|
MICHEZO NI UMOJA NA MSHIKAMANO WEKEZA KATIKA MICHEZO ILI KUOKOA VIPAJI VYA VUJANA VISIISHIE KWENYE KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA UJAMBAZI NA UKABAJI
Oct 31, 2011
Yanga New Force
Oct 24, 2011
Kiiza aipasha Yanga
Sosthenes Nyoni
MSHAMBULIAJI
Hamis Kiiza aliyeingia kutokea benchi aliiongoza Yanga kuichapa JKT
Oljoro kwa bao 1-0, katika mchezo ulioshudiwa na mashabiki ni wengi
kwenye Uwanja wa Azam Chamazi.Kiiza aliyeingia kuchukua nafasi ya Jerryson Tegete katika dakika 61, alimsha shangwe za mashabiki wengi wa mabingwa hao katika dakika 86 akimalizia kazi nzuri ya Haruna Niyonzima.
Kwa ushindi huo Yanga sasa imefikisha pointi 21 na kushika nafasi ya pili sawa na Azam yenye pointi 21 lakini wama kutofautia kwa mabao.
Kocha Sam Timbe baada ya kukubwa na madai ya kutimuliwa kutokana na kukoseka kwenye benchi katika mchezo wao dhidi Toto African jana Mganda alikuwa wepo uwanjani hapo kuwaongoza mabingwa hao kupata pointi tatu muhimu.
Timbe alisema mchezo ulikuwa mgumu kwao, lakini anashukuru wamefanikiwa kupata pointi tatu muhimu kabla ya mechi yao dhidi ya Simba hapo Jumamosi.
Mshambuliaji Asamoah alikosa bao dakika 19 kwa shuti lake kugonga mwamba na kurudi uwanjani alipounganisha krosi ya Shamte Ally kutoka winga ya kulia.
Kipa wa JKT Oljoro, Said Salehe alifanya kazi nzuri dakika 27, 30, kudaka shuti la umbali wa mita 20 lililopigwa na Oscar Joshua na mpira wa kichwa wa Shamte.
Kiungo Haruna Niyonzima akiwa umbali wa mita 25 alipiga shuti kali lilipanguliwa na kipa Salehe aliyekuwa kikwazo kwa Yanga katika kipindi cha kwanza kilichotawaliwa na mabingwa hao.
Washambuliaji wa Yanga,Jerryson Tegete, Shamte na Asamoah walioneka kukosa mbinu ya kuipenya ngome ya Oljoro iliyoruhusu mabao nne tu tangu kuanza kwa ligi msimu huu.
Kocha wa Oljoro amempumzisha Ally Kani na kumwingiza Frank George ambaye dakika 52 alionyeshwa kadi ya njano na mwamuzi Abdalah Kambuzi kutoka Shinyanga kwa kumchezea vibaya Niyonzima.
Asamoah alipoteza nafasi ya kufunga dakika 55 kwa shuti lake kumgogo kipa Salehe na kutoka na kuwa kona ambayo haikuwa na madhara.
Mchezaji Sunday Musa wa Oljoro walikosa bao dakika 60, baada ya kuwatoka mabeki wa Yanga, lakini kipa Yaw Berko alikuwa makini kuwahi kucheza mpira huo.
Timbe alimpumzisha Shamte na Tegete na kuwaingiza Hamis Kiiza na Rashidi Gumbo mabadiliko hayo yalikuwa na faida kwa Yanga.
Dakika ya 86 Kiiza alifungia Yanga bao kuongoza kwa shuti kali la pembeni akimalizia pasi ya Niyonzima aliyewazidi ujanja mabeki wa Oljoro.
Akizungumzia mchezo huo kocha wa Oljoro, Ally Mohamed aliyepoteza mechi ya pili tu hadi sasa dhidi ya Simba na Yanga alisema ameridhishwa na kiwango cha wachezaji wake na kufungwa ni sehemu ya mchezo.
Wakati huo huo; Juma Mtanda anaripoti Katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Jamhuri timu ya Polisi Morogoro ilichakaza AFC ya Arusha kwa mabao 2-0.
Polisi walipata bao la kwanza dakika ya tisa kupitia Juma Maboga kwa mpira wa adhabu uliombabatiza beki wa AFC na kuingia goli, dakika 81, Nicolaus Kabipe aliunganisha vizuri krosi ya Hassan Kodou kuandika bao la pili kwa wenyeji.
chanzo na
www.mwananchi.co.tz
YANGA WAOMBA ARDHI KWA SERIKALI - KUJENGA UWANJA MPYA WA KISASA
Uongozi
wa mabingwa soka Tanzania Bara, Yanga ya jijini Dar es Salaam,
umeiandikia barua Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuomba
kiwanja ambacho wanatarajia kujenga uwanja wa kisasa hivi karibuni.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa klabu hiyo, Celestine
Mwesiga, alisema, wameiandikia barua wizara hiyo, kutaka kupewa kiwanja
cha hekari 20 katika Manispaa ya Kinondoni au Ilala, ili waweze kutimiza
ndoto yao ya kutaka kumiliki kiwanja hicho cha kisasa kama ilivyo kwa
klabu mbalimbali duniani.
“Tumeishafanya
mawasiliano na wenzetu wa Wizara ya Ardhi kuomba kupatiwa kiwanja hicho
na wameonyesha wapo tayari kutufanikishia lengo letu, hivyo tunasubiri
wakati wowote watujulishe wapi wametupata,” alisema Mwesiga.
Alisema
uongozi wake umejipanga kuhakikisha unajenga uwanja huo, ili Yanga
iweze kupunguza gharama mbalimbali zinazolipwa kupitia viwanja
wanavyochezea sasa, ili waweze kujiimarisha kiuchumi.
Akifafanua
kuhusu uwanja huo, Mwesiga alisema utakuwa na bwawa la kuogelea, uwanja
wa tenisi, mpira wa mikono, sambamba na hosteli kwa ajili ya wachezaji
wa klabu hiyo.
Hivi
karibuni, watani zao Simba walitangaza mikakati mbalimbali kujenga
vitega uchumi ikiwamo kujenga jengo la ghorofa 12 yalipo makao makuu ya
klabu hiyo mtaa wa Msimbazi sambamba na uwanja wa kisasa ‘Simba Sports
Arena, huko Bunju nje kidogo ya jiji.
chanzo na http://www.shaffihdauda.com
Ferguson rues 'worst ever day'
City, the Barclays Premier League leaders, stormed into Old Trafford
to rout their 10-man rivals 6-1 and send out an ominous warning to their
title rivals.
It was United's heaviest derby defeat since 1926, their first loss at
home in 18 months and left them trailing City by five points in the
table.
Ferguson said: "It was our worst ever day. It's the worst result in
my history, ever. Even as a player I don't think I ever lost 6-1. That's
a challenge for me too.
"I can't believe the scoreline. The first goal was a blow for sure but it was retrievable at 1-0.
"The sending off was a killer for us. We kept attacking when we went
4-1 down and we should have just said, 'We've had our day'."
City striker Mario Balotelli began the rout with a first-half opener.
He was then the man fouled as Jonny Evans earned a straight red card and added a second before Sergio Aguero slid in the third.
Darren Fletcher pulled one back but Edin Dzeko came off the bench to
score twice as City ran their hosts ragged in the closing minutes wuth
David Silva also hitting the target.
Ferguson added: "We just kept attacking. They were attacking three versus two. It was crazy football.
"I thought with the experience we've got - Rio Ferdinand, Patrice
Evra - they would (have defended more) but we just kept attacking.
Sometimes there has to be common sense about it. It was a bad day."
Oct 22, 2011
KIKAO CHA VILABU 14 KILICHOAMUA LIGI KUU KUENDESHWA NA KAMPUNI.
Baada
ya kikao cha karibia masaa 4 au zaidi viongozi wa vilabu 14
vinavyoshiriki ligi kuu ya Tanzania bara walifikia maamuzi ya kuanzishwa
kwa kampuni itayoendesha ligi kuanzia msimu ujao.
Kikao
hicho kilichofanyika katika hoteli ya JB Del-monte (zamani Paradise) @
Benjamin Mkapa Tower kilihudhuriwa na viongozi 13 kati ya 14 wa vilabu
vya ligi kuu isipokuwa Kagera Sugar waliotoa udhuru lakini wakisema
wataunga mkono maamuzi yatakayotolewa
Katika
kikao hicho maamuzi yaliyotolewa ni kwamba uanzishwe mchakato wa
kuwezesha usajili wa kampuni ambayo itaendesha ligi hiyo, huku Makamu
mwenyekiti wa Simba Godfrey Nyange Kaburu akiteuliwa kuwa mwenyekiti wa
kamati hiyo, Celestine Mwesiga katibu mkuu Yanga-Makamu mwenyekiti, Meja
Ruta wa Ruvu Shooting- akiteuliwa Katibu wa hiyo kamati, na Shani wa
Azam FC na Evadius Mtawala wa Simba wakiwa wajumbe, ambao wote kwa
pamoja watashugulikia mchakato wa kupatikana kwa usajili wa kampuni
hiyo.
“Dauda alialikwa na viongozi wa vilabu kutoa mawazo yangu juu mchakato mzima wa kuundwa kwa kampuni itayoendesha ligi kuu.”
Pia
viongozi hao wa vilabu 13 vya ligi kuu walitoa shukrani sana kwa vyombo
vya habari hususani kwa watangazaji wa vipindi vya Sports extra na
Sports Bar kutoka Clouds media group kwa kuwa watu wa kwanza kuanzisha
na kusimamia mjadala wa kuanzishwa kwa kampuni ya kuendesha ligi kuu
Tanzania bara.
chanzo na shaffih dauda wa
www.shaffihdauda.comBREAKING NEWS: HATIMAYE LIGI KUU YA TZ BARA KUENDESHWA NA KAMPUNI.
Taarifa
za kuaminika za hivi sasa zinasema kuwa mkutano wa vilabu vyote
vinavyoshiriki katika ligi kuu ya Tanzania bara vimeamua kwa pamoja
kuanzia msimu ujao ligi kuu ya Tz bara itaendeshwa na kampuni
itakayoundwa na muunganiko wa vilabu vishiriki katika premier league,
hivyo kuanzia msimu ujao T.F.F wataicha ligi hiyo kuendeshwa na kampuni.
Kwa maelezo zaidi endelea kutembelea blog yako namba ya michezo na burudani.
chanzo na shaffih dauda blogspot
Oct 20, 2011
Timu ya Bonde fc kujipinga nguvu na kawe mkwamani
Timu ya Bonde Fc inatarajia jumapili hii kujipima nguvu zidi ya kawe mkwamani mchezo utakao chezwa katika uwanja wa Luck Rangers katika shule ya msingi Mwananyamala hivyo inawakaribisha wadau wote wa soka kufika bila kukosa akiongea na chumba cha habari Bonde fc kepteini wa timu hii ya under 14 aliwahakikishia washabi waje waone soka safi kama walilionyesha siku ya jumapili dhidi ya lion ya magomeni kwani waliipiga goli 1-0
hata hivyo kocha wa timu hiyo bwana Issa Joseph (ndonga) alisema mechi hiyo ni ya kujipima nguvu kwa ajiri na vilevile wanategemea jumapili kupata wageni kutoka Bagamoyo ambao watakuja kwa ajiri ya kucheza nao mechi ya kirafiki
Timbe amtolea uvivu Kiiza
Jackson Odoyo
KATIKA kuonyesha hataki mzaha, kocha wa Yanga Sam Timbe, jana alijikuta akimfokea vikali winga wake Hamisi Kiiza baada ya kwenda kinyume na maelekezo wakati wa mazoezi ya timu hiyo.Ukali Timbe ulimpelekea kuongea kwa hasira huku akichanganya lugha kwa wakati mmoja, yaani Kiingereza, Kiswahili na Kiganda.

Winga huyo raia wa Uganda wakati wa mazoezi ya asubuhi Uwanja wa Kaunda alifanya kosa lililompelekea Timbe kupandwa na hasira.
Kosa
la Kiiza ilikuwa ni kushindwa kutafuta nafasi ili apokee pasi kutoka
kwa Jerry Tegete aliyekuwa na mpira huku akizongwa na mabeki wa timu
nyingine.
Kiiza alishindwa kutafuta nafasi ya kupokea pasi badala
yake alichukua mpira mguuni mwa Tegete ili asitoe pasi kwa mchezaji
mwingine na mwisho akapoteza mpira kirahisi.
Baada ya kosa hilo
Timbe alimuuita kwa hasira kwa lugha ya Kiswahili Kiingereza na Kiganda
na baada ya mchezaji huyo kufika mbele yake aliendelea kumfokea kwa
hasira huku akichanganya lugha hizo tatu.
chanzo na www.mwananchi.com
chanzo na www.mwananchi.com
Simba 'full' shangwe Yanga yaiva Toto leo
Calvin Kiwia na Jesca NangawMABINGWA
wa Ngao ya Jamii, Simba jana waliendelea kujiimarisha kileleni mwa Ligi
Kuu kwa kuichakaza Ruvu Shooting mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Chamazi
jijini Dar es Salaam, huku watani zao Yanga wakishuka dimbani leo
kuikabili Toto African.
Vinara hao walilazimika kusubili hadi kipindi cha pili kusherekea pointi tatu muhimu kwa vijana hao Msimbazi shukrani kwa mabao ya Emmanuel Okwi na Haruna Moshi aliyeingia akitokea benchi na kuifanya Simba kufikisha pointi 24.
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye uwanja wa Azam, Chamazi, nje kidogo ya jiji na kuhudhuriwa na watazamaji wachache kulinganisha na mechi zingine za Simba kwenye uwanja huo, ilikuwa na upinzani mkali tangu mwanzo mpaka mwisho.
Kiu ya kutaka kufunga mabao kwa Simba ilianza kwa shambulizi la dakika ya kwanza ya mchezo, baada ya washambuliaji wake Okwi, Felix Sunzu na Uhuru Seleman kugongea vizuri kabla ya jitihada zao kutibuliwa na mabeki wa Ruvu Shooting.
Ruvu Shooting inayoundwa na wachezaji chipukizi, ilijibu shambulizi hilo dakika saba baadaye, lakini kiki ya Abdallah Juma ilipaa juu ya lango, huku Jerry Santo wa Simba naye akikosa kwa staili hiyo ya kupaisha mpira juu ya mwamba dakika ya 18.
Vinara hao wa Ligi Kuu walitawala sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza, na nusura wabadilishe matokeo kama shuti la Uhuru lisingegonga mwamba na kurudi uwanjani kufuatia gonga nzuri na Sunzu.
Mabadiliko yaliyofanywa na kocha wa Simba, Moses Basena ya kumtoa Uhuru na kumuingiza kiungo Haruna Moshi 'Boban' dakika ya 46, yalizaa matunda dakika moja baadaye kufuatia kazi nzuri ya Boban kumwezesha Okwi kufunga bao la kuongoza kirahisi kutokana na mabeki wa Ruvu kujichanganya.
Washambuliaji Simba waliojenga 'netiweki' nzuri ya ushambuliaji langoni mwa Ruvu baada ya kupewa 'dawa' ya kuongeza hamu ya kufunga mabao kama alivyodai kocha Basena, waliandika bao la pili safari hii likiwekwa kimiani na Boban.
Kocha wa Basena alisema wachezaji wake walicheza vizuri na kutegeneza nafasi nyingi za kufunga ni jambo la kujivunia kwa sababu uelewana wao umetoa ushindi.
Boban aliyeonekana kucheza vizuri na Okwi alifunga bao hilo kwa shuti kali dakika ya 54 na kumwacha kipa wa Ruvu, Benjamin Haule aliruka bila mafanikio.
Kocha wa Ruvu, Boniface Mkwasa alifanya madadiliko ya kuwatoa Abdallah Juma na Raphael Keyala na nafasi zao kuchukuliwa na Seif Abdallah na Abdallah Abraham.
Mabadiliko hayo yaliwapa nguvu Ruvu baada ya kufanya mashambulizi matano langoni mwa Simba katika muda mfupi, lakini yaliishia mikononi kwa kipa Juma Kaseja au kutibuliwa na mabeki wa Simba.
Ushindi huo umeifanya Simba kuzidi kujiimarisha kileleni mwa msimamo kwa kufikisha 24, baada ya michezo 10, huku ikiendeleza rekodi yake ya kutopoteza mchezo mpaka sasa.
Mkwasa amesikitika kwa washambuliaji wake kutegeneza nafasi nyingi na kushindwa kuzitumia anajipanga kwa wakati ujao.
Wakati huo huo, ligi hiyo inaendelea tena leo kwa mabingwa watetezi Yanga kuwavaa ndugu zao wa Toto African kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu nzuri dhidi ya Toto mara ya mwisho walipokutana msimu uliopita mabingwa hao walishinda kwa mabao matatu.
Makocha wa pande zote mbili wameapa kuweka undugu pembeni na kuhaidi mchezo kusaka pointi tatu muhimu kwa kila mmoja.
Akizungumza wakati wa mazoezi ya jana asubuhi kocha mkuu wa Yanga, Sam Timbe amesema anafahamu ubora na kiwango cha wapinzani wao na kikosi chake kipo kamili kukabiliana na wapinzani wao.
"Kila mmoja wetu anataka ushindi, nategemea upinzani mkubwa kwani timu ya Toto Afrikan ni nzuri na kila tukikutana nayo kunakuwa na upinzani mkubwa, wachezaji wote wako kwa sasa wako kwenye hali,"alisema Timbe.
Naye kocha wa Toto, John Tegete amesema historia si kigezo cha wao kupoteza kwani msimu huu wamejidhatiti kikamilifu kufuta uteja.
Tegete alisema kikosi chake kiko imara kukabiliana na mabingwa hao na anategemea mchezo kuwa mgumu kutokana na kila mmoja wao kuhitaji ushindi kwa namna yoyote.
Alisema wamecheza na Yanga mara nyingi na anatambua upinzani unaokuwepo mara timu hizo zinapokutana hivyo hana wasiwasi wowote kukabiliana na kikosi hicho huku akitamba wapo kamili kuivaa Yanga.
"Sitegemei mteremko wowote licha ya timu hizi kuwa karibu na sisi tupo ugenini kwa sababu huu ni ushindani na kila mmoja anataka apate nafasi ya kuwa katika nafasi nzuri kwenye msimamo," alisema Tegete kwa akijiamini.
Yanga yenye pointi 15 ikiwa nafasi ya nne katika msimamo inashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya ushindi kiduchu dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo uliopita huku wapinzani wao Toto wakiwa na pointi10 na kukamata nafasi ya tisa.
chanzo na www.mwananchi.co.tz

Oct 19, 2011
Somalia/Ethiopia World Cup 2014 match venue switched
The
2014 World Cup first leg preliminary round match between Somalia and
Ethiopia has been moved from Nairobi to Djibouti, a Somali Football
Federation (SFF) official said on Tuesday.
The match was originally scheduled to be played at Nairobi's Nyayo National stadium on November 11 after Kenya accepted the request by the SFF to stage the game in the country due to the insecurity in Mogadishu.
The Somali national team was expected to arrive in Kenya this week for a four-week residential training ahead of the match but all the arrangements were cancelled after FIFA enforced their two-match international ban on the local national stadiums.
The suspension was however later lifted by FIFA.
"Because of the confusion, FIFA has instructed us to switch the match to Djibouti instead," SFF committee member Hassan Amir told AFP in Nairobi.
"The match will be played on November 12 to enable the hosts to play Namibia, in another qualifier a day earlier. Kenya would have been a good venue for us to play this game because we consider here our second home.
community residing in Nairobi," he added.
Oct 18, 2011
Mwasika, Nsajigwa warejea
NI habari mbaya ambazo Simba hawatapenda kuzisikia za mabeki wa pembeni
wa Yanga, Shadrack Nsajigwa na Stephano Mwasika kurejea uwanjani na
kuanza mazoezi jana Jumatatu.
Mwanaspoti iliwashuhudia mabeki hao wenye sifa ya kuzuia na kupandisha
mashambulizi wakijifua na wenzao kwenye mazoezi makali yaliyokuwa
yakisimamiwa na kocha Sam Timbe kwenye Uwanja wa Kaunda jijini Dar es
Salaam.
Daktari wa Yanga, Dk. Juma Sufiani alidokeza kuwa wakali hao, ambao pia
ni tegemeo la Taifa Stars watakuwa fiti kuivaa Simba, Oktoba 29.
Sufiani alisema mabeki hao wanahitaji mazoezi ya wiki moja tu na
watakuwa fiti kucheza mechi yoyote kuanzia Oktoba 24, mwaka huu.
Yanga na Simba zitakutana kwenye pambano la Ligi Kuu Bara Oktoba 29
jijini Dar es Salaam ikiwa ni mara ya tatu tangu mwaka huu kuanza baada
ya kuvaana kwenye Kombe la Kagame Julai 10 na katika Ngao ya Hisani,
Agosti 17, mwaka huu.
Mwasika alifanyiwa upasuaji wa goti nchini India mwezi Juni, mwaka huu, baada ya kuumia kwenye mazoezi ya Taifa Stars.
Nsajigwa, ambaye ni nahodha wa Yanga na Stars, naye aliumia nyonga
kwenye mazoezi ya Stars ilipokuwa inajiandaa na pambano la kusaka tiketi
ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Morocco.
Mwasika alirejea kwa kishindo na kutishia amani ya beki mwenzake Oscar
Joshua baada ya kufunga bao kwa shuti kali lililomshinda kipa Shaaban
Kado na kujaa kimiani kwenye mazoezi ya timu hiyo.
Katika hatua nyingine, kocha wa timu hiyo, Sam Timbe amedai hakuna
tatizo kwa Mwasika kurejea uwanjani kwani ataendelea kupanga kikosi kwa
kulingana na uwezo mchezaji aliouonyesha kwenye mazoezi.
"Siwezi kumuonea aibu mchezaji yeyote yule kumweka benchi kama
atashindwa kuonyesha bidii na kujituma kwenye mazoezi yangu,"
alisisitiza Timbe, ambaye anashikilia rekodi ya kutwaa Kombe la Kagame
na timu tatu tofauti na Yanga, Atraco ya Rwanda, SC Villa na Polisi za
Uganda.
Zitto aingia kwenye utawala wa soka la bongo
Mbunge mwenye makeke bungeni toka Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ameingia
kwenye tawala za soka la bongo baada ya kuteuliwa kuwa mmoja wawajube
wapya wa Simba sambamba na Mbunge wa Mvomero Amos Makala.
Mwenyekiti wa klabu ya Simba ambaye ni mbunge, Ismail Rage, alizitaja
kamati zilizo pitishwa katika kikao cha kamati ya utendaji
kilichofanyika Jumamosi ya Oktoba 15 ambapo kumefanyika mabadiliko
katika kamati mbalimbali.
Kamati hizo ni:
KAMATI YA FEDHA:
Mwenyekiti: Geofrey Nyange 'Kaburu'
Makamu mwenyekiti: Adam Mgoyi
Wajumbe: Said Pamba, Juma Pinto na Zitto Kabwe.
KAMATI YA MASHINDANO:
Mwenyekiti: Joseph Itang'are
Makamu Mwenyekiti: Azim Dewji
Wajumbe: Jarry Ambe, Swedy Nkwabi, Hassan Hasanoo, Mohamed Nassor, Richard Ndasa na Suleiman Zakazaka.
KAMATI YA UFUNDI:
Mwenyekiti:Ibrahim Masoud,
Makamu Mwenyekiti: Evance Aveva
Wajumbe: Danny Manembe, Khalid Abeid, Musley Luwey, Mulamu Nghambi, Said Tuli, Rodney Chiduo, Patrick Rweyemamu.
KAMATI YA USAJILI:
Mwenyekiti: Zakaria Hans Poppe,
Makamu mwenyekiti: Kassim Dewji
Wajumbe: Francis Waya, Crecensies Magori, Salim Abdallah, Collins Fransch na Gerald Lukomay.
KAMATI YA NIDHAMU:
Peter Swai, Jamal Rwambo, Charles Kenyela, Evody Mmada na Chaurembo.
Rage alisema kamati hizo zimeanza kazi zake mara moja kwa kuwa kila mjumbe tayari ameshakabidhiwa barua yake.
Katika hatua nyingine Rage alisema kuwa kundi la marafiki wa Simba
(friends of Simba) ambalo linafanyakazi pega kwa pega na Simba SC
wamemaliza tofauti zao.
chanzo na aboodmsuni.blogspot.com
Oct 10, 2011
MTIBWA WAPIGISHWA KWATA NA JKT RUVU
JKT Ruvu imeichapa Mtibwa Sugar mabao 3-2 katika mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania iliyochezwa kwenye uwanja wa Azam, Chamazi jijini Dar es Salaam.Kwa ushindi huo klabu ya JKT Ruvu imefikisha pointi 15 kama ilizonazo klabu za Mtibwa Sugar na Azam.
Mtibwa ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya tisa lililofungwa na Vicent Barnabas aliyeunganisha krosi ya Issa Rashid.JKT Ruvu walisawazisha bao hilo katika dakika yabaada ya Mtibwa kujifunga wenyewe wakizembea kuondoa mpira wa kona.
JKT Ruvu pia waliongeza bao la pili kupitia kwa Rajab Chau aliyepokea mpira wa faulo ndogo uliopigwa na Emmanuel Linjechele.Timu hizo mpaka zinaenda mapumziko JKT Ruvu ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-1, lakini katika kipindi cha kwanza timu zote zilicheza kwa kushambuliana.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ya wachezaji, lakini mabadilko hayo yalionekana kuwasaidia zaidi JKT Ruvu kwa sababu walipata penati katika dakika ya 85 ambayo ilifungwa na Stanley Nkomola na kuandika bao la tatu.
Penati hiyo ilipatikana baada ya Hussein Bunu kudondoshwa na Salvatory Ntebe katika eneo la hatari na mwamuzi Amon Paul wa Mara aliamuru ipigwe penati.Slavatory Ntebe aliipatia Mtibwa bao la pili katika dakika ya 89 baada ya kupiga shuti kali lililomshinda kipa wa JKT, Hamis Seif.
Ligi Kuu itaendelea tena Oktoba 14 kwa Yanga kucheza na Kagera Sugar, halafu Oktoba 15 JKT Ruvu itacheza na Azam, pia Oktoba 16 Simba itacheza na African Lyon.
chanzo na shaffidauda.blogspot.com
MATCH REPORT: MOROCCO 3-1 TANZANIA
Wenyeji Morocco ndiyo
walioanza kupata bao dakika ya 19 mfungaji akiwa Marouane Chamakh kwa
mpira wa kichwa ambao ulidunda kabla ya kumpita kipa Juma Kaseja wa
Taifa Stars. Abdi Kassim aliisawazishia Stars dakika ya 40 kwa shuti la
nguvu- umbali wa meta 35 lililomshinda kipa Nadir Lamyaghri kufuatia
pasi ya Idrisa Rajab.
Mabao mengine ya Morocco ambayo imepata tiketi ya kucheza fainali za AFCON zitakazochezwa mwakani katika nchi za Equatorial Guinea na Gabon yalifungwa dakika ya 68 na Adel Taarabt. Mbark alifuta matumaini ya Stars kupata sare katika mechi hiyo kwa bao lake la tatu alilifunga dakika ya 90 kwa shuti la chini akiwa ndani ya eneo la hatari.
Mwamuzi Bakary Gassema kutoka Gambia aliwaonya kwa kadi za njano Idrisa Rajab, Juma Nyoso, Dan Mrwanda na Mohamed Rajab wa Stars wakati kwa upande wa Morocoo aliyeoneshwa kadi ya njano alikuwa nahodha wa timu hiyo Houcine Kharja.
Akizungumza baada ya pambano hilo, Kocha wa Taifa Stars, Jan Poulsen aliwataka wachezaji wake wasikate tamaa kutokana na matokeo hayo kwa vile walicheza na timu bora kuliko wao. Alisema hivi sasa wanatakiwa kuelekeza akili kwenye mechi mbili zilizo mbele yao dhidi ya Chad. Mechi hizo za mchujo kwa ajili ya kuingia hatua ya makundi ya mchujo Kanda ya Afrika kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Brazil mwaka 2014 zitachezwa Novemba 11 mwaka huu jijini Ndjamena na Novemba 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Stars; Juma Kaseja, Erasto Nyoni/Nassoro Cholo, Idrisa Rajab, Juma Nyoso, Aggrey Morris, Shabani Nditi, Dan Mrwanda, Henry Joseph, Mbwana Samata/John Bocco, Abdi Kassim na Mohamed Rajab/Mrisho Ngasa.
Morocco; Nadir Lamyaghri, Michael Basser, Abdelhamid El Kaoutari, Badri El Kaddouri, Mehdi Benatia, Younes Belhanda, Houcine Kharja, Mbark Boussoufa, Adel Taarabt/Youssef El Arabi, Marouane Chamakh/Said Fettah na Oussama Assaidi/Karim Al Ahmadi.
Taifa Stars inatarajiwa kurejea Dar es Salaam saa 2.30 asubuhi Oktoba 11 mwaka huu kwa ndege ya Qatar Airways.
chanzo na http://www.shaffihdauda.com/

Oct 5, 2011
Timu ya Bonde fc inaendelea na mazoezi kwa ajiri ya mechi zake
Timu ya bonde fc ya mwananyamala inaendelea na mazoezi magumu ili kujiwinda na mechi zinazowakabiri akiongea na mwandishi wa habari hii kiungo mkabaji wa timu hiyo ya under 14 Hassani Rashid Banda alisema kuwa mazoezi wanayopewa na makocha wao ni magumu na ya kufa mtu . Ila amewatoa wasi wasi mashabiki wao kuwa yeye na wenzeke watandeleza mapambano mazito katika mechi ijayo ya jumamosi dhidi ya mikocheni kids itakayochezwa katika uwanja wa mikocheni shule ya msingi na pia aliwasihii mashabiki wa soka kokote pale jijini kujitokeza kwa wingi kuja kujionea vipaji vya kweli na pasi za kweli na si butua butua kama baadhi ya timu za ligi kuu
Subscribe to:
Posts (Atom)