MICHEZO NI UMOJA NA MSHIKAMANO WEKEZA KATIKA MICHEZO ILI KUOKOA VIPAJI VYA VUJANA VISIISHIE KWENYE KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA UJAMBAZI NA UKABAJI
Sep 29, 2011
ABOODMSUNI NA SOKA LA BONGO: YANGA NA MWENDELEZO WA PROJECT ZAO
ABOODMSUNI NA SOKA LA BONGO: YANGA NA MWENDELEZO WA PROJECT ZAO: Baada ya Azam FC kuanza kuutumia uwanja wake wa Azam uliopo maeneo ya Chamanzi umeamsha project iliyokuwa imesimama pale Jangwani. Katika ...
ABOODMSUNI NA SOKA LA BONGO: ASAMOAH AFUNGUKA, YANGA WAWASAMBARATISHA WAGOSI
ABOODMSUNI NA SOKA LA BONGO: ASAMOAH AFUNGUKA, YANGA WAWASAMBARATISHA WAGOSI: Mshambuliaji wakimataifa toka Ghana anaekipiga kwa mabingwa wa Tanzania Bara Yanga, Kenneth Asamoah leo kafunguka kwenye michuano ya ligi ku...
ABOODMSUNI NA SOKA LA BONGO: CECAFA wazialika Nigeria, Cameroon nchini Tanzania...
ABOODMSUNI NA SOKA LA BONGO: CECAFA wazialika Nigeria, Cameroon nchini Tanzania...: TIMU za soka za Cameroon na Nigeria zinatarajiwa kushiriki michuano ya Kombe la Chalenji inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya soka Afrika Ma...
ABOODMSUNI NA SOKA LA BONGO: Sunzu fiti, Machaku aondolewa POP
ABOODMSUNI NA SOKA LA BONGO: Sunzu fiti, Machaku aondolewa POP: SIMBA imepata matumaini ya kuendelea kufanya vema katika Ligi Kuu soka Tanzania Bara, baada ya nyota wake waliokuwa majeruhi akiwemo kiungo ...
Sep 28, 2011
KIKOSI CHA TAIFA STARS KWA AJILI YA MECHI YA MOROCCO
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen leo (Septemba 27 mwaka huu) ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mechi ya mwisho ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani dhidi ya Morocco.
Kikosi hicho kitaingia kambini Septemba 29 mwaka huu jijini Dar es Salaam, na kinatarajiwa kuondoka nchini Oktoba 6 mwaka huu kwenda Casablanca, Morocco kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Oktoba 9 mwaka huu kwenye mji wa Marrakech.
Wachezaji walioitwa ni makipa Shabani Dihile (JKT Ruvu Stars), Juma Kaseja (Simba) na Shabani Kado (Yanga).
Mabeki wa pembeni ni nahodha Shadrack Nsajigwa (Yanga), Erasto Nyoni (Azam), Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya) na Amir Maftah (Simba).
Mabeki wa kati ni Aggrey Morris (Azam), Juma Nyoso (Simba) na Victor Costa (Simba).
Viungo wakabaji ni Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Nurdin Bakari (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar) na Jabir Aziz (Azam).
Viungo washambuliaji ni Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada), Mrisho Ngassa (Azam) na Ramadhan Chombo (Azam).
Washambuliaji ni Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Dan Mrwanda (DT Long An, Vietnam), Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden), John Bocco (Azam) na Hussein Javu (Mtibwa Sugar).
chanzo na Shaffih Dauda wa
www.shaffih.blogspot.com
Sep 26, 2011
Bonde fc yaichapa Magomeni kids
Vijana wa Bonde fc wakipasha kabla ya mechi kuanza. vijana hawa wa Bonde fc waliibuka na ushindi mnono wa gili 2-0 dhidi ya Magomeni kids mechi ilichezwa katika uwanja wa magomeni barafu hapo jana tarehe 25/09/2011
Sep 24, 2011
Timu ya Bonde fc inaendelea na mazoezi kama kawida
VIJANA WAKIMSIKILIZA MWALIMU WAO CHIDI BANDA HAPA
MAKIPA NAO WAKIENDELEA NA MAZOEZI YAO
VIJANA WAKIPASHA
Sep 20, 2011
Kama ulidhani unaujua utani, basi sikia hii
Mashabiki hao wamefanya hivyo kupitia kura ya maoni iliyokuwa ikiendeshwa na mtandao maarufu wa habari za michezo duniani wa TalkSports, ambao katika ukurasa wao wa Facebook, waliendesha kura hiyo kwa kuuliza “Fergie amemfananisha Wayne Rooney na Pele, lakini unadhani ni nani mchezaji bora kabisa wa Manchester United?”
Kwenye kura hiyo, mtandao huo uliainisha majina ya wachezaji kadhaa wakiwemo Bobby Chalton, Ryan Giggs, Eric Cantona, Eric Djemba Djemba, Duncan Edwards, Wayne Rooney, Cristiano Ronaldo, Paul Scholes na wengineo wengi ambapo katika hali ya kustaajabisha wapiga kura walimtaja Howad Webb kama mchezaji bora kwa zaidi ya asilimia 48, akiwaacha mbali kweli magwiji wa ukweli.
Webb alipata asilimia 48, akifuatiwa katika nafasi ya pili na Bobby Chalton (20%), Ryan Giggs akishika nafasi ya tatu.
Kazi kweli kweli…
Giggs aweka rekodi United wakianza kwa sare
Ryan Giggs, alikuwa na usiku
wa aina yake baada ya kufanikiwa kujiwekea historia ya kuwa mchezaji
mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kufunga katika michuano ya klabu bingwa
Ulaya na kuisaidia klabu yake ya Manchester United kufanikiwa kupata
sare ya bao 1-1 dhidi ya Benfica ya Ureno.
Katika pambano hilo ambalo lilikuwa wazi
kwa timu zote huku yeyote kati ya timu hizo mbili akionekana angeweza
kuibuka na ushindi ndani ya dakika tisini za mchezo, wenyeji
walitangulia kufunga kupitia kwa Oscar Cardozo kunako dakika ya 24 ya
mchezo.
Alifunga bao hilo baada ya kutumia
makosa ya mabeki wa United, ambapo aliachia shuti kali la umbali wa
takriban mita 18 hivi lililomshinda mlinda mlango wa United na baada ya
hapo wenyeji wakaonekana kama wangeongeza bao wakati wowote.
Hata hivyo, dakika chache kabla ya
mapumziko, Ryan Giggs alipokea pasi safi toka wingi ya kulia mwa uwanja
kabla ya kukokota mpira huku akiwadhibiti mabeki kadhaa wa Benfica na
kisha kuachia mkwaju safi na kuandika bao la kusawazisha, na matokeo
hayo yakasimama hivyo hadi wakati wa mapumziko.
Kipindi cha pili kilishuhudia timu zote
zikifanya mabadiliko kadhaa sanjari na kucheza kandanda safi lakini
zaidi ya kosakosa kadhaa kwa kila upande, hakuna timu iliyoweza kuliona
lango la mwenzie na hivyo hadi mwisho wa mchezo Benfica 1-1 United.
Bao la Giggs linamfanya aweke rekodi ya
kuwa mchezaji mkongwe zaidi kufunga katika michuano hiyo akiwa na umri
wa miaka 37 na siku 289, ambapo pia anampita mkongwe Raul Gonzalez kwa
kuwa mchezaji aliyefunga katika misimu mingi zaidi ya michuano hiyo,
akiwa amefikisha misimu 16 hivi sasa.
Wakati United wakiambulia sare ya
ugenini, jirani zao Manchester City nao walijikuta wakiambulia sare ya
nyumbani dhidi ya Napoli kwenye mechi ambayo wageni Napoli walitangulia
kufunga kupitia kwa Edinson Cavani lakini wenyeji wakajitutumua na
kusawazisha kupitia kwa Aleksander Kolarov dakika chache baadae.
Kule nchini Uholanzi, Ajax walibanwa
vilivyo na waliokuwa wageni wao Lyon ya kutokea nchini Ufaransa na
kuambulia sare ya bila kufungana lakini miamba ya Hispania Real Madrid
wakianza michuano hiyo vyema baada ya kuchomoza na ushindi wa bao 1-0 wa
ugenini kwenye uwanja wa Dinamo Zagreb, bao pekee la mchezo huo
likiwekwa kimiani na Angel Di Maria.
Mechi zingine za usiku huu zimeshuhudia
FC Basle wakiibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya SC Otelul Galati, huku
Inter Milan wakianza vibaya baada ya kukubali kichapo cha nyumbani cha
bao 1-0 toka kwa Trabzonspor.
Nao wafaransa Lille wakiwa nyumbani
wakaambulia sare ya bao 2-2 dhidi ya CSKA Moscow Ilhali Villarreal
wakiwaruhusu wageni wao Bayern Munich kuwaadhiri nyumbani kwa kichapo
cha bao 2-0
Maftah- Yanga walitaka kuua kipaji changu
Maftah- Yanga walitaka kuua kipaji changu
BEKI wa kushoto wa timu ya taifa, Taifa
Stars na Klabu ya Simba, Amir Maftah ameamua kuweka wazi kile
kilichomtokea wakati akiwachezea watoto wa Jangwani, Yanga Afrika.
Katika mahojiano maalumu na safu hii, Maftah anasema kwamba ana
mshukuru Mungu kwa sasa yupo kwenye timu ambayo ina viongozi wanaotambua
mchango wake na wasio na mizengwe kama ilivyokuwa kwa upande wa Yanga.Anasema; “Kwa hakika kabisa naamini hivi sasa nisingekuwepo tena kwenye ulimwengu wa soka, kwani pale Yanga nilifanyiwa mambo ya ajabu mno yaliyokuwa yanatishia majaliwa yangu ya baadaye.”
Anasema licha ya kuichezea Yanga kwa moyo wake wote na mapenzi makubwa aliyokuwa nayo, lakini alishangaa kujikuta akihusishwa na kuihujumu timu hiyo.
“Kiukweli, mimi nilikuwa naipenda Yanga tangu nikiwa mdogo kabisa, malengo yangu yalikuwa ni kuhakikisha siku moja nakuja kuichezea.
“Mapenzi na Yanga yalikuwa ni ya kutoka moyoni kabisa, lakini niliyoyakuta, na mizengwe niliyofanyiwa, kwa hakika kabisa naweza kusema hakuna klabu ninayoichukia kama Yanga.
“Hata ninapocheza dhidi ya Yanga huwa nafurahi mno kuhakikisha tumewanyanyasa tunavyotaka na kuwafunga, kwani siipendi kabisa Yanga.
“Na katika kila mchezo nitahakikisha nacheza kufa au kupona kuhakikisha tu furaha nyangu ya kulipiza kisasi cha waliyonifanyia inatimia.”
Anasema wakati akiwa katika Klabu ya Mtibwa ya Manungu Turiani mkoani Morogoro, Simba walimfuata mara kadhaa kwa ajili ya kutaka kumsajili, lakini yeye akaikataa ofa hiyo.
“Niliikataa Simba kwa sababu tu nilikuwa na mapenzi makubwa na Yanga, hivyo sikutaka kuwachezea watoto hao wa Msimbazi, kwani akili yangu ilikuwa kwa watoto wa Jangwani.
“Na hata Yanga waliponifuata kwa ajili ya kutaka kunisajili sikuwa na kipingamizi, kwa sababu tayari walikuwa moyoni mwangu, hivyo nikatua kwao.” Maftah anasema licha ya kucheza kwa kujituma wakati akiwa na Yanga, lakini alishangaa kuona mizengwe ya hapa na pale kutoka kwa viongozi wa timu hiyo.
Anasema awali alichukulia ni mambo ya kawaida, lakini siku jinsi zilivyokuwa zinakwenda, akajiridhisha kwamba viongozi hao hawakuwa na nia nzuri na yeye.
“Ilifikia kipindi eti nikawa nashutumiwa kwamba mimi naihujumu Yanga kwa sababu ni mpenzi wa Simba, kitu ambacho kwangu kilikuwa kigeni kabisa kukisikia, lakini niliamua kuvumilia.
“Hata hivyo, kuna siku nitamuweka hadharani kiongozi mmoja wa Yanga ambaye alisababisha matatizo yote haya kiasi kwamba hadi mimi kuonekana msaliti.” Maftah anasema baada ya kuachwa na Yanga katika mazingira ya kutatanisha, alikuwa na wakati mgumu mno kwenye mustakabali wa maisha yake ya soka.
“Mimi ajira yangu ni soka. Soka ndiyo ninayoitegemea kuendesha maisha yangu ya kila siku pamoja na familia yangu, hivyo kuacha soka maana yake ni kwamba nakosa ajira. “Nilisota, huku nikijaribu kuangalia muelekeo utakuwaje, lakini namshukuru Mungu kwamba Simba wakaniona na wakanisajili kwa mkataba mnono.”
Anasema baada ya kutua Simba aliona mambo mengi ni tofauti, kwani viongozi wake walikuwa wanaonyesha kumjali kila mchezaji na hakuna mizengwe yoyote inamkera.
“Kwa uhakika kabisa naweza kusema hapa Simba nimefika, kwani viongozi wake wanawajali wachezaji na hata kiwango changu kimezidi kuimarika kwa sababu akili yangu yote ipo kwa ajili ya kuhakikisha inafanya vizuri katika kila mchezo.
“Simba wananilipa dola 600 kwa mwezi (sawa na zaidi ya shilingi 900,000) ambazo kwangu zinanitosha kabisa, hasa ukizingatia kwamba tunapata posho katika kila mechi, hivyo sina tatizo.”
Katika kuonesha shukrani zake, Maftah anasema kwamba amekuwa anajifua mno kivyake kuhakikisha kwamba anaendelea kuwa fiti ili kuweza kucheza katika kiwango cha juu kabisa.
Anasema hatarajii kuichezea timu nyingine kwa hapa Tanzania, kwani iwapo ataondoka Simba ndiyo utakuwa mwisho wake kama hatakuwa amepata timu nje ya nchi.
“Kwa kweli kwa upande wangu nikitoka hapa Simba, sina mpango wa kucheza katika timu yoyote ya hapa Tanzania, kwani kama sitapata timu ya nje ya nchi basi huo utakuwa ni mwisho wangu wa kucheza soka.”
Maisha kwenye Filamu Aidha Maftah anasema kwamba yupo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha filamu yake inayozungumzia ukweli halisi wa soka la Tanzania (A True Story of Tanzanian Football).
Anasema kwenye filamu hiyo ataonesha matukio yote halisi ya mwenendo wa mchezo huo nchini pamoja na mwendendo wa klabu zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.
“Humo kutakuwa na kila kitu kinachohusu maisha ya soka la Tanzania pamoja na historia yangu nilikozaliwa na nilikoanza kucheza soka.
“Pia nitazungumzia kwa kina yale yote yaliyonitokea katika maisha yangu ya soka kwa uhalisia wote.”
Anasema katika filamu hiyo atamshirikisha gwiji wa soka la zamani hapa nchini Zamoyoni Mogella pamoja na wasanii wengine ambao hakuwa tayari kuwataja kwa sababu bado hajakamilisha nao mazungumzo.
“Kutakuwa na watu wengi kwenye filamu hii ambayo inatengenezwa na kampuni ya Asaa chini ya Meneja wangu, Imam Maunda.”
Sep 17, 2011
Yanga yaona mwezi
Yanga yaona mwezi
Jesca Nangawe
MABINGWA watetezi, Yanga jana walipata ushindi wao wa kwanza kwenye Ligi Kuu baada ya kuichapa African Lyon kwa mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Azam, Chamazi jijini Dar es Salaam.
Mashabiki wa Yanga waliokuwa na hamu ya kuona timu yao ikishinda
mchezo huo walisubiri kwa dakika 35, mpaka mshambuliaji wa kimataifa wa
zamani wa Zambia, Davies Mwape alipofunga bao la kuongoza, lakini Lyon
walisawazisha bao hilo kupitia kwa Hamis Shengo kabla ya Rashid Gumbo wa
Yanga aliyeingia akitokea benchi kufunga bao la ushindi katika dakika
ya 63.MABINGWA watetezi, Yanga jana walipata ushindi wao wa kwanza kwenye Ligi Kuu baada ya kuichapa African Lyon kwa mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Azam, Chamazi jijini Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo Yanga imejinasua mkiani kwa kufikisha pointi sita katika michezo mitano na kurudisha faraja kwa mashabiki wao kabla ya mechi ya Jumapili dhidi ya Azam itakayofanyika kwenye Uwanja wa Taifa.
Pamoja na rekodi mbaya ya utovu wa nidhamu kwa timu za Ligi Kuu msimu huu jana mwamuzi Mathew Akrama wa Mwanza alichezesha mechi bila ya kuonyesha kadi kwa mchezaji yeyote.
Mchezo ulianza kwa kasi na katika dakika ya 4, Sino Agustino alifanikiwa kuunganisha vizuri krosi ya Seleman Kassim, lakini shuti lake liligonga mwamba na kurudi uwanjani.
Yanga ilijibu mapigo katika dakika ya 10 na 14 kupitia kwa Mwape aliyeshindwa kumalizia nafasi mbili baada ya kupigiwa pasi nzuri na Nurdin Bakari na Shamte.
Bao la kwanza la Yanga lilipatikana baada ya Pius Kisambale kupiga pasi ndefu kutoka katikati ya uwanja ambayo ilitua kwa Shamte Ally aliyemtengenezea nafasi Mwape ambaye aliusukuma mpira wavuni katika dakika ya 35 na kuamsha shangwe kwa wanajangwani.
Dakika tano baadaye, Kassim wa Lyon aliwatoka mabeki wa Yanga na kipa Berko na kupiga shuti golini, lakini Juma Seif alifanya kazi ya ziada kuwahi mpira huo na kuutoa nje.Ikiwa inaonekana timu hizo zitaenda mapumziko huku Yanga ikiongoza kwa bao moja, Hamis Shengo aliisawazishia Lyon kwa mpira wa adhabu alioupiga na kwenda moja kwa moja wavuni na kumwacha Berko asijue la kufanya.
Kabla ya kufungwa bao hilo katika dakika ya 42, beki wa Yanga, Bakari Mbegu alimchezea vibaya kiungo Kassim nje kidogo ya eneo la 18, faulo ambayo ilitoa nafasi kwa vijana wa Lyon kupata sare 1-1 hadi mapumziko.Kipindi cha pili Yanga ilianza kwa kasi na katika dakika ya 47, Pius Kisambale alikosa bao kwa shuti lake kupanguliwa na kipa Juma Abdul na kutoka nje.
Kocha Sam Timbe aliwapumzisha Shamte, Kigi Makasi na Juma Seif na kuwaingiza Kenneth Asamoah, Rashid Gumbo na Godfrey Bonny mabadiliko ambayo yaliisaidia Yanga.
Mabadiliko hayo yaliisaidia Yanga kwa sababu Gumbo aliyechukua nafasi ya Kigi aliipatia Yanga bao la pili katika dakika ya 63 kwa shuti la umbali wa mita 32, lililomshinda kipa wa Lyon, Abdul.Washambuliaji wa Lyon, Adam Kingwande na Agustino Sino watajilaumu wenyewe kwa kupoteza nafasi nyingi za kufunga katika mechi hiyo.
Katika mechi hiyo pia Gumbo alipiga shuti kali ambalo liligonga mwamba katika dakika ya 71 na kutoka vile vile Kenneth Asamoah alishindwa kumalizia pasi Kisambale akiwa ndani ya 18. Katika mechi hiyo kocha wa Lyon alifanya mabadiliko mapema, ambapo katika dakika ya 16 alimtoa Benedictor Jacob na kumwingiza Sammy Kessy pia baadaye alimtoa Kessy na kumwigiza Jacob Masawe.
Licha ya kuwapo ulinzi mkali kwenye uwanja wa Azam, wapo baadhi ya mashabiki waliruka ukuta ambao sio mrefu sana na kuingia uwanjani.Yanga: Yaw Berko, Shadrack Nsajigwa, Abuu Zuberi, Bakari Mbegu, Chacha Marwa, Juma Seif, Shamte Ally, Nurdin Bakari, Davis Mwape, Pius Kisambale na Kigi Makasi.
African Lyon: Juma Abdul, Aziz Sibo, Hamis Shengo, Shaban Aboma, Hamis Yusuph, Razaki Khalfan, Adam Kingwande, Seleman Kassim, Benedictor Jacob, Hood Mayanja na Agustino Sino.
MSIMAMO WA LIGI KUU BONGO
msimamo wa ligi kuu ndo huo:
nfs timu chz shd sul ptz fga fgw tmg pts
1. simba sc 5 4 1 0 5 0 4 13
2. jkt ruvu 5 2 3 0 8 4 4 9
3. azam fc 5 2 2 1 4 2 2 8
4. moro utd 5 2 2 1 7 6 1 8
5. mtibwa 5 2 2 1 4 3 1 8
6. toto 5 2 1 2 7 5 2 7
7. madume 5 1 3 1 4 4 0 6
8. jkt oljoro 5 1 3 1 3 4 1 6
9. a. lyon 5 1 2 2 3 4 1 5 k. sugar 5
0 4 1 6 7 1 4 10. R.shooting 5 0 4 1 3 4 -1 4
12. c. union 5 1 1 3 3 7 -4 4
13. v. squad 5 1 1 3 3 8 -5 4
14. p. dodoma 5 0 3 2 3 5 -2 3
mechi za leo ni:
ruvu shooting v coastal union
toto african v jkt ruvu
villa squad v mtibwa sugar
Sep 15, 2011
siku Bonde fc ilipochukua ubingwa wa Kidiyosa 2011/12
Baadhi ya wachezaji na mashabiki wa Bonde Fc siku ilipochukua Ubingwa wa kidiyosa Eid fitri Cup 2011/12
Sep 13, 2011
siku under 14 ilipokwenda jipima nguvu na leaders kids
Hapa kabla ya kuhailishwa kwa mechi kati ya bonde kids dhidi ya leaders kids hapo jumamosi mechi hii iliahilishwa kwa sababu ya mama Salma kikwete kuwa na mkutano na akinamama ndani ya viwanja vya leaders
Sep 7, 2011
baada ya kuchukua ubingwa wa eid el fitri sasa timu inaendelea jifua
Timu ya bonde fc inaendelea na mazoezi yake kama kawaida katika uwanja wake wa nyumbani ili kujiwinda na michuanoi ya ligi ya tanzania betting inayoendelea katika viwanja vya garden kinondoni
Sep 3, 2011
Arsenal yawa klabu ya mfano Ulaya
Raisi huyo wa Shirikisho la Vyama vya
soka barani Ulaya (UEFA), akiongea kwenye mkutano uliofanyika mjini
Zurich jana, alisema kuwa, mpango wa kuvidhibiti vilabu ambavyo vimekuwa
vikifanya matumizi makubwa ambayo ni nje ya uwezo wake wa uzalishaji,
uko palepale na kwamba utaanza kutumika kwenye msimu wa mwaka 2012/13,
kama ambavyo imeshakubaliwa.
Chini ya mpango huo, vilabu
havitaruhusiwa kufanya manunuzi ya wachezaji au kulipa mishahara mikubwa
kwa wachezaji wao zaidi ya kile klabu inachoingiza kama mapato yake
kutokana na mikataba mbalimbali ya kibiashara na vyanzo vyao vya mapato
na kwamba vilabu ambavyo vitashindwa kutimiza sharti hilo, vitafungiwa
kushiriki michuano yoyote ya Ulaya katika ngazi ya vilabu.
Akizungumza katika mkutano huo, Platini,
gwiji wa zamani katika kikosi cha Ufaransa na vilabu mbalimbali
alitolea mfano wa klabu ya soka ya Arsenal, ambayo alisema kuwa miaka
kumi iliyopita, mzunguko wake wa fedha kwa mwaka ulikuwa chini sana
kiasi cha kupitwa na vilabu kama Chelsea, Liverpool na Newcastle, lakini
kutokana na mipango mizuri na matumizi sahihi ya fedha, leo hii klabu
hiyo imekuwa juu ya vilabu hivyo kwa karibu mara mbili kiuchumi.
Mkali wa Arsenal aanza na hat-trick
Mshambuliaji mpya wa Arsenal Chu-Young
Park, amesherehekea kutimia kwa ndoto yake ya kuwachezea washika bunduki
hao wa London, kwa kuiongoza nchi yake ya Korea Kusini kuibuka na
ushindi wa bao 6-0 dhidi ya Lebanon, katika michuano ya kuwania kufuzu
fainali zijazo za kombe la dunia.
Park, ambaye alitua Arsenal hivi
karibuni akitokea Monaco ya Ufaransa, aliwaonyesha mashabiki wa Arsenal
kuwa huenda akawa tiba ya timu yao kushindwa kupata mabao katika baadhi
ya nyakati, baada ya kutikisa nyavu mara tatu kwenye mechi hiyo
iliyofanyika leo huko nchini kwao.
Pak, alifunga mabao yake kunako dakika
za 8, 45 na 67, huku mabao mengine yakiwekwa nyavuni na Don Won Ji (66
na 85) pamoja na Jung Woo Kim, aliyefunga bao moja kunako dakika ya 82.
Yossi Benayoun amwaga wino Arsenal
Dilila kumsaini mchezaji huyo ambalo lilionekana kushika kasi saa chache zilizopita baada ya Arsenal kuelekea kumkosa Mikel Arteta, lilikuwa likiendeshwa kimya kimya sana ukiachilia mbali taarifa zilizokuwa zikitolewa na mchezaji huyo mwenyewe kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Haijawekwa wazi dau lake na lakini inaelezwa kuwa amesaini kwa mkopo wa muda mrefu ambao unaweza kugeuzwa kuwa wa kudumu na bila shaka hizi ni habari njema sana kwa mashabiki wa Arsenal ambao walichokuwa wakiangalia ni kuimarishwa kwa kikosi chao kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Benayoun mwenyewe amezungumzia usajili huo kwa ufupi sana katika ukurasa wake wa Twitter ambako ameandika “I sign with arsenal,very happy and excited about it,but now my head is only in the game against grecce on friday,thanks for the support”.
Je, ni nani atasaini dakika hizi takriban 20 zilizobaki? Ni Arteta, ambaye amelazimisha Everton wamuachie baada ya awali kukataliwa kwa maombi ya Wenger au basi ndio kocha huyo Mfaransa kafunga duka?
Sep 2, 2011
Timu ya Bonde fc inawatangazia kuwa kesho itacheza mechi ya nusu fainali katika uwanja wa Mwenge shouting
Kaptein wa Bonde fc Swalehe( Canavaro) amewahaidi mashabiki wa Bonde fc kuwa kesho lazima aingoze timu yake kutinga hatua ya fainali katika mechi ya nusu fainali itakayochezwa hapo katika viwanja vya Mwenge shoutting watu wote mnakaribishwa
AFRICAN LYON WASHINDWA TAMBA MBELE YA COASTAL UNION
AFRICAN LYON WAPOTEA CHAMANZI
African
lyon ya Mbagala wakiwa katika uwanja wa Azam uliopo Chamanzi jana
walitoka mikono mitupu baada ya Coastal union kunyakuwa point zote 3
katika muendelezo wa Ligi kuu ya Vodacom.
African lyon wakiwa wenyeji wa Coastal union ya Tanga ja walishindwa kutamba na kuwaruhusu wagosi kuondoka na ushindi wa goli moja bila, goli likifungwa na Salum Azizi Gilla katika dakika ya 20 ya mchezo.
Kutokana na Ushindi huo Coastal union imevikisha point 4 na kupanda mpaka nafasi ya 5.
MSIMAMO WA VPL.
Kwenye Mabano Idadi ya Mechi Zilizochezwa.
1. Toto Africa (4) 7
2. Simba SC (2) 6
3. JKT Ruvu (3) 5
4. Africa lyon (4) 5
5. Coastal Union (3) 4
6. Moro United (3) 4
7. MtibwaSugar (3) 4
8. Villa Squad (3) 4
9. Azam FC (2) 3
10. JKT Oljoro (2) 3
11. KageraSugar (4) 3
12. PolisiDodoma (3) 2
13. RuvuShooting (2) 1
14. Yanga SC (2) 1
African lyon wakiwa wenyeji wa Coastal union ya Tanga ja walishindwa kutamba na kuwaruhusu wagosi kuondoka na ushindi wa goli moja bila, goli likifungwa na Salum Azizi Gilla katika dakika ya 20 ya mchezo.
Kutokana na Ushindi huo Coastal union imevikisha point 4 na kupanda mpaka nafasi ya 5.
MSIMAMO WA VPL.
Kwenye Mabano Idadi ya Mechi Zilizochezwa.
1. Toto Africa (4) 7
2. Simba SC (2) 6
3. JKT Ruvu (3) 5
4. Africa lyon (4) 5
5. Coastal Union (3) 4
6. Moro United (3) 4
7. MtibwaSugar (3) 4
8. Villa Squad (3) 4
9. Azam FC (2) 3
10. JKT Oljoro (2) 3
11. KageraSugar (4) 3
12. PolisiDodoma (3) 2
13. RuvuShooting (2) 1
14. Yanga SC (2) 1
Subscribe to:
Posts (Atom)