwa Ndg. Michael Wambura kugombea uomgozi ni
kutokana na kuogopwa na viongozi wa TFF. Kamati ya Uchaguzi ya TFF
inapenda kufafanua kwa kina maamuzi yote yaliyofanyika kuhusu maombi
yote ya uongozi ya Ndg. Michael Wambura na kuweka wazi vielelezo
vilivyotumika kufikia maamuzi hayo ili umma wa watanzania wafahamu
kinagaubaga ukweli kuhusu maamuzi hayo:
UCHAGUZI MKUU WA TFF 2008
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF ilimwengua Ndg. Michael Wambura kugombea nafasi ya
Makamu wa kwanza wa Rais wa TFF kwa kutokidhi matakwa ya uadilifu kwa
mujibu wa Kanuni za Uchaguzi na Katiba ya TFF. Ndg. Michael Wambura
hakuridhika na uamuzi huo na alikata rufaa kwenye Kamati ya Rufaa ya
TFF. Hata hivyo baada ya Kamati ya Rufaa kupitia nyaraka mbali mbali
zilizowasilishwa kwenye Kamati hiyo ikiwa ni pamoja na ripoti ya ukaguzi
wa maheabu ya TFF/FAT kwa mwaka 2002, 2003 na 2004 rufaa yake
ilishindwa baada ya Kamati ya Rufaa kuridhika na kuweka bayana kuwa
mwomba rufaa, Michael Richard Wambura aliipa Zabuni kampuni yake iitwayo
Min Investments & Commercial Services Co. wakati akiwa Katibu Mkuu wa FAT/TFF na hivyo kushindwa kukudhi kigezo cha uadilifu.
Katika kufikia maamuzi yake, Kamati ya rufaa pia ilibaini kuwa Ndg.
Michael Richard Wambura alionyesha kuwa alikuwa amechana na umiliki wa
kampuni hiyo kuanzia tarehe 12 Novemba 2003 kwa mabadiliko
yaliyotekelezwa tarehe 28 Februari 2007 kwa malipo ya Shs. 34,500/= ya “exchequer receipt No. 28173444’.
Hata hivyo, Kamati ya Rufaa iliridhika kuwa utekelezaji wa mabadiliko
ya umiliki wa kampuni hiyo ulichukua takribani miezi arobaini (40).
Baada ya majadiliano ambayo yalikuwa yamekitwa (pegged) kwenye uadilifu (integrity), Kamati ya Rufaa iliridhika kuwa taswira inayojitokeza kwenye muktadha imegubikwa na wingu jeusi la mashaka kuhusu “integrity” ya Muomba Rufaa (Ndg. Michael Richard Wambura).
Uthibitisho kwamba mmilki wa Kampuni ya Min Investments & Commercial Services Co
ni Ndg. Michael Richard Wambura ulitolewa na Msajili wa Makampuni
(Business Registration and Licensing Agency-BRELA) kwa barua yenye
Kumbukumbu Na. MITM/RBN/93017 ya tarehe 16 Agosti 2006. Kampuni hiyo
ilisajiliwa tarehe 17 Julai 1992.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF inatoa sehemu ndogo tu ya ubadhirifu uliokuwa unafanywa kwa kutumia Kampuni hiyo (Min Investments & Commercial Services Co)
ya Michael Wambura kinyume na utaratibu wa utoaji tenda wa FAT/TFF na
malipo aliyojilipa bila maelezo yoyote kama ilivyoainishwa kwenye Ripoti
ya Ukaguzi wa Mahesabu iliyowasilishwa na wakaguzi tarehe 19 Septemba
2005 na Ripoti maalumu ya ukaguzi iliyowasilishwa Novemba 2006, kama
ifuatavyo:
(i) Tarehe
28 Julai 2004 Michael Wambura akiwa Katibu Mkuu wa TFF alilipwa Dola za
Kimarekani 16,548.00 (US$ 16,548 sawa na Tshs. 17,170,040 wakati huo)
kwa ununuzi wa samani (furniture) za Hosteli ya TFF. Pesa hizo
zilizoombwa kulipwa kwa Michael Wambura zimeonyeshwa kwenye fomu ya
malipo ya TFF ya tarehe 28 Julai 2004. Pesa hizo zilipokelewa na Kampuni
ya Min Investments & Commercial Services Co
na kuthibitisha kupokelewa na kampuni hiyo kwa risiti Na. 020 ya tarehe
21 Julai 2004 ya kampuni hiyo, ingawa hapakuwa na maombi ya manunuzi
(order) iliyokuwa imefanywa na TFF kwa kampuni hiyo.
(ii) Baada
ya kujilipa pesa zilizotajwa hapo juu, kesho yake tarehe 29 Julai 2004
Ndg. Michael Wambura akiwa Katibu Mkuu wa TFF alijilipa Dola za
kimarekani 25,000.00 (US$ 25,000.00 sawa na Tshs. 25,937,500 wakati
huo), kama ilivyoonyeshwa kwenye vocha ya malipo ya TFF Na. 5324 ya
tarehe tajwa hapo juu, ikionyesha kuwa ni kwa ajili ya malipo ya samani
za Hosteli (US$ 15,000.00) na malipo ya awali ya Gari (US$ 10,000.00).
Ndg. Michael Wambura alithibitisha kupokea malipo hayo. Ripoti ya
Ukaguzi inabainisha wazi kuwa vifaa vichache vilivyonuliwa kwa hosteli
ya TFF thamani yake haikuainishwa na hapakuwa na gari lililolipiwa
malipo ya awali katika vitabu vya mahesabu ya TFF.
(iii) Katika
kipindi cha mwaka 2002 Ndg. Michael Wambura akiwa Katibu Mkuu wa FAT
alijikopesha jumla ya Tshs. 36,850,750 bila idhini ya Kamati ya
Utendaji.
(iv) Tarehe 20 Mei 2002 Ndg. Michael Wambura akiwa Katibu Mkuu wa FAT alijilipa Tshs. 12,147,837 ambazo hazina maelezo yoyote.
(v) Imebainishwa
wazi kuwa FAT/TFF ilikuwa mfilisi katika kipindi cha 2002-2004 (Nukuu:
“The Association was actually insolvent during the period.”)
Kamati
inaweka wazi tena kwamba maamuzi yaliyofikiwa na Kamati ya Rufaa ya
kumuengua Michael Wambura kwenye uchaguzi Mkuu wa TFF yanaweza tu
kubadilishwa na Mahakama ya usuluhishi wa masuala ya michezo (CAS)
endapo Michael Wambura atakata rufaa CAS kupinga maamuzi hayo na
kushinda rufaa, na si vinginevyo.
MAAMUZI YA MKUTANO MKUU WA TFF 2007
Mkutano Mkuu wa TFF ambacho ndicho chombo cha juu kabisa cha TFF (Supreme Authority of TFF)
katika kikao chake mwaka 2007 kilipitia ripoti za ukaguzi wa mahesabu
ya FAT/TFF kwa kipindi cha mwaka 2002 hadi 2004 na baada ya kujiridhisha
kuhusu ubadhirifu uliofanywa na Ndg. Michael Wambura, Mkutano Muu wa
TFF uliamua kwamba Ndg.
Michael Wambura afikishwe kwenye vyombo vya dola kwa ubadhirifu wa
fedha za FAT/TFF alioufanya kama ilivyoainishwa kwenye ripoti za ukaguzi
wa Mahesabu. Sekretarieti ya TFF mwaka 2007 ikitekeleza maagizo ya
Mkutano Mkuu wa TFF na suala hilo lilpelekwa Jeshi la Polisi. Jeshi la Polisi ilithibitisha maombi ya TFF kwa barua yake ya tarehe 18 Januari 2008 na kumfungulia jalada Ndg Michael Wambura kwa kosa la wizi akiwa Mtumishi. Kamati ya Uchaguzi ya TFF inaheshimu maamuzi ya Mkutano Mkuu wa TFF na hadi sasa haijataarifiwa kwa maandishi na chombo chochote kama suala hilo limefikia ukomo wa aina yoyote.
UCHAGUZI WA KLABU YA SIMBA MWAKA 2010
Ndg.
Michael Richard Wambura aliomba kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu
ya Simba. Hata hivyo alikatiwa rufaa na Ndg. Daniel T. Kamna kwa
kutotimiza matakwa ya Ibara ya 9 ya Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa
TFF kama ilivyoamuliwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF na pia Kamati ya
Rufaa ya TFF mwaka 2008 wakati alipoomba kugombea nafasi ya Makamu wa
kwanza wa Rais wa TFF. Kamati ilikubaliana na maamuzi yaliyotolewa na
Kamati ya Uchaguzi na Kamati ya Rufaa ya TFF mwaka 2008 kwamba Bw.
Michael R. Wambura si mwadilifu kama
ilivyonyeshwa kwenye aya ya 2.1 na 2.2 hapo juu na hivyo hakukidhi
matakwa ya Ibara ya 29(7) ya Katiba ya TFF na Ibara ya 9 ya Kanuni za
Uchaguzi za wanachama wa TFF. Kamati ilimuondoa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Simba SC.
Baada
ya maamuzi hayo ya Kamati, Ndg. Michael Richard Wambura alikwenda
Mahakamani na akafungua kesi kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es salaam
dhidi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba kuzuia uchaguzi wa klabu ya Simba
usifanyike. Kwa kufanya hivyo alivunja Katiba ya Klabu ya Simba na
kukiuka Katiba ya TFF Ibara ya 12(2) (e) na Katiba ya FIFA Ibara ya
64(2). Klabu ya Simba ilichukua hatua za kikatiba, na katika kikao chake
cha 5/5/2010, ilimsimamisha uanachama Ndg. Wambura kwa kukiuka katiba
ya klabu hiyo. Klabu ya Simba iliitaarifu TFF uamuzi huo kwa barua yenye
Kumbukumbu Na. SSC/MMKT/162/Vol.40/10 ya tarehe 06 Mei 2010
iliyoambatanishwa na Muhtasari wa kikao cha Kamati ya Utendaji
kilichofanya uamuzi huo. Uamuzi wa kumrudishia uanachama unafanywa na
Mkutano Mkuu wa Klabu ya Simba. TFF haijapokea taarifa yoyote kutoka
Klabu ya Simba kwamba Mkutano Mkuu wa Klabu hiyo ulikwisha msamehe. Kwa
hali hiyo taarifa ya kusimamishwa kwake iliyotumwa TFF mwezi Mei 2010
itaendelea kuzingatiwa hadi hapo Klabu ya Simba itakapo ijulisha TFF
mabadiliko ya maamuzi hayo.
3. MAAMUZI KUHUSU UCHAGUZI WA FAM
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF ilimuondoa Ndg. Michael Wambura kugombea nafasi ya
Mwenyekiti wa FAM kwa kuwa alifungua kesi kwenye Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, Dar es salaam dhidi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba akiwa
ni mwanachama wa Klabu ya Simba kuzuia uchaguzi wa klabu ya Simba
usifanyike, jambo ambalo ni uvunjaji wa Katiba ya Klabu ya Simba,
ukiukwaji wa Katiba ya FAM, TFF na FIFA.
Pia, Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliweka wazi kama
ilivyobainisha kwenye uchaguzi wa Klabu ya Simba kwamba suala la
uadilifu wa Ndg. Wambura lilishafanyiwa maamuzi na Kamati ya Rufaa ya
TFF mwaka 2008 kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi Mkuu wa TFF. Kwa mujibu
wa Kanuni za Uchaguzi huo na Katiba ya TFF Mamlaka pekee inayoweza
kutengua uamuzi huo ni Mahakama ya Usuluhishi wa masuala ya Michezo
(CAS) iliyo na makao yake Lausanne, Switzerland.
Baada
ya uamuzi huo, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeshuhudia baadhi ya vyombo
vya TFF vikishughulikia masuala ya uchaguzi kinyume na matakwa ya Katiba
ya TFF na Kanuni za Uchaguzi, kama ifuatavyo:
(i) Katika
hali isiyozingatia Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF, Kamati ya
Nidhamu ilipokea malalamiko ya Ndg. Michael Wambura yaliyoitwa ‘rufaa’.
Kwa kuwa hakuna utaratibu wa masuala ya uchaguzi kukatiwa rufaa kwenye
Kamati za nidhamu katika ngazi zote za uchaguzi na hivyo pia kutokuwepo
ada ya ‘rufaa’ za aina hiyo, mlalamikaji alilazimisha kupokelewa ada ya
Tshs 300,000/= ambayo ni ada inayotumika kwa rufaa za Ligi Kuu ya Vodacom ambayo imeainishwa katika Ibara ya 17 ya kanuni za mashindano hayo. Ada
hiyo iliwekwa (deposited) kwenye Akaunti ya TFF bila ridhaa ya TFF.
Pamoja na mapungufu hayo “rufaa’ hiyo ilisikilizwa na Kamati ya Nidhamu
na kutolewa maamuzi. Mlalamikaji hakuridhika na maamuzi ya Kamati hiyo
na aliamua kukata ‘rufaa’ katika Kamati ya Rufaa ya TFF.
(ii) Kamati
ya Rufaa ya TFF ilipokea na kusikiliza ‘rufaa’ ya Ndg. Michael Richard
Wambura, kinyume na matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF.
Kwa kuwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF hakuna
rufaa inayokatwa kwenye Kamati hiyo, hivyo kutokuwapo ada yoyote kwa
“rufaa” ya aina hiyo, ili kutimiza azma ya kusikiliza ‘rufaa’ hiyo,
palifanyika juhudi za kulazimisha kupokelewa ‘ada’ ya Shilingi 500,000/=
ambayo ni ada ya rufaa za mashindano ya Ligi Kuu ya Vodacom ambayo
imeainishwa pia katika Ibara ya 17 ya kanuni za mashindano ya Ligi Kuu ya Vodacom. Hata hivyo, ada hiyo ambayo si halali, haikupokelwa na Sekretarieti ya TFF baada ya kushindikana kuainisha ada ya mashindano ya Ligi Kuu ya Vodacom na masuala ya Uchaguzi. Bila kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF na Katiba ya TFF Ibara ya 47(4) inayotamka na kuikataza Kamati ya Rufaa kusikiliza rufaa kwa mambo yaliyowekewa ukomo na Kanuni husika; Ibara hiyo inatamka; ‘The
Appeal Committee shall be responsible for hearing appeals against
decisions from the Disciplinary Committee that are not declared final by
relevant regulations as well as decision passed by the players’ Status
Committee concerning the eligibility of players for the teams’,
Kamati hiyo ilisikiliza malalamiko ya Ndg. Michael Richard Wambura na
kutoa uamuzi bila kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF
ambazo ni ‘relevant regulations’ na Ibara ya 12(4) ya Kanuni hizo
kutamka wazi kuwa; ‘The decisions of the TFF Elections Committee are final and conclusive and shall not be monitored by any other body’.
(iii) Kamati
ya Uchaguzi ya TFF inatamuka wazi kuwa utaratibu mzima uliotumika
kupokea rufaa hiyo toka Kamati ya Nidhamu hadi ya Kamati ya Rufaa
haukufanyika kwa mujibu wa taratibu za ukataji rufaa zilizoainishwa
kwenye Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF. Ukataji
rufaa huo uliongozwa zaidi na hila kuliko dhamira ya kuheshimu taratibu
zilizowekwa. Mbali na kutumia kanuni za Ligi kuu ya Vodacom kusikiliza
‘rufaa’ hizo, uthibitisho mwingine wa hila na ujanjaujanja ni pale
mlalamikaji alipokwenda kuweka kwenye akaunti ya TFF ada ya rufaa ya
mashindano ya Ligi Kuu ambayo haitambuliki kwa mujibu wa Kanuni za
Uchaguzi na kutumia vyombo vya habari kutangaza kitendo hicho, lakini
baada ya kutolewa maamuzi na Kamati ya Rufaa alienda kimya kimya TFF
kuchukua ada hiyo ambayo ni ya rufaa kwa mashindano ya Ligi kuu.
(iv) Kamati
ya Uchaguzi ya TFF, kwa mamlaka yaliyo kasimiwa kwake na Katiba ya TFF
Ibara ya 49(1) , Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 6, Kanuni za
Uchaguzi za wanachama wa TFF Ibara ya 8(2), 10(6), 12(4) na 26(2), na
pia kwa mamlaka yaliyoainishwa katika Katiba za wanachama wa TFF kuhusu
uchaguzi, katika kikao chake kilichofanyika 03 Desemba 2011 iliamua na
inatamka wazi kuwa maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya Rufaa ni BATILI kwa
kuwa hayakuzingatia Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF. Kamati ya
Uchaguzi ya TFF inaziagiza Kamati zote za Uchaguzi za wanachama wa TFF
na wanachama wao kuendelea kuzingatia Kanuni za Uchaguzi katika utendaji
wa kazi zao za kuendesha na kusimamia chaguzi zote za vyama vya mpira
wa miguu nchini, ikiwa ni pamoja na kutozingatia maamuzi yoyote ya
uchaguzi yatakayofanyika kinyume na Kanuni za Uchaguzi.
4. TAARIFA ZA UDANGANYIFU KUTOKA KWA BAADHI YA WAGOMBEA UONGOZI KWENYE VYAMA WANACHAMA WA TFF.
Kamati
ya Uchaguzi inapenda kuwakumbusha wadau wote wa soka wenye nia ya
kugombea uongozi TFF na vyama wanachama wa TFF kuwa kwa mujibu wa Kanuni
za Uchaguzi za TFF ibara ya 25(8) na Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa
TFF Ibara ya 26(8) ni makosa kuwasilisha taarifa za udanganyifu kwenye Kamati ya Uchaguzi. Kanuni hizo zinatamka kuwa; During
the election process any person or member who contravenes this code or
provides false particulars or qualification, may be penalized to a fine
not exceeding five hundred thousand shillings or be barred to
participate in the election process for 2 years or for both a fine and
such barring, provided that the General Secretary lodges a complaint to
the TFF judicial organ for disciplinary action.
Kamati
imebaini kuwa baadhi ya wagombea walifanya udanganyifu kuhusu vyeti
halisi walivyowasilisha kwenye uchaguzi wa FAM na pia baadhi ya waombaji
uongozi katika uchaguzi wa klabu ya Villa. Kwa mfano mwombaji aliyeomba
kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Villa cheti chake cha Elimu
ya Msingi alichowasilisha kwenye Kamati ya Uchaguzi kina utata. Vyote
hivyo viko katika hatua za uhakiki kwenye mamlaka husika, uhakiki
utakapokamilika Kamati itachukua hatua kwa mujibu wa Kanuni tajwa hapo
juu.
Kamati
imebaini na kujiridhisha kuwa Ndg. Michael Wambura alitoa taarifa
zinazokinzana kwenye Kamati ya Uchaguzi kuhusu umri wake. Katika
Uchaguzi wa Klabu ya Simba mwaka 2010, aliwasilisha taarifa kwamba
amezaliwa mwaka 1967 lakini katika uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Mara aliwasilisha taarifa kwamba alizaliwa mwaka 1965. Taarifa
za umri zinazokinzana za mwombaji uongozi zinashiria mashaka ya umakini
na uadilifu wa mgombea hasa ikizingatiwa kuwa nafasi ya uongozi ya
mwenyekiti kwa vyama wanachama wa TFF na Rais wa TFF zina ukomo wa wa umri. Kamati itachukua hatua zilizoainishwa kwenye Kanuni za Uchaguzi tajwa hapo juu.
5. KAULI ZENYE LENGO LA KUVURUGA CHAGUZI ZA WANACHAMA WA TFF.
Katika siku za karibuni Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeshuhudia kauli amabazo si za kiwanamichezo zenye lengo la kuleta vurugu katika michakato ya Uchaguzi. Kwa mfano
kauli za kuwahamasisha wadau wa soka kwenda mahakamani kwa masuala ya
michezo, hususan, kupinga michakato ya uchaguzi ni uvunjaji wa Kanuni za
Uchaguzi na Katiba ya TFF na FIFA. Kamati inawataka wadau wote wa soka
kuheshimu na kuzingatia Kanuni na taratibu za uchaguzi na Katiba ya TFF,
vinginevyo Kamati haitasita kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa Kanuni
za Uchaguzi.
Deogratias J. Lyatto
MWENYEKITI
KAMATI YA UCHAGUZI
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
chanzo na Shaffi Dauda
chanzo na Shaffi Dauda
Chuji: Nilifanya makusudi kumchapa kiatu
KIUNGO wa Yanga, Athuman Idd 'chuji' amesema hakuwa na jinsi ya kufanya zaidi ya kumchapa kiatu straika wa Zamalek, Razak Omotoyossi na kuonyeshwa kadi nyekundu. Chuji alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 63 baada ya kumkwatua Omotoyossi, kitendo ambacho Kocha Kosta Papic alikilalamikia baadaye kwa madai kuwa kiliharibu mfumo wake wa uchezaji. "Hakukuwa na jinsi nyingine zaidi ya kufanya nilivyofanya, bora nilivyofanya kuliko ningeacha tukafungwa goli la pili, yule jamaa alikuwa anakwenda kufunga goli kabisa," alisema Chuji, ambaye alicheza katikati kwenye ulinzi na Nadir Haroub `Cannavaro'. "Lakini ukiangalia aina ya mchezo, yaani hii mechi ya hapa Misri ilikuwa nyepesi kuliko ile ya Dar es Salaam, haikuwa bahati yetu tu," alisema mchezaji huyo wa zamani wa Polisi Dodoma na Simba. Yanga ilitolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wikiendi iliyopita kwa jumla ya mabao 2-1 na Zamalek ya Cairo. Katika mchezo wa kwanza ilitoka sare ya bao 1-1 jijini Dar es Salaam kabla ya kufungwa bao 1-0 katika Uwanja wa Jeshi la Misri, Jumamosi iliyopita. Viongozi wa Yanga wamekuwa wakilalamikia uchezeshaji mbovu, huku baadhi ya wachezaji wakisema mabadiliko ya kumtoa Jerry Tegete na kumuingia Chacha Marwa hayakuwa na manufaa. |
||
Samata afunika Mazembe
Mwandishi wetu
KLABU ya TP Mazembe ya DR Congo imetumia mwezi Februari kufanya utafiti kwa wachezaji wake walioitumikia klabu hiyo mwezi huo, huku Mbwana Samatta akiibuka kinara wa kupachika mabao kwa timu hiyo.
Katika utafiti huo uliofanywa na klabu ya TP Mazembe, takwimu zinaonyesha mshambuliaji Mbwana Samatta ameongoza katika kufumania nyavu, ambapo kati ya mabao 15 yaliyofungwa Samata amefunga matano.
Samata amewashinda Luka Lungu aliyefunga manne, Yannick Tusilu amefunga mawili, Treasury Mputu amefunga mawili, Guy Lusadisu amefunga moja na Eric Kanteng amefunga moja pia.
Kwa mujibu wa utafiti huo wa mwezi Februari wa TP Mazembe walitumia wachezaji 31 katika mechi tano, ambapo Samatta, Patrick Ilongo, Joel Kimwaki na Robert Kidiaba waliongoza kwa ubora baada ya kufanya vizuri katika mechi nne kati ya tano walizocheza. Wakati Treasury Mputu akifanya vyema katika mechi 3 kati ya 5, huku Thomas Ulimwengu akitumika kama mchezaji wa akiba.
Katika suala la kutoa pasi za mwisho za ushindi, mchezaji Treasury Mputu aliongoza kwa kutoa pasi sita akifuatiwa na Patrick Ochan pasi mbili, Eric Nkulukuta , Herve Ndonga, Samatta, Serge Lofo, Eric Bokanga, Thomas Ulimwengu na Treasury Salakiaku wote wamepiga pasi moja za mwisho za ushindi.
Kwa jumla, Samatta na Treasury Mputu ndiyo waliofanya vizuri katika takwimu za TP Mazembe, ambapo Samatta aliibuka katika ufungaji na Mputu katika utoaji wa pasi za mwisho za ushindi.
chanzo na aboodmsuni na soka la bongo
Yanga yaizidi Simba mapato Taifa
Yanga yaizidi Simba mapato Taifa |
Vicky Kimaro
MECHI ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba na Kiyovu ya Rwanda imeingiza kiasi cha Sh 208 milioni, kikiwa ni pungufu ya kiasi kilichopatikana kwenye mechi ya Yanga na Zamalek ya Misri, ambapo zilipatikana Sh 280 milioni. Katika mchezo huo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 na hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa mabao 3-1, kufuatia sare ya bao 1-1 katika mechi ya kwanza mjini Kigali, Rwanda wiki mbili zilizopita. Kwenye mechi ya Yanga dhidi ya Zamalek, timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1. Simba itashuka dimbani kati ya Aprili 27, 28 na 29 kwenye Uwanja wa Taifa kucheza na Entente Setif ya Algeria katika raundi ya pili ya michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika CAF. Katika taarifa iliyotolewa na wasimamizi wa mchezo huo, Prime Time Promosheni, mashabiki 34,506 waliingia uwanjani, wakati kwenye mechi ya Yanga, mashabiki 48,000 ndiyo walioingia. Katika mchanganuo wa mapato baada ya kukata makato yote Simba imepata zaidi ya shilingi milioni 100. VIP A zilichapishwa tiketi 740 na ziliuzwa tiketi 287, tiketi za bure 200 na tiketi 253 zilibaki. Kingilio cha Sh 30,000 zilipatikana Sh 8,610,000, wakati VIP B zilichapishwa tiketi 3,760 ziliuzwa 965, tiketi 92 zilikuwa tiketi za bure. Kwa upande wa VIP C, kingilio kilikuwa sh 15,000 zilichapishwa tiketi 4,077 ziliuzwa 692 (50 tiketi za bure) zilizobaki 3,335 ambapo zilipatika Sh 10,380,000, viti vya Orange zilichapishwa tiketi 10,897 ziliuzwa tiketi 2,581 (26 tiketi za bure), zilibaki tiketi 8,290 kingilio kilikuwa ni Sh8,000 na zilipatikana Sh20,648,000. Viti vya Blue kingilio kilikuwa Sh5,000, zilichapishwa tiketi 36,640 ziliuzwa 29,981 na zilibaki tiketi 6,665, zilipatika Sh 149,905,000.chanzo mwanaspoti |
Waarabu wampoteza Mganga wa Yanga
INACHEKESHA lakini inavutia kusikia, kuona na hata kusoma. Yanga na Zamalek wikiendi iliyopita zilikuwa zikipimana nguvu ndani na nje ya uwanja jijini Cairo, Misri, katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Yanga ilikuwa na mganga wake ambaye alitua Cairo kimyakimya na muda wote alikuwa bize na mambo yake kama walivyokuwa wenzake wa Zamalek. Waganga wa Zamalek inadaiwa walikuwapo uwanjani kuanzia Alhamisi usiku Yanga ilipokuwa ikipasha mazoezi. Awali waganga hao pia walikuja karibu na hoteli ya Holiday Express ilipofikia Yanga lakini wakazuiwa. Lakini cha kuchekesha zaidi mtaalamu huyo wa Yanga alifanya mambo yake kwenye Uwanja wa Jeshi wa Misri, siku moja kabla ya mechi na kuchafua hali ya hewa uwanjani huku kila mchezaji akijiuliza kunani? Viongozi wa Yanga walionekana kuzuga na kuwa mbali na mtaalamu wao muda mwingi ili kupoteza ushahidi. Lakini ujanja wote wa mganga huo ukakoma Jumamosi iliyopita ambayo ilikuwa ni siku ya mechi. Mambo yalianza wakati msafara wa timu ulipotaka kuondoka hotelini kuelekea uwanjani. Mtaalamu huo aliwatia Yanga hofu kubwa baada ya kutojulikana aliko kwani alitafutwa kila kona ili aingie kwenye gari la mbele lililobeba viongozi na waandishi wa habari. Hakuonekana wala kwenye simu hakuwa akipatikana. Hatua hiyo iliwafanya baadhi ya wazito wa Yanga kubaki hotelini kumtafuta zaidi. Baadaye ikaja kugundulika kuwa alikuwa amepitiwa na usingizi mzito chumbani kwake. Ndipo walipolazimika kubisha hodi kwenye mlango wa chumba hicho kwa muda mrefu, hadi mtaalamu huyo alipoamka. Baada ya kuamka, haraka haraka akapiga sala zake kisha wakaanza safari ya kuelekea Uwanja wa Chuo cha Jeshi la Misri, Yanga ilipokuwa ikicheza na Zamalek kwenye mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa. Mmoja wa viongozi waliokuwa kwenye msafara huo wa kumsaka, alidai kuwa mtaalamu huo alipitiwa kwa vile alikuwa hajui mechi ni saa ngapi inachezwa ingawa mwingine alikuwa akikejeli kwamba utaalamu wake umegongana na ule wa Zamalek. Lakini mganga huyo alipandishwa gari lenye kasi kubwa ambalo liliwahi kufika uwanjani na kuwakuta wachezaji kabla hawajaingia vyumbani, aliingia nao na wanajeshi wanaolinda uwanjani hapo walionekana kumhisi, lakini hawakumfanya lolote. Alikuwa mjanja na aliwazidi maarifa kila alipobaini wanataka kumzuia. Ingawa wachezaji walijua kinachoendelea na kuuchuna, lakini kocha Kosta Papic alionekana kutofurahishwa na uwepo wa mtaalamu huyo. Hata hivyo naye hakuweza kumfanya lolote kwani alikuwa hakai sehemu moja muda mwingi. Siku ya Ijumaa wakati wa usiku baada ya Yanga kutoka mazoezini, mtu mmoja raia wa Misri aliyekuwa amevalia kiutata utata, alionekana akiranda nje ya hoteli ya Yanga ambako kiongozi wa msafara wa Yanga, waliyepewa na Zamalek, akawaambia askari wasimruhusu kuingia ndani kuwabughudhi Yanga. �Mzuie huyo asije kuharibu mambo hapa,� alisikika kiongozi huyo wa msafara aliyeagizwa na Zamalek kuiongoza Yanga. Ingawa hakuna kiongozi yoyote wa Yanga aliyekuwa tayari kuzungumzia vituko hivyo, lakini baadhi ya wanachama wa Yanga waliokuwepo jijini hapa, walidai kuwa hata Zamalek walikuwa fiti kwenye mambo ya uganga ndiyo maana mganga wa Yanga akawa anapambana nao kwa nguvu huku wakidai wakati fulani walimzidi nguvu. Hata wakati Yanga inaondoka kurudi Dar es Salaam, mtaalamu huyo wa Yanga alichelewa kwa vile alikuwa akipiga dua na habari za uhakika zinadai alikuwa anatupa mabaki ya utaalam wake kwenye Uwanja wa Ndege wa Cairo juzi Jumatatu usiku. Soka la Afrika limekuwa likitawaliwa na imani za ushirikina kwa miaka mingi sasa lakini makocha hususani wa kigeni wamekuwa wakidai haisaidii kwani ni imani tu. Kocha wa Ghana, Goran Stevanovic, amekiri hivi karibuni kuwa wachezaji wake wanalogana na ndiyo maana timu hiyo iliboronga kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika. chanzo na mwanaspoti | ||||
Subscribe to:
Posts (Atom)